safuher
JF-Expert Member
- Feb 11, 2019
- 12,312
- 18,194
Boding ni kumuua mtoto kitabia hasa hizi o level,bora umlee mwanao akifika advance hapo nadhani inaweza saidia na haitomuathiri akienda boarding.hawa ndio waende inapobidi
1.kama kakosa shule sehem unayoishi
2.Kama kapangiwa shule inayoleta changamoto ya usafiri
Mi nashangaa hadi leo imekua kama fasheni kupeleka watoto boarding.
tukianza na elimu ya msingi kiukweli sio haki kumpeleka mtoto boarding maana shule zipo nyingi sana na wazazi wa hiki kizazi wengi tumesoma, binafsi kila siku mtoto wangu lazima nimsaidie haya mambo ya shule za msingi maana hii ni elimu nyepesi mno kwa mtu mzima endapo alisoma. Huko boarding wanakosema kuna elimu nzuri ya shule ya msingi sijaona kipya.
Tukija sekondari shule za day zipo kibao tu na watu wanafaulu vizuri tu
Kwa form 5 wengi huwa washafikisha umri wa miaka 18 kidogo wanajielewa hivyo hata wakienda boarding au hostel iwapo wataenda chuo hakuna tatizo
Lakini katoto hata hakana nguvu ya akili ya kujiepusha na mabaya mtu anakapeleka boarding matokeo yake teenager inamchukua vibaya ukizingatia na makundi ya huko shule