Kuna vitu vya kununua used ila fridge sikushauri,sisemi usinunue nunua kama anayekuuzia ni mtu mnaeheshimiana sana maana risks za kuikuta tofauti na matarajio yako ni nyingi mno.
Brother angu mwaka flani alifanya hiko kitendo,alijuta maana inafika home wiki tu ikazingua peleka kwa mpemba mpemba kamwambia iache ipitie jioni akaifikisha tena kwake siku ya nne imekataa tena akaipeleka tena ikirudi yale yale yaani ikifanya kazi muda mrefu ni wiki 3......
Alikaa akapiga hesabu zile route za kuitoa K/koo mtaa wa Uhuru hadi kwake Kibamba na kirikuu changanya na muda aliopoteza na vifaa alivyonunulishwa akakuta kumbe angeongeza 85,000/= tu angepata fridge mpya yenye ukubwa sawa na ile ile na siku iliposumbua tena akaibeba kuipeleka akaambiwa anunue compressor aliiacha huko huko akajichanga akanunua mpya dukani.
Wakati wa kununua hakikisha contract unayoingia na muuzaji inam'bana yeye maana wana kawaida ukiishawapa hela ukabeba zigo nakuambia hata ukija kesho yake asubuhi na mapema ukawaambia ina tatizo basi wataongea na wewe as if umekuja kuwaomba ushauri,yaani hawakujali kabisa!