Hii ni dangerous warning light. Inaonyesha computer ya gari yako ime-detect something wrong which need attention. Kuna vitu vingi sana vinaweza sababisha taa hiyo kuwaka. Baadhi yake ni kama hivi:-
- Evaporative Emmission Control System ina matatatizo (Mfano tenki lako la mafuta halina mfuniko au mfuniko wako haufungi vizuri, Catalytic converter ni mbovu, Charcoal Canister ni mbovu, nk
- Exhaust Gas Recirculation (EGR) system Failure (Mfano EGR valve imestark open au imestark closed, etc)
- Oxygen Sensor imefeli
- Crankcase Ventilation System imefeli
- Crankshaft Position Sensor imefeli
- Air fuel Mixture yako is too Rich au too lean (Hii ina maana kwamba mchanganyiko wa mafuta na hewa unaoingizwa kweye combustion chambers either una kiwango kikubwa cha mafuta kuliko hewa au una kiwango kikubwa cha hewa kuliko mafuta. Hii inaweza sababishwa na uchakavu wa nozzle au fuel filter imeziba kutokana na kujaa uchafu, nk
- Throttle Position Sensor imefeli na hivyo haipeleki signal sahihi kwenye computer ya gari
- Knock Sensor failure, etc
Kwa kifupi kuna mambo mengi yanayoweza sababisha CHECK ENGINE LIGHT iwake. Kuna baadhi ya gari inapowaka hiyo taa kuna error code number huwa inaapia kwenye dashboard kwa urahisi wa kufahamu tatizo. Aidha, kwa gari ambazo zinawaka taa peke, error code huwa inajirekodi kwenye computer ya gari na ili kuifahamu inabidi uipeleke gari garage ili computer ya gari iwe scanned na scan tool kuipata hiyo code na hatimae waweze kuitafsiri na kujua tatizo.
Sometimes ukichelewa kupeleka gari garage tatizo moja linaweza kuzalisha tatizo lingine na hivyo kupelekea zaidi ya error code moja being stored in the computer.
Mfano kama tatizo ni Nozzle/Injectors kushindwa ku-withstand fuel pressure na hivyo kuachia mafuta mengi kuingia kwenye combustion chambers kuliko inavyopaswa, kutokana na hali hii Oxygen sensor will detect moshi wako wa gari una-contain a lot of unburned fuel gases kwa muda mrefu na hivyo kupelekea taa ya CHECK ENGINE iwake. Kama ukichelewa kupeleka gari kwa fundi may be kwa zaidi ya wiki mbili maana yake utakuwa unaibebesha Catalytic Converter mzigo wa ziada wa kuharibu unburned fuel gases kwa kwa muda mrefu. Hali hii itapelekea Catalytic Converter kupata joto kali kwa muda mrefu na hatimae na yenyewe kufeli na mwisho na yenyewe error code yake kurekodiwa kwenye computer.
So unaweza kuta unatibu magonjwa mengi ambayo kimsingi yamesababishwa na gonjwa moja la awali. Na usipopata fundi mzuri kutibu magonjwa yote kwa mpigo unaweza shangaa ameteneza gari leo keshokutwa taa inarudi kuwaka tena.