Mambo ya kutisha kuhusu Mamelod Sundowns "Masandawana"

Wagumu nyumbani, sio wanyonge ugenini

Mamelodi Sundowns ni miongoni mwa timu ambazo huwa sio rahisi kupoteza mechi kwenye uwanja wao wa nyumbani pindi inaposhiriki Ligi ya Mabingwa Afrika jambo linalochangia kuzipa presha timu nyingi ambazo huenda kukabiliana nayo.

Tangu ilipofungwa mabao 2-1 na CR Belouizdad, Aprili 9, 2021, hadi sasa imecheza mechi 16 mfululizo za Ligi ya Mabingwa kwenye Uwanja wa Loftus Versfeld uliopo Pretoria, Afrika Kusini bila ya kupoteza ikishinda mechi 12 na kutoka sare nne.

Lakini ubabe wa Mamelodi haushii kwa mechi za nyumbani tu bali hata ugenini imekuwa ikifanya vyema na kuthibitisha hilo katika mechi 10 zilizopita za Ligi ya Mabingwa Afrika, imefungwa moja, kutoka sare mbili na kuibuka na ushindi katika michezo saba.

BENCHI LILILOSHIBA

Mamelodi Sundowns ni miongoni mwa timu zenye rasilimali watu za kutosha kwenye mabechi yao ya ufundi ambazo zimekuwa chachu kwao kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali inayoshiriki.​

Timu hiyo ina jopo la wataalam 24 wanaohusika na idara ya ufundi wakiongozwa na kocha mkuu Rhulani Mokwena huku msaidizi wake akiwa ni Manqoba Mngqithi.​

KIKOSI GHALI

Kwa mujibu wa mtandao wa www.transfermarkt.com, thamani ya kikosi cha Mamelodi Sundowns kinachonolewa na Rhulani Mokwena wa Afrika Kusini ni Euro 33.15 milioni (Sh92.3 bilioni).​

Mchezaji ghali zaidi ni Matías Esquivel aliyenunuliwa katika dirisha dogo la usajili, Januari kwa ada ya Euro 2.3 milioni (Sh6.4 bilioni) kutokea Lanus ya Argentina.​

Nyota tegemeo wa Mamelodi Sundowns ni makipa Denis Onyango na Ronwen Williams, mabeki ni Rushine De Reuck, Mothobi Mvala, Grant Kekana, Abdelmounaim Boutouil na Khuliso Mudau.​

Viungo ni Teboho Mokoena, Thapelo Maseko, Gaston Sirino, Bongani Zungu, Marcelo Allende, Aubrey Modiba, Thembinkos Lorch na Junior Mendieta wakati washambuliaji ni Siyabonga Mabena, Abubeker Nasir na Peter Shalulile.​

Naishia hapo tu, msijekusema nawatishia maisha
Mamamamaaaaaa, Huyo BONGANI ZUNGU yupo, hilo jitu la miraba minne limepachikwa jina la "Mkata Umeme" ni hatari unaambiwa hilo jitu
 
Wydad si kabondwa kwenye final ya AFL? au unazungumzia wydad ipi? Mazembe si kapigwa kwenye makundi? Au habari huna??
Nazungumzia mechi za knockouts Wydad aliwafunga kwake, Mazembe aliwafunga pia kwake.

Kwenye knockouts Wydad msimu uliopita tu aliwachomoa kwa sare ya mbili mbili.

Ukiwashambulia defenders wao huwa wanafanya makosa mengi sana.

Timu ambayo haijazoea kushambuliwa sana weakness kubwa huwa kwenye centre backs hawawezi kuabsorb pressure ya mashambulizi ya mara kwa mara.
 
Wagumu nyumbani, sio wanyonge ugenini

Mamelodi Sundowns ni miongoni mwa timu ambazo huwa sio rahisi kupoteza mechi kwenye uwanja wao wa nyumbani pindi inaposhiriki Ligi ya Mabingwa Afrika jambo linalochangia kuzipa presha timu nyingi ambazo huenda kukabiliana nayo.

Tangu ilipofungwa mabao 2-1 na CR Belouizdad, Aprili 9, 2021, hadi sasa imecheza mechi 16 mfululizo za Ligi ya Mabingwa kwenye Uwanja wa Loftus Versfeld uliopo Pretoria, Afrika Kusini bila ya kupoteza ikishinda mechi 12 na kutoka sare nne.

Lakini ubabe wa Mamelodi haushii kwa mechi za nyumbani tu bali hata ugenini imekuwa ikifanya vyema na kuthibitisha hilo katika mechi 10 zilizopita za Ligi ya Mabingwa Afrika, imefungwa moja, kutoka sare mbili na kuibuka na ushindi katika michezo saba.

BENCHI LILILOSHIBA

Mamelodi Sundowns ni miongoni mwa timu zenye rasilimali watu za kutosha kwenye mabechi yao ya ufundi ambazo zimekuwa chachu kwao kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali inayoshiriki.​

Timu hiyo ina jopo la wataalam 24 wanaohusika na idara ya ufundi wakiongozwa na kocha mkuu Rhulani Mokwena huku msaidizi wake akiwa ni Manqoba Mngqithi.​

KIKOSI GHALI

Kwa mujibu wa mtandao wa www.transfermarkt.com, thamani ya kikosi cha Mamelodi Sundowns kinachonolewa na Rhulani Mokwena wa Afrika Kusini ni Euro 33.15 milioni (Sh92.3 bilioni).​

Mchezaji ghali zaidi ni Matías Esquivel aliyenunuliwa katika dirisha dogo la usajili, Januari kwa ada ya Euro 2.3 milioni (Sh6.4 bilioni) kutokea Lanus ya Argentina.​

Nyota tegemeo wa Mamelodi Sundowns ni makipa Denis Onyango na Ronwen Williams, mabeki ni Rushine De Reuck, Mothobi Mvala, Grant Kekana, Abdelmounaim Boutouil na Khuliso Mudau.​

Viungo ni Teboho Mokoena, Thapelo Maseko, Gaston Sirino, Bongani Zungu, Marcelo Allende, Aubrey Modiba, Thembinkos Lorch na Junior Mendieta wakati washambuliaji ni Siyabonga Mabena, Abubeker Nasir na Peter Shalulile.​

Naishia hapo tu, msijekusema nawatishia maisha
Hao ni wakawaida sana tu 😂
 
Back
Top Bottom