Mambo ya JF na zama zake

Mambo ya JF na zama zake

Mkuu naelewa hili hitaji la numbers ni muhimu sana Ila pamoja na yote, bado jf ni forum kubwa ukanda wa Afrika Mashariki na hata kwa Africa sidhani kama itakosa top 10 or 5

Kwa hiyo hatupo vibaya sana na kama watataka kuifikisha kwa audience kubwa zaidi. Nadhani ingefikiriwa namna ya kutambua na kuipata hiyo "right audience" Kwa sababu hawa wanaoharibu ni wengi lakini wanapunguza overall quality ya forum.

Kwa hiyo sidhani kama ni sawa sana kuharibu brand yako ili uwafurahishe watu wenye mchango mdogo kwa hadhi yako
Mkuu Eyce...

Hiki unachokieleza upo sahihi asilimia mia, nimependa mawazo yako chanya hakika ilikuwa ushauri mzuri sana kama ungeweza kuwafikia walengwa.
 
Miaka michache nyuma nilisema kuwa Jf inatakiwa kubaki na tag ya "where we dare to talk openly" Ila home of great thinkers badhaai Era yake ipo mwishoni na hivyo kulifanya jukwaa kutoakisi hicho kitu.

Natamani maxcence na mushi wangeweka quality control, mfano baadhi ya threads au forums ziruhusiwe kwa watu maalumu tu ambao wamekidhi vigezo flani kutokana na uwezo au haiba zenye ustaarabu wa kutoharibu mijadala.

Hao watu wawe kama panelists huku wengine wawekewe utaratibu aidha wa kuweka comments ndani ya comments pasipo kufanya interruption ya mada husika. Mfumo ambao upo kwenye Twitter spaces

Hii itasaidia intruders kutoharibu mijadala na hivyo kuwapa uwanda mpana zaidi wataalamu kumwaga madini yao pasipo dhihaka ama matusi ambayo yanawakatisha tamaa kiasi cha kususia mijadala hivyo, kukosa ile ladha ya mijadala bora ya jf.

Maxcence akumbuke tu, Jf ni user generated content ambazo ni za maandishi zaidi hivyo, wengi wanaoingia humu hawatarijii jazba na uzushi usio na mipaka kuliko hard facts.

Akiamua hali hii iendeleee pasipo kutafuta namna ya kuokoa hii hali ni wazi, jf itakosa ile ladha ama mvuto wake na hivyo kuchukuliwa kama social media platforms kama Facebook which is not right
Umeongea kama wewe ndio mmiliki WA Jamii Forum..au kama Una genge lako ambalo mkipost nyuzi hamtaki tusiwakosoe,ninyi ndio mnajifanya wajuaji...mnajiita akili kubwa

#Aibukwenu#

Sent from my SM-A047F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom