Mambo ya ajabu yamelighubika taifa letu. Umeme unakatika ovyo huku Waziri mwenye dhamana anadai kuna Megawatts 14000 za ziada

Hao watu unaosema waoga hivi walionesha kweli dalili za kukusudia kutaka kuandamana? Wakati polisi wanatoa mikwara humu mitandaoni watu wanasema lazima kieleweki wanaonesha hawaogopi chochote ila huko mtaani hakukuwa na dalili za watu kutaka kuandamana na ndio maana siku ya tukio watu waliamka na wakiendelea na shughuli zao huku mitandaoni(mliojifanya hamuogopi vitisho vya polisi) ndio mlikuwa mnasikilizia muone hayo maandamano wengi mkiwa nje ya nchi na wengine sio wale wa kuingia road. Hivi kweli utasema hapo tatizo ni uoga?

Nchi hii haina upinzani serious na ina wananchi wajinga, hata hao wanaoshabikia hiyo cdm wala hata sio sera ndio walizovutiwa nazo ni muendelezo wa ujinga tu ndio maana Mbowe anafanya huo ujinga na bado watu huwaambii kitu wao wanaona Mbowe kuendelea kuwepo pale ni kuwakomoa ccm.
 

Kwa taarifa yako mabadiliko sio lazima yaletwe na wasomi, au watu waelewa sana, bali ni jambo automatic toka kizazi kimoja hadi kingine. Unadhani hatukuona dhamira ya watu kuandamana, au kwakuwa wewe ulikuwa mitandaoni unasubiri kuona watu wakiandamana, na hukuona basi ni dalili kuwa watu hawakuwa tayari?

Kama watu sio waoga, mbona wafanyakazi hawajapandishiwa mishahara na wala hujaona migomo? Mbona huduma ya umeme inasumbua na watu wanashindwa kuzalisha, na huoni mtu akijigusa huko mtaani zaidi ya malalamiko huku mitandaoni?

Ukiona watu kama akina Mbowe wanafanya hayo na bado wanaungwa mkono, ujue watu wameichoka ccm, ila uoga ndio kikwazo.
 
Ni dhamira ipi ambayo watu walionesha ya kutaka kuandamana huko mtaani? Kwa sababu huku mitandaoni nakubali kweli dhamira mliionesha na kwenda mbali zaidi hamkuogopa hata mikwara ya polisi ila huku mitaani kwenye uhalisia hali haikuwa kama ilivyokuwa ya mitandaoni, sasa ajabu mnakuja na kisingizio cha uoga sijui mikwara ya polisi sijui magari yamefanyaje. Mimi naamini kabisa dhamira iliyokuwepo mitandaoni ndio ingekuwepo na huku mitaani basi pengine tungekuwa tumebadili historia damu ingemwagika.

Ujinga wa watanzania ni mtaji kwa vyama vya siasa ccm na cdm.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…