FaizaFoxy
Platinum Member
- Apr 13, 2011
- 100,246
- 123,145
Ahsante kwa taarifa, tutalifanyia kazi.Aunt siku moja nitakutembelea kwako.
Nitakutembelea kwako zingatia haya maneno.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ahsante kwa taarifa, tutalifanyia kazi.Aunt siku moja nitakutembelea kwako.
Nitakutembelea kwako zingatia haya maneno.
Never bro neverNyakati zinabadilika......
Members walikuwa wachache wakati huo, sasa members ni wengi ( kwenye Wengi pana mengi).
Na haya malalamiko sio JF pekee, ni kwenye Forum zote duniani.
Hata ukienda reddit pia wanalia same thing.
Hii inamaanisha nini?
Era yenu imeisha, kuliko kushinda mnalalamika kila siku ni Vyema mkastaafu pia au mka adopt.
Ila there is no going Back, itafika wakati hata sisi wa juzi tutakuwa hatufit kwenye mfumo.
We kantri huyo Lenie na Mwachiluwi ni pete na kidole wanapendana kinoma sasa hapo unapomwambia hivyo hawezi kukuelewa bro.Haukua na uzuri wowote, kulikua na unafki na kuogopana tu.
Machoko kweli walikuwepo, mmoja wao ni mwachuluwi confirmed 100%, nilikua nasubiri ajichanganye tu nimlipue
Kumbe ndo wewe🤣🤣🤣🙌... namsubiri Lovie Lady aje aseme neno hapa😂😂Ww ukitaka kujua fungua pm chap. 🤣🤣🤣🤣 Tena ww lile penzi lako na YE67NBE sijui liliishia wapi 🤭🤭🤭.
Sio mimi ww. Woiih demu mwenyewe ashapotea alipata bwana akasepa mazima harudi tena huyo. Anaolewa mwezi wa 1 huko. Yupo kwenye heka heka saiviKumbe ndo wewe🤣🤣🤣🙌... namsubiri Lovie Lady aje aseme neno hapa😂😂
Tatizo una I'd nyingi... nipe moja ya uhakika nikufollow nije unipe simulizi😃😎Fungua pm mchumba. Tena ww navyokupendaga 😘😘.
Ooh jamani... ndo uje sasa unisimulie movie hii hapa😂😂Sio mimi ww. Woiih demu mwenyewe ashapotea alipata bwana akasepa mazima harudi tena huyo
😀😀😀 Ntakupaje hadharani my wangu fanya kufungua ntakupea humo humo ndani. 😃😆Tatizo una I'd nyingi... nipe moja ya uhakika nikufollow nije unipe simulizi😃😎
Ndo ufanye haraka sasa, kabla mda wa church haujafika niwe nishatubu kabisa... umbea huu😂😂🤭😀😀😀 Ntakupaje hadharani my wangu fanya kufungua ntakupea humo humo ndani. 😃😆
Nenda misa ya 3. Mafile ni mengi 🏃🏃🏃 nakuja ❤️Ndo ufanye haraka sasa, kabla mda wa church haujafika niwe nishatubu kabisa... umbea huu😂😂🤭
Sawasawa... nimekaa vizuri kabisa kukusubiriNenda misa ya 3. Mafile ni mengi 🏃🏃🏃 nakuja ❤️
Kabla ya Faiza alikuwepo dada mmoja akiitwa WOS (Woman of substance). Yuko wapi?Wasalam,
Leo katika pitapita zangu humu jamvini nikakutana na andiko moja kutoka kwa member fulani (simkumbuki jina) akihoji ni muda gani watu wa jf hufanya kazi sababu wapo baadhi ya members (nikiwepo mimi mwenyewe) kila uchwao ni kukesha na kuzurula mitaa tofauti ya humu ndani, kiukweli nikajikuta kicheko kimenishika na kuacha kile nilichokuwa nikifanya.
Tabasamu likanivaa usoni pale nilipokumbuka namna uraibu huu uliponianza ni kama masikhara na leo JF imekuwa kama ulevi wa unga ama 'punyeto' rahisi kuingia na ngumu mno kutoka. Mathalani ikitokea nipo mahali kwenye shida ya mtandao ama kukosa huduma ya internet basi arosto ya kuingia kuperuzi jf huwa ni ya hali ya juu.
Nimefikaje huku?
Nakumbuka takribani miaka 10 nyuma kipindi cha 2010, 2011 niliingia mtandaoni na ku'search' dalili za ugonjwa fulani uliokuwa ukinisumbua, basi katika matokeo yaliyokuja ilikuwa ni jf na nyuzi zilizokuwa zikifanana na tatizo langu, na nilipata msaada mzuri kutoka kwenye maoni ya nyuzi hizo, huu ndio ukawa mwanzo wa kuifahamu na kuipenda JF, HOME OF GREAT THINKERS niseme tu hii jf ilikuwa jf kwelikweli, mada za kufichua maovu na makando kando ya serikali zilianzia humu, taarifa confidential zilimwagwa humu, harakati za kisiasa zilifanyika humu na members wengi niliowakuta kwa wakati ule walikuwa ni wale waandamizi walioanza na 'Jambo forum' 2006 ikiwemo viongozi maarufu wa kisiasa (hawa kwenye familia au koo ni kama kizazi cha kwanza kuzaliwa, ), basi na mimi nikatamani kuchangia lakini sikuwa member nilikuwa nikiingia kama guest user.
Basi 2012 mwishoni nakumbuka namimi nikajiunga rasmi kama GT na kuanza kutoa michango kwenye nyuzi mbalimbali, lahaula nikakutana na bibi kifimbo cheza huyu hana muda wa kuchangia mada husika yeye anapita kuhakiki muandiko tu hata mchango wako ukakosea neno moja au herufi mathalani kwenye 'r' ukaweka 'l' basi atakuja kukusahihisha na kukuachia comment yake "shuleni ulienda kujifunza ujinga??"
si mwingine huyu bali ni bi FaizaFoxy ,bi faiza alikuwa faiza kweli si huyu wa sasa wa mchongo, alijua kunikera ila alinisaidia kuwa makini na kuhakiki kila mchango nilioleta jukwaani. Ghafla baada ya kuingia 'mkulu' jiwe, masikini si wakamficha bi faiza wa watu (inasemekana alikuwa kwenye uangalizi maalumu huko kisiju)
Nikikumbuka nyakati hizo palikuwa na vita kubwa ikiendelea humu ndani vita ya diaspora a.k.a "wabeba box" wakiongozwa na rais wao Nyani Ngabu , "USA baby" dhidi ya wazalendo waliochagua kubaki kwa mtogole na kupigwa na jua la 'daresalama' nikikwambia vita elewa neno vita hii ilikuwa vita kweli kweli watu mapovu yalijua kuwatoka humu.
Nyakati za usiku ratiba ilikuwa ni "kula pilau" hii iliitwa "wakubwa tu" hakika bundle lilikuwa likinikatikia nyakati zote za usiku katikati ya kula pilau, pilau ilikolea minyama na viungo tele, sijui kwanini liliondolewa lile jukwaa. Waandamizi wa jukwaa lile nawakumbuka vizuri na baadhi bado wapo active hata kipindi cha sasa, sitawataja hapa.
Mara akatokea mganga wa kienyeji na mada zake za urozi hapa ndugu Mshana Jr hakuna mada nyingine aliyokuwa akianzisha kwa kipindi kile tofauti na uchawi, humu mpaka tukaanza kufundishwa kupaa usiku, sijui meditation za kibuddha jinsi ya kusafiri ukiwa umelala jamani si tukaanza kupractice, huyu mzee alishaanza kutuingiza chamani.
Jukwaa la historia hapa mzee wetu Mohamed Said alikuwa wamoto kutupa story za watoto wa kariakoo akina Abdulwaheed skyes na story za kunyimwa "utambuzi" katika historia ya uhuru wa tanganyika hapa hata kama umezaliwa daslam utajiona wakuja utahadithiwa mpaka historia ya majina mzizima, muhimbili n.K hakika jukwaa la historia lilifana.
Upande wa siasa napo ndugu rutashoba na shemeji yangu Pascal Mayalla nao hawakuwa nyuma hapa nadhani mayalla alikuwa bado hajaanza kupiga mapambio alikuwa akichachafya kweli watawala.
Udaku wa mjini wote ulikuwa chini ya warumi (rip) alipigwa vita mno humu lakini tutaendelea kumkumbuka kwa namna ya uwasilishaji wake wa kipekee na ulioburudisha.
Likatokea wimbi kubwa la nyuzi za kuingia "viwanja" ughaibuni kusaka green pasture hapa wakina Dr Matola PhD hawakuwa nyuma walimwaga sana nondo, hapo kabla hajawa dr phd wa sasa, nakumbuka huu upepo na mimi ukanipeleka mpaka "yuropu", watu waliunda mpaka magroup ya watsapp wengine walifanikiwa wengine wakaishia kupigwa ili mradi taflani.
Huu uteja wa kushinda jf hata tukiwa kwenye mihangaiko yetu haukuanzia leo na hii ni kutokana na umahiri wa wadau katika kuleta nyuzi zenye kuelimisha, kuburudisha n.K.
Heshima kubwa ziwaendee member waandamizi na waanzilishi wa platform hii, hakika tutaienzi.
Kichuguu Mwanagenzi
unakumbuka moments zipi ama nyuzi gani zilizokufanya ukawa mraibu wa jf?
Umeongea kama wewe ndio mmiliki WA Jamii Forum..au kama Una genge lako ambalo mkipost nyuzi hamtaki tusiwakosoe,ninyi ndio mnajifanya wajuaji...mnajiita akili kubwa
#Aibukwenu#
Sent from my SM-A047F using JamiiForums mobile app
Shukrani mkuu🙏🏽Mkuu Eyce...
Hiki unachokieleza upo sahihi asilimia mia, nimependa mawazo yako chanya hakika ilikuwa ushauri mzuri sana kama ungeweza kuwafikia walengwa.
JF ya sasa kama imenunuliwa na kikundi furani cha watu ambao hawataki kabisa habari zao zikaja humu kwa njia ya kuibua mijadala moderators wako busy kuhariri nyuzi za watu kwa kuzipa lugha nyepesi tamu yakuvutia wawekezaji wao wapo busy kuficha thread imekuwa ya hovyo hovyoHakuna shaka juu ya hilo. Na hiyo qty haikuishia kwa members tu, imekwenda mpaka kwa moderators.
Kuna moderators wa ovyo kabisa JF kwa sasa.
Hujaulizwa kaa kimyaKuna crew ikiingia kwenye uzi lazima tafrani zianze.
Sijaulizwa na nani?Hujaulizwa kaa kimya