safuher
JF-Expert Member
- Feb 11, 2019
- 12,312
- 18,194
Unawaza kama mimi mkuu.Peleka mtoto bwenini at your own risk and benefits.
Ila kwangu Mimi mtoto ataenda boarding akifika advance tu. Ni afadhali nimlipie pesa ya usafiri, nimpeleke tution za maana kipindi Cha likizo pamoja na kumnunulia vitabu atakavyohitaji. Ila Kila siku lazima nimuone Kila siku na kujua anaendelea vipi kimaadili, kidini na kimitazamo. Hata akiharibikiwa Basi iwe mikononi kwangu lakini siyo aje aseme Kama vijana wengi walioharibikiwa wakiwa boarding "ningekuwa nyumbani nisingefanyiwa vile, ona Sasa nashindwa kuacha hii tabia chafu"
Lakini pia kwangu Mimi maadili, utimamu wa mwili na akili, dini na uhusiano wa mtoto na Mimi ni Mambo ya muhimu kiasi kwamba hayana thamani inayolingana na kufaulu Sana kwa mtoto wangu kwa kumpeleka bwenini.
Mimi mtoto bora afeli lakini awe na maadili mazuri ya kijamii na mahusiano mazuri na mimi kuliko afaulu huku haoni thamani ya mimi baba yake kwa sababu tu muda mrefu sikuwa nae karibu.
Wazazi wengi hawajui kuwa kinachoweka ile strong bond baina ya mtoto na mzazi ni ule ukaribu katika maisha mnajadiliana na kuzungumza mambo mbali mbali