Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji849]Mi nilijamba wakati natongoza nilijua ni ile kitu cha yusuphuuu kumbe ni matarumbeta ya buza. Hahaa niliondoka bila kuaga!
Ndiyo mkuu mchana nilikula chapati na harage lililoungwa vizuriMkuu umetupia kitu cha maharage nn [emoji23][emoji23][emoji23]
Alafu huwa unatoka kimya kimya balaa[emoji23][emoji23]Mkuu inaonekana unajamba na kabla haijafika sekunde 10 unahama position kama sniper [emoji23][emoji23][emoji23]
Ushuzi wa mayai mixer maharage na mahindi kwenye bus masafa marefu unakuwa kama bomu.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23], sometimes gari kubwa au unapita mbele ya duka la CD sauti ya ushuzi inamezwa[emoji23][emoji23].Unasubiri bodaboda ipite unaunganisha, kitaalamu inaitwa "cross dissolve".
Huko kwetu mkoani Tanga wilayani Pangani kuna timu ya mpira wa miguu(football club) inayojulikana kwa jina Maskani fresh, almaarufu "Maskani mashuzi" hapo kuna wataalam wakujamba vijambo vya kila aina, kisha mjambaji anajikausha kama sio yeye vile, yaani hapo usijaribu kupita na Mzazi wako au mtu unaemuheshimu utajuta, Mara utasikia pyuuuuu!!! Mara prwaaäa!!!Mara tiiiiiiii!!! Mara utamuona baba mtu mzima kabisa anajiweka upande anakalia tako moja ghafla utasikia psiiiiiiii!!!! Yaani panakusidi hatari naukijifanya kuchukia ndivyo wanavyotaka. Ajabu mashuzi yote hayo hayana harufu kabisa.
Kwanini tunajamba? kwanini "ushuzi" unanuka? Kujamba inaweza kuwa kitendo cha aibu kwa wengi wetu,lakini inaweza kukufanya ujisikie vizuri kujua kwamba ni tendo la kawaida sana kwa mwili wa binadamu kutenda. Kila mtu anajamba,hata Sky Eclat nae hujamba.
1. Kujamba ni nini hasa?
Kujamba kunasababishwa na kubanwa kwa hewa,ambayo inaweza kutoka mwilini kwa njia nyingi. Baadhi ni hewa tuliyoimeza wakati wa kula au kunywa. Hewa ingine husababishwa na gesi kuingia kwenye utumbo wetu kutoka kwenye damu, na baadhi ya gesi huzalishwa na kemikali katika utumbo au bakteria.Kwa kawaida "ushuzi" unakua na asilimia 59 ya gesi ya nitrogen, asilimia 21 ni hydrogen, asilimia 9 ni carbon dioxide, asilimia 7 methane na asilimia 4 ni oygen.
Asilimia moja tu ya "ushuzi" inaweza kuwa hydrogen sulfide na mercaptans,ambayo ndio ina sulfur ndani yake,sulfur ndo hufanya "ushuzi" utoe harufu mbaya Kujamba huambatana na sauti,hii ni kutokana na "vibration" katika njia ya haja kubwa.Ukubwa wa mlio wa kujamba hutegemea "presha" inayosukuma gesi itoke nje na pia ugumu wa misuli ya njia ya haja kubwa.
2. Kwa nini Ushuzi hutoa Harufu mbaya?
Harufu mbaya ya ushuzi hutegemea na ulaji wa mtu, vyakula vyenye sulfur kwa wingi ndio husababisha hili. Vyakula vyenye sulfur kwa wingi ni kama maharage, kabichi, soda na mayai.
View attachment 1498819
3. Watu hujamba hadi mara 14 kwa siku
Mtu wa kawaida hutoa hata nusu lita ya ushuzi kwa siku 😂😂. Inasemekana mtu akijamba mfululizo kwa kipindi cha miaka 6,anaweza kuzalisha nishati ya kutosha kutengeneza bomu la atomiki.😎
4. Ushuzi husafiri kwa mwendo wa futi 10 kwa sekunde
Harufu ya ushuzi huanza kusikika sekunde 10-15 baada ya mtu kujamba,hiyo ni kwa sababu inachukua muda mrefu kwa harufu kufikia pua. (Kwa mtu mnene kama Kiduku Lilo inaweza chukua hata nusu saa😂😂)
5. Kujizuia Kujamba Inaweza Kuhatarisha Afya Yako
Madaktari hawajakubaliana moja kwa moja kama kujizuia kujamba ni hatari kiafya.Baadhi ya wataalam wanafikiri kujamba ni sehemu muhimu katika mfumo wa mmeng'enyo wa chakula,hivyo kujizuia kujamba haitakuletea madhara.Wengine wanadhani kwamba kujizuia kujamba kunaweza kusababisha tumbo kujaa gesi, na pia inaweza sababisha kikundu(hemorrhoids).
View attachment 1498820
6. Kwa Baadhi ya Tamaduni, Kujamba Sio Ishu
Wakati tamaduni nyingi zikichukulia tendo la kujamba lifanywe kistaarabu, kuna baadhi ya tamaduni hawaoni haya kujamba hadharani, na pia hufurahia tendo hilo. Mfano kabila la Yanomami huko America ya Kusini,kwao husalimiana kwa kujamba,na China unaweza kupata kazi ya kunusa ushuzi! Katika Roma ya zamani, Mfalme Claudius akihofia kwamba kujizuia kujamba inaweza kuwa hatari kiafya, alipitisha sheria kwamba ni ruhusa kujamba kwenye "banquets".
Swali kwako.
Je, ulishawahi kujamba sehemu ambayo ukahisi hukustahil kufanya hivyo iwe kwa bahati mbaya au kukusudia?
Hahahahahaha!!! Afya ya mduzi![emoji23][emoji23] Mku umenikumbusha jirani yetu mmoja kipindi chanyuma , aliku akiwaadhibu wanae wasiposema "afya ya baba" pindi anapojamba
Hahahahaha!!! Kombora lilipiga kinyume na matarajio!Mi nilijamba wakati natongoza nilijua ni ile kitu cha yusuphuuu kumbe ni matarumbeta ya buza. Hahaa niliondoka bila kuaga!