Mambo ya kisheria unayotakiwa kuyajua kabla haujaamua kumuoa Single Mother

Mambo ya kisheria unayotakiwa kuyajua kabla haujaamua kumuoa Single Mother

Wanawake mkaage tu kwenye ndoa zenu kama mume sio violent; as long as Mume Hana fujo, anawahudumia hata kama anafanya Umalaya wa chini chini!

Mnawafelisha sana watoto wenu!
Mambo ya usawa wa kijinsia hayo. Wanasema mume akicheat, na mke anacheat.

Ingawa sijawahi kusikia waumini wa 50/50 wakisema mwanamke akimpa hela mwanaume, na mwanaume atampa hela mwanamke.
 
Kuna mpumbavu mmoja kaoa kwa mbwembwe nyingi mama mwenye watoto wawili kila mtoto ana baba yake na hao mababa wapo hai wanatunza watoto wao waliaoachwa kwa bibi mzaa mama. Sijui huyo jamaa kama ana akili timamu siku mke wake atakapowasiliana na waume zake wa zamani, maana kuna sherehe za watoto shuleni zinazowataka wazazi wahudhurie. Huyo mama anaweza asihudhurie ili kulinda ndoa yake mpya isivunjike kama mume mpya ataona kuna ushirikiano wa mke wake na waume zake wa mwanzo. Ni mjinga sana huyo jamaa, ataoaje mke wa watu wawili?
Kuoa single mother kuna utata kidogo. Maana anakuja na vipengere vya mtoto na baba mtoto. Unaweza ukamchukua kwa nia njema lakini kuna consequences zake ambazo hazijali nia njema yako
 
Kuoa single mother kuna utata kidogo. Maana anakuja na vipengere vya mtoto na baba mtoto. Unaweza ukamchukua kwa nia njema lakini kuna consequences zake ambazo hazijali nia njema yako
hatujui huyo jamaa nini kimemsibu kwa huyo mke wake mwenye ex hasband wawili, jamaa anamdunda na mke amechoka kupigwa na anataka kumtoroka huyo fala arudi kwao. Jamaa anadai mke anaongeaongea sana na simu anazopigiwa na wanaume wasiofahamika. Manzi anadai alilipiwa mahari kubwa sana anavumilia tu manyanyaso maana akiondoka jamaa ataenda kudai arudishiwe mahari zake kitu ambacho wazazi wake hawana uwezo wa kurudisha hizo fedha za mahari
 
Kumbe kuna mambo ya kisheria?

Hata hivyo, hao ndio wanawake wazuri wa kuwaoa, Wamejifunza na wako tayari kucompromise. Ninyi hamshangai kwanini wanaolewa sana huku “inje”?

Mnajua jeuri inayokuja na mtu kutokuwa na baby daddy nyie? 😅

Vijana sitawafundisha kila kitu.
 
Mahari haina compensation. Kama anakutana na manyanyaso ya kupigwa ni vyema akaondoka tu hata kwa kutoloka.
 
Single mother sio wabaya, waishie tu kwenye urafiki wa kimapenzi hata kama watakuzalia mtoto, si wa kuishi pamoja kutokana na uwepo wa utata wa mahusiano na wazazi wenza wa awali. Ukizaa na single mother msaidie tu misaada yote anayohitaji ili aweze kutunza mtoto uliyezaa naye, maana huwezi kujua kama ma ex wake kama wanamchangia au hawamsaidii. Hakuna kuweka kambi pamoja kama una wivu na hauwezi kuvumilia kufanyiwa matukio ya kuchitiwa
 
Kumbe kuna mambo ya kisheria?

Hata hivyo, hao ndio wanawake wazuri wa kuwaoa, Wamejifunza na wako tayari kucompromise. Ninyi hamshangai kwanini wanaolewa sana huku “inje”?

Mnajua jeuri inayokuja na mtu kutokuwa na baby daddy nyie? 😅

Vijana sitawafundisha kila kitu.
Tatizo baby daddy lazima afanye doria nyumbani kwako, yaani ni kama yupo juu ya ghorofa na glasi ya mvinyo halafu anaangalia kila kinachoendelea nyumbani kwako huku akijua anaweza kuvuluga kila kitu kwa sms moja tu kwenda kwa baby mama wake.
 
Back
Top Bottom