Mambo ya kisheria unayotakiwa kuyajua kabla haujaamua kumuoa Single Mother

Mambo ya kisheria unayotakiwa kuyajua kabla haujaamua kumuoa Single Mother

Kwenye sheria hazitumiki hisia, kinachoangaliwa ni kile kilichoandikwa kwenye vitabu. Hivyo maamuzi yoyote utakayofanya hata kama ni kwa nia nzuri lazima ujue kuna consequences zake. Kumbuka kwenye sheria hauwezi kujitetea kwa kusema "nilikua sijui"

Yafuatayo ni mambo ya muhimu kuyajua utakaamua kuoa au kuishi na single mother

1.Mtoto wa single mother sio mtoto wako na hatokua mtoto wako.

Haijalishi umejitoa, umeonyesha upendo au umeingia gharama kwa kiasi gani kwa ajiri ya malezi ya mtoto. Mama na baba mzazi ndio wenye haki ya mzazi wa mtoto. Suala la haki ya mzazi determinant factor ni biology. Emotional bond au mtoto kutumia ubini wako hivyo vitu havina uzito. Baba wa mtoto akiibuka muda wowote na kumtaka mtoto wake, hautakua na nguvu ya kumzuia wala kudai fidia ya gharama ya malezi ya mtoto ulioingia.

2.Hauwezi kuasili/adopt mtoto ambae baba ake yupo hai.

Hata kama baba mzazi amemtelekeza mtoto wake au ana ugomvi na mama mtoto. Hauna uhalali wa kisheria kumuasili mtoto ikiwa baba ake yupo hai. Unaruhusiwa ku-play nafasi ya baba kama kugharamia malezi, emotional support n.k lakini sio kumuasili/adopt mtoto

3.Utakapoamua kubeba jukumu la malezi ya mtoto wa single mother sheria itaendelea kukubesha ilo jukumu hata pale mtakapoachana.

Kwa masilahi ya mtoto na dhamira ya dhati ya serikali kumaliza tatizo la watoto wa mtaani, basi utatakiwa kuendelea kutoa gharama za malezi/child support hata mkiachana na mama mtoto. Kumbuka hiyo ni shurti kisheria, sio hiyali.

4.Baba na mama mzazi wana haki ya kujumuika pamoja katika kushirikiana malezi ya mtoto wao.

Hauna mamlaka ya kuwazuia kuwasiliana au kuonana. Hauna mamlaka ya kumzuia mama mtoto kumpeleka mtoto nyumbani kwa baba ake. Kitu pekee unachoweza kufanya ni kuzuia tu baba mtoto asije nyumbani kwako. Nje ya himaya ya nyumbani kwako hauna mamlaka ya kuzuia wala kuingilia interactions za wazazi wa mtoto hata wakiamua kukutana lodge. Ukifanya jaribio lolote la kuzuia kukutana kwao unaweza kushtakiwa kwa kosa la kuingilia faragha ya watu.

5.Safari yoyote na mtoto, baba ake anatakiwa kujua na kutoa ruhusa.

Mfano mmepanga trip ya kifamilia kwenda mkoani basi baba wa mtoto lazima apewe taarifa na atoe ruhusa ya mwanae kusafiri. Akikataa hakuna safari au mtatakiwa kumuacha mtoto nyumbani. Baba mzazi anatakiwa kujua kila sehemu ambayo mtoto wake anasafiri, kutompa taarifa anaweza kukufungulia mashtaka ya kumtorosha mtoto wake.

6.Kumuasili/adopt mtoto bila baba ake kujua ni child trafficking.

Ukiadopt mtoto ambae baba ake yupo hai na akajua na kukufungulia kesi utapandishwa kizimbani kwa mashtaka ya child trafficking.

Naomba niwatakie siku njema mababa wa kambo na vijana wote wenye wapenzi au wachumba ambao ni single mother.
Mbona harmonize ameweza jipe moyo kiongozi
 
Mkuu tafuta hela, yaani hela namaanisha.
Mtoto ukimgharamia kwa kila kitu huyo baba yake mzazi atakuogopa na mkeo ataku heshimu.
Ukitengeneza urafiki ndani ya familia ni rahisi sana kuishi na singo maza kwenye ndoa kuliko hao wa bikira mifukoni.
Kutafuta hela ni jukumu la kila mtu mzima, maana anawajibika kujihudumia mahitaji yake. Sidhani kama ilo ni jambo la kuhimizana. Kama mtu mzima unatakiwa kujua huo ni wajibu wako

Mada inaongelea masuala ya kisheria ambayo tunayapuuzia lakini yana consequences bila kujali ulikua na nia njema.
 
Single mother kwenye ujenzi wa familia kuna utata mwingi kama mume/waume zake wako hai. Hawa waishie kwenye uhusiano wa kimapenzi tu na si kwenye ndoa. Labda mwanaume ajitoe ufahamu na asiwe na wivu siku atakapoona mke wake anawasiliana na ex wake kuhusu mtoto wao
 
Shida ya singo maza ni historia zao, wengi wao wana utitiri wa maex, waliwahi kuishi kinyumba na hao baba wa watoto wao.

Mbaya zaidi muoaji wa huyo singo maza ukiwa simp baaasi ndio kwisha habari yako.

Singo maza ni mtaji kwa baadhi ya vijana maana ni kamserereko, ganda la ndizi hatoi huduma, hamuhongi anaahidi ndoa tu na tunda anapata.
Ila kama ni simp singo maza anakuua kwa presha ukiwa na miaka 20 tu.
Aisee🤔
 
Duh,

Hii noma sana, mke wako anakuwa wa watu tena??
Maana yake unakuwa mtumwa wa huyo mwamba wa mwanzo kabla yako.

Kwa maana hiyo ukivutiwa na singo mama ni bora uichape na kusepa upesi
Dah jamaa amegongelea misumari mizito sana hivi haya yana ukweli au jamaa anatutisha tu.
Mtoto unayemlea upewe kesi ya kumtorosha kweli
 
Duh,

Hii noma sana, mke wako anakuwa wa watu tena??
Maana yake unakuwa mtumwa wa huyo mwamba wa mwanzo kabla yako.

Kwa maana hiyo ukivutiwa na singo mama ni bora uichape na kusepa upesi
Ukiamua kuoa single mother lazima baba mtoto apate update ya kila kinachoendelea maana umehifadhi familia yake nyumbani kwako.
 
Kutafuta hela ni jukumu la kila mtu mzima, maana anawajibika kujihudumia mahitaji yake. Sidhani kama ilo ni jambo la kuhimizana. Kama mtu mzima unatakiwa kujua huo ni wajibu wako

Mada inaongelea masuala ya kisheria ambayo tunayapuuzia lakini yana consequences bila kujali ulikua na nia njema.
Umemsoma alichoandika matical? Sijamshauri kuhusu sheria bali ujenzi wa familia iliyo bora.
 
Back
Top Bottom