Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Uchafu tuHivi kwann kuna kuwa na wadada wa hivi?! Me hii huwa nakutana nayo sana kwenye daladala, unakutana na mdada ananuka jasho la kichwa balaa yaani harufu ambayo ni kali kuvumilia.
Mara nyingi huwa ni kipindi cha jua kali. Au mvua imnyeshee halafu jua liwake muda huo huo.
Najijua nilivyo ndo mana nakwambia hivyousisema hutowahi mkuu! safari bado inaendelea.
Sijakataa ila kwangu hazifui dafu mana na mie zimetimia etiWew usiseme hivyo!!! Watu wana techniques nying za kula mzigo😁😁😁
.... ndio maana nasema tunza akiba ya maneno mkuu, watoto ni kwa vile hawapost ila nao wanaongoza kwa kula kimasikhara... itakuja kukukuta tu hata ya mtoto.Najijua nilivyo ndo mana nakwambia hivyo
Kimasihara siliwi mkuu
Ova🤣🤣🤣🤣
Haahaa,Wanawake hao.Halafu baadaye wanaanza kuomba asaidiwe mara hiki mara kile.
Mabasi yenye muziki, mhudumu /konda au dereva wasifungulie mziki sauti kubwa mno kana kwamba humo ndani ni Bar. Wazingatie kwamba kila abiria ana mambo yake kichwani yaliyomfanya asafiri na sio kuja kusikiliza muziki kwenye gari lao.1. Salimia unayemkuta kwenye siti maana hujui ya baadae. Inakera hukusalimia halafu baadae unaanza kuuliza "Eti hapa tumefika wapi?" 🙄🙄🙄
2. Kuwa mstaarabu unapoingia kwenye basi hasa kama tayari unajua siti yako haina haja ya kugombania mlangoni.
3. Sikiliza nyimbo na video za kwenye simu yako kwa kutumia earphones kwani kinachokufurahisha wewe kwa mwingine yawezekana ni kero.
4. Usiongee na simu kwa sauti kubwa hasa mambo yako binafsi kwani hakuna anayehitaji kujua mambo yako.
5. Kuwa mwangalifu unaposinzia epuka kumlalia jirani yako unaposinzia. Sambamba na hilo soma gazeti lako kwa uangalifu sio unalitandaza hadi linagusa pua ya mwenzako.
6. Usilazimishe kuchungulia dirishani kila mara wakati umekaa siti ya katikati, hiyo ni kero kwa aliyekaa dirishani.
7. Kama unasafiri na watoto wakatie siti yao isiwe kero kwa jirani yako. Unasafiri na watoto watatu kwenye siti moja ni kero kwa jirani yako na kwa watoto.
8. Usipake pafyumu kali za kukereketa wenzio. Sambamba na hilo piga mswaki vizuri ni kero kukaa na abiria anayenuka mdomo hasa anapokusemesha.
9. Msome abiria uliyekaa naye kama hapendi kusemeshwa usimsemeshe semeshe, mwache, wengine wana mambo yao kichwani, wengine wanaenda kwenye misiba, wengine wamefukuzwa na waume zao huko walikotoka, sio kila mtu anapenda kuongea safarini.
10. Kama unajijua una tatizo la kutapika safarini jiandae mapema kwa kuwa na vifaa vya kukusaidia kwenye hali hiyo.
Ongezea la kwako hapo kama unalo.
Hii naomba iwe namba moja 😂😂😂11. Usitongoze au kulazimisha kupewa namba ya jirani yako
Hao wasukuma ndio kiboko 😂😂ndoo ya majiYani ndio Bus linatoka mule Mbezi Louis kuitafuta Morogoro road, mama na mtoto waliokaa pembeni yangu wote kwa pamoja wakaanza kutapika. Dakika sifuri tu nimepakwa matapishi dadek.
Sijawahi kusafiri kwa raha mimi.
Enzi za Mohammed trans, natoka kanda ya ziwa kuitafuta Dar. Kuna wabibi ndani ya bus wanasafiri na wajukuu wao wadogo sana kiumri. Mmoja kati yao akaachia uharo kwenye corridor zile za katikati ya siti. Bus zima tulitafutana kwa hiyo harufu yake!
Mara nyingine tena natoka Dar kwenda Kanda ya Ziwa, ndani kuna familia ya hawa ndugu zetu wasukuma. Yani mmoja amekaa siti ya nyuma kabisa, anapiga story na mwenzie aliekaa siti ya katikati ya Bus. Walipanda na ndoo ndogo ya maji ya kunywa, wanachota kwa kikombe then wanapasiana kutoka nyuma mpaka katikati. Siku hiyo kabila lote la wasukuma lilinikwaza!
Mara ya mwisho nimepanda Bus, siti ya pembeni akakaa mzee mmoja hivi. Asee mzee alikua ananuka tumbaku sijawahi ona. Kila watu wakishuka kula na kuchimba dawa, yeye anashuka kuvuta tumbaku zake. Nilifika kwa tabu sana wakuu!
😂😂😂😂Hivi Muha Yale yupo kweli?wiki hii sijakutana nae kabisa au kaanza kutulia
Ulimpa dozi ya uhakika, katulizana😂😂😂😂Hivi Muha Yale yupo kweli?wiki hii sijakutana nae kabisa au kaanza kutulia
😂😂😂Sema tuliunganisha nguvuUlimpa dozi ya uhakika, katulizana
Mwenzangu wewe ni Kiboko yake ujue😂😂😂Sema tuliunganisha nguvu
Tuendelee kumuonya anapokoseaMwenzangu wewe ni Kiboko yake ujue