UHURU JR
JF-Expert Member
- Jul 24, 2014
- 16,543
- 7,880
Hao watu unaosema waoga hivi walionesha kweli dalili za kukusudia kutaka kuandamana? Wakati polisi wanatoa mikwara humu mitandaoni watu wanasema lazima kieleweki wanaonesha hawaogopi chochote ila huko mtaani hakukuwa na dalili za watu kutaka kuandamana na ndio maana siku ya tukio watu waliamka na wakiendelea na shughuli zao huku mitandaoni(mliojifanya hamuogopi vitisho vya polisi) ndio mlikuwa mnasikilizia muone hayo maandamano wengi mkiwa nje ya nchi na wengine sio wale wa kuingia road. Hivi kweli utasema hapo tatizo ni uoga?Hiyo ya Lowassa kuwa aliongeza kura kila siku huwa napinga hapa maana ni uongo, aidha wa viongozi wa CDM kuficha kosa lao la kumpokea Lowassa. Ama ni upotoshaji wa wanaccm kutaka kuhadaa umma kuwa Cdm haikuwa na nguvu, bali ilitegemea nguvu ya Lowassa. Huwa ninawauliza wanaosema Lowassa alileta kura 6m+ na viti vingi vya ubunge na udiwani akiwa na miezi miwili, je alileta viti vingapi vya ubunge na udiwani akiwa na miaka miwili? Huwa nikifika hapo wote wanakaa kimya.
Narudia tena watu ni waoga hilo wala halina mjadala. Vitisho huwa tunaviona na sio jambo la siri. Watu kujaa kwenye mikutano ya CCM sio kwenda kusikiliza sera, bali wengi hufuata burudani, na shamrashamra zinazokuwepo kwenye mikutano ya CCM. Kama watu sio waoga, tusingeona wafanyakazi kutopandishiwa mishahara zaidi ya miaka 5, na kuishia kulalamika. Au huu mgao wa umeme na maji na watu wakawa wanalalamika tu. Labda kama una tafsiri tofauti ya uoga.
Hiyo watu kuwa waliogopa vitisho vya vyombo vya dola wala halina mjadala, labda kama utakwazika huu kuwa ndio ukweli. Tunakumbuka vitisho na magari ya vyombo vya usalama yalivyozunguka baada ya Mange kimambi na Tundu Lisu kutangaza maandamano. Labda kama tusingeona vyombo vya dola kisha watu wasiandamane ungekuwa na hoja.
Nchi hii haina upinzani serious na ina wananchi wajinga, hata hao wanaoshabikia hiyo cdm wala hata sio sera ndio walizovutiwa nazo ni muendelezo wa ujinga tu ndio maana Mbowe anafanya huo ujinga na bado watu huwaambii kitu wao wanaona Mbowe kuendelea kuwepo pale ni kuwakomoa ccm.