Mambo ya JF na zama zake

Mambo ya JF na zama zake

Nyakati zinabadilika......
Members walikuwa wachache wakati huo, sasa members ni wengi ( kwenye Wengi pana mengi).
Na haya malalamiko sio JF pekee, ni kwenye Forum zote duniani.
Hata ukienda reddit pia wanalia same thing.
Hii inamaanisha nini?
Era yenu imeisha, kuliko kushinda mnalalamika kila siku ni Vyema mkastaafu pia au mka adopt.
Ila there is no going Back, itafika wakati hata sisi wa juzi tutakuwa hatufit kwenye mfumo.
Never bro never
 
Haukua na uzuri wowote, kulikua na unafki na kuogopana tu.

Machoko kweli walikuwepo, mmoja wao ni mwachuluwi confirmed 100%, nilikua nasubiri ajichanganye tu nimlipue
We kantri huyo Lenie na Mwachiluwi ni pete na kidole wanapendana kinoma sasa hapo unapomwambia hivyo hawezi kukuelewa bro.

Au hujui crew yake?. Utaja chekwa
 
Wasalam,

Leo katika pitapita zangu humu jamvini nikakutana na andiko moja kutoka kwa member fulani (simkumbuki jina) akihoji ni muda gani watu wa jf hufanya kazi sababu wapo baadhi ya members (nikiwepo mimi mwenyewe) kila uchwao ni kukesha na kuzurula mitaa tofauti ya humu ndani, kiukweli nikajikuta kicheko kimenishika na kuacha kile nilichokuwa nikifanya.

Tabasamu likanivaa usoni pale nilipokumbuka namna uraibu huu uliponianza ni kama masikhara na leo JF imekuwa kama ulevi wa unga ama 'punyeto' rahisi kuingia na ngumu mno kutoka. Mathalani ikitokea nipo mahali kwenye shida ya mtandao ama kukosa huduma ya internet basi arosto ya kuingia kuperuzi jf huwa ni ya hali ya juu.

Nimefikaje huku?

Nakumbuka takribani miaka 10 nyuma kipindi cha 2010, 2011 niliingia mtandaoni na ku'search' dalili za ugonjwa fulani uliokuwa ukinisumbua, basi katika matokeo yaliyokuja ilikuwa ni jf na nyuzi zilizokuwa zikifanana na tatizo langu, na nilipata msaada mzuri kutoka kwenye maoni ya nyuzi hizo, huu ndio ukawa mwanzo wa kuifahamu na kuipenda JF, HOME OF GREAT THINKERS niseme tu hii jf ilikuwa jf kwelikweli, mada za kufichua maovu na makando kando ya serikali zilianzia humu, taarifa confidential zilimwagwa humu, harakati za kisiasa zilifanyika humu na members wengi niliowakuta kwa wakati ule walikuwa ni wale waandamizi walioanza na 'Jambo forum' 2006 ikiwemo viongozi maarufu wa kisiasa (hawa kwenye familia au koo ni kama kizazi cha kwanza kuzaliwa, ), basi na mimi nikatamani kuchangia lakini sikuwa member nilikuwa nikiingia kama guest user.

Basi 2012 mwishoni nakumbuka namimi nikajiunga rasmi kama GT na kuanza kutoa michango kwenye nyuzi mbalimbali, lahaula nikakutana na bibi kifimbo cheza huyu hana muda wa kuchangia mada husika yeye anapita kuhakiki muandiko tu hata mchango wako ukakosea neno moja au herufi mathalani kwenye 'r' ukaweka 'l' basi atakuja kukusahihisha na kukuachia comment yake "shuleni ulienda kujifunza ujinga??"


si mwingine huyu bali ni bi FaizaFoxy ,bi faiza alikuwa faiza kweli si huyu wa sasa wa mchongo, alijua kunikera ila alinisaidia kuwa makini na kuhakiki kila mchango nilioleta jukwaani. Ghafla baada ya kuingia 'mkulu' jiwe, masikini si wakamficha bi faiza wa watu (inasemekana alikuwa kwenye uangalizi maalumu huko kisiju)

Nikikumbuka nyakati hizo palikuwa na vita kubwa ikiendelea humu ndani vita ya diaspora a.k.a "wabeba box" wakiongozwa na rais wao Nyani Ngabu , "USA baby" dhidi ya wazalendo waliochagua kubaki kwa mtogole na kupigwa na jua la 'daresalama' nikikwambia vita elewa neno vita hii ilikuwa vita kweli kweli watu mapovu yalijua kuwatoka humu.

Nyakati za usiku ratiba ilikuwa ni "kula pilau" hii iliitwa "wakubwa tu" hakika bundle lilikuwa likinikatikia nyakati zote za usiku katikati ya kula pilau, pilau ilikolea minyama na viungo tele, sijui kwanini liliondolewa lile jukwaa. Waandamizi wa jukwaa lile nawakumbuka vizuri na baadhi bado wapo active hata kipindi cha sasa, sitawataja hapa.

Mara akatokea mganga wa kienyeji na mada zake za urozi hapa ndugu Mshana Jr hakuna mada nyingine aliyokuwa akianzisha kwa kipindi kile tofauti na uchawi, humu mpaka tukaanza kufundishwa kupaa usiku, sijui meditation za kibuddha jinsi ya kusafiri ukiwa umelala jamani si tukaanza kupractice, huyu mzee alishaanza kutuingiza chamani.

Jukwaa la historia hapa mzee wetu Mohamed Said alikuwa wamoto kutupa story za watoto wa kariakoo akina Abdulwaheed skyes na story za kunyimwa "utambuzi" katika historia ya uhuru wa tanganyika hapa hata kama umezaliwa daslam utajiona wakuja utahadithiwa mpaka historia ya majina mzizima, muhimbili n.K hakika jukwaa la historia lilifana.

Upande wa siasa napo ndugu rutashoba na shemeji yangu Pascal Mayalla nao hawakuwa nyuma hapa nadhani mayalla alikuwa bado hajaanza kupiga mapambio alikuwa akichachafya kweli watawala.

Udaku wa mjini wote ulikuwa chini ya warumi (rip) alipigwa vita mno humu lakini tutaendelea kumkumbuka kwa namna ya uwasilishaji wake wa kipekee na ulioburudisha.

Likatokea wimbi kubwa la nyuzi za kuingia "viwanja" ughaibuni kusaka green pasture hapa wakina Dr Matola PhD hawakuwa nyuma walimwaga sana nondo, hapo kabla hajawa dr phd wa sasa, nakumbuka huu upepo na mimi ukanipeleka mpaka "yuropu", watu waliunda mpaka magroup ya watsapp wengine walifanikiwa wengine wakaishia kupigwa ili mradi taflani.

Huu uteja wa kushinda jf hata tukiwa kwenye mihangaiko yetu haukuanzia leo na hii ni kutokana na umahiri wa wadau katika kuleta nyuzi zenye kuelimisha, kuburudisha n.K.

Heshima kubwa ziwaendee member waandamizi na waanzilishi wa platform hii, hakika tutaienzi.
Kichuguu Mwanagenzi

unakumbuka moments zipi ama nyuzi gani zilizokufanya ukawa mraibu wa jf?
Kabla ya Faiza alikuwepo dada mmoja akiitwa WOS (Woman of substance). Yuko wapi?
 
Umeongea kama wewe ndio mmiliki WA Jamii Forum..au kama Una genge lako ambalo mkipost nyuzi hamtaki tusiwakosoe,ninyi ndio mnajifanya wajuaji...mnajiita akili kubwa

#Aibukwenu#

Sent from my SM-A047F using JamiiForums mobile app

Kama unaona ni sawa kwa mijadala inayohitaji akili kubwa kujadiliwa kwa uchama na ushabiki ni sawa pia. Ila mimi kwangu ni turn off

Kuna kipindi, jf ilikuwa ya moto, watu wanashusha nondo hadi unaona aibu kucomment kwa sababu huna cha kuchangia. Hiyo ndiyo ilikuwa Jf, home of great thinkers

Ila kwa sasa

"Mpumbavu wewe, huna akili, mama anaupiga mwingi, wewe chadomo au mboga mboga, huna unalolijua" Hadi wanaojua wanasusia mijadala

Sasa huo ni ukosoaji au upuuzi, kama wewe unaona sawa ni wewe Ila kwa wengine tunaopenda kujifunza hatuoni kama ni haki
 
Hakuna shaka juu ya hilo. Na hiyo qty haikuishia kwa members tu, imekwenda mpaka kwa moderators.

Kuna moderators wa ovyo kabisa JF kwa sasa.
JF ya sasa kama imenunuliwa na kikundi furani cha watu ambao hawataki kabisa habari zao zikaja humu kwa njia ya kuibua mijadala moderators wako busy kuhariri nyuzi za watu kwa kuzipa lugha nyepesi tamu yakuvutia wawekezaji wao wapo busy kuficha thread imekuwa ya hovyo hovyo

Leo JF uwezi ibua mjadala, mwananzego ukiona mjadala umetoka JF leo basi ni wao kwa wao viongozi wameamua chomeana si mwananzego
 
Back
Top Bottom