Mambo ya kwa Babu LOLIONDO

sio siri dawa ya babu wa loliondo imenifunza mambo mengi sana kuhusu tanzania na watanzania.mungu bariki.
 
Afande pia ni binadam kama sisi na kama ni maradhi hata yeye anaweza kuwa nayo,big up afande kwa kuokoa maisha yako huku ukiwaacha watu wanashangaa.
 
kinachonisikitisha ni uvivu wa waandishi wetu katika kazi zao za kiandishi.hawana uwezo wa kufanya investigative jouarnalism.

Waandishi mnaosoma hii thread nendeni loliondo fuatilieni mgonjwa ambaye ameacha dawa za hospitali na kunywa dawa ya babu halafu subirini siku 14 muende naye hospitali kufanya vipimo na hapo mtatupa jibu kamili kama babu anatibu au la.acheni kudakia minong'ono ya mtaani na kuifanya ndio headline ya habari zenu,umizeni vichwa!
 
Big up kwa sana mkubwa.Hiyo itakuw imekaa vizuri sana na sio kil kitu ni habari ila inawez kuw ni taalifa 2.Kwa mfan unakut Mwandishi wa habar anaish Morogoro harafu anatak kutupatia Habar za Babu wa Loliondo na wakat loliondo penyew hajawah hat kufika.Basi kinachofanyik ni kupig simu kwa marafik zak waliok huk loliondo na kupashwa taarifa tu juu juu na yey kuichukua hiy taarifa kam Habari.Hivyo anakuw hajatoo ule uhalisia wa habar unavyotakiw kuwa.
Simba kaua mtu hiyo sio habari ila mtu kaua simba hiyo ni habari ya kusisimua zaidi.
 

Napenda kuchangia kidogo, ni kweli waandishi wameshindwa kututhibitishia kwa ushahidi matokeo ya babu wa Loliondo, jambo ambalo naamini halihitaji msaada wa interpol kuthibitisha,

nikirudi kwako ntobistan, mfano wako sio relevant na mada inayozungumzwa.

Kwanza simba kuua mtu bado ni habari, ingawa mtu kuua simba ni habari zaidi,
labda ungesema mbwa kuuma mtu si habari, ila mtu kuuma mbwa ni habari.

lakini pia kinachozungumzwa hapa ni waandishi kushindwa kufuatilia habari mpaka kujua mwisho wake. ili kukidhi haja ya wasomaji bila kuacha kiu majibu, kama alivyosema mtoa mada, wangeweza tu kumfuatilia mtu mmoja tangu anakunywa dawa na matokeo yake baada ya vipimo vya kisasa, jambo ambalo ni rahisi tu kwa mwenye nia ya kufanya hivyo.

I hope nimejieleza vizuri
 
Ni vizuri kweli kufanya hivyo unavyoshauri lakini sidhani kama ulipaswa kulaumu kwanza. Unajuaje kuwa hawafanyi hivyo kwa sababu hizo wiki mbili hazijapita (namaanisha tangu huu buzz ya hivi karibuni kuhusiana na babu ianze). lakini tusubiri tuone
 
Ni vizuri kweli kufanya hivyo unavyoshauri lakini sidhani kama ulipaswa kulaumu kwanza. Unajuaje kuwa hawafanyi hivyo kwa sababu hizo wiki mbili hazijapita (namaanisha tangu huu buzz ya hivi karibuni kuhusiana na babu ianze). lakini tusubiri tuone


Habari za tiba ya bau zilianza tangu mwaka jana ila hivi karibuni ndio zimetapakaa zaidi.
 
Ni vizuri kweli kufanya hivyo unavyoshauri lakini sidhani kama ulipaswa kulaumu kwanza. Unajuaje kuwa hawafanyi hivyo kwa sababu hizo wiki mbili hazijapita (namaanisha tangu huu buzz ya hivi karibuni kuhusiana na babu ianze). lakini tusubiri tuone

babu wa loliondo ameanza kufanya miujiza yake kuanzia mwezi wa 8 au kabla mwaka 2010,kwa sasa kuna wagonjwa wengi wameshatimiza masharti na inawezekana kuwafuatilia kama tiba imefanya kazi au la.kuhusu kuwalaumu waandishi naona ni sawa kwasababu they giving very cheap news,kila taarifa utasikia "wananchi watoa maoni yao" au "mh waziri kasema"
 
siasa wamwachie nani kila siku ni kikwete na dowans bora umewaambia na huko wanakwepa sababu hakuna mshiko
 
Nimepita kwenye facebook ya mwandishi mmoja anajisifu kuwa wao kule hawafuati habari wanafuata dawa na wanatumia taaluma yao kuweza kupatiwa huduma mapema ilinisikitisha sana inaonyesha ni kiasi gani tz uzalendo umetoweka
 
Hakuna jinsi we unaumwa hafu ujifanye mbabe si itakukula kwako?
 
Maaandiko yametimia mkuu hakuna intelijensia kila ulimi utakiri na kila goti litapigwa///// thanks sana
 
ndugu zanguni nashauri wenger aende loliondo maana si bure hata kidogo
 
yule mzee iko gonjwa mkuu...nadhan dawa ya babu wa loliondo inaweza mwondolea mikosi
 
aliota makombe 4, sasa limebaki moja nalo ni tia maji tia maji.

Ameshindwa ku prove kwa dunia kwamba " Soccer is not Money" and "Soccer is not about maturity" na ndiyo maana ana timu ya vitoto vya shule - under 24.

Morinho alishamwambia wenger " You will never win anything using those school boys".

Habari ndiyo hiyo unune usinune.
 
Nimeupata ujumbe huu toka kwa mtumishi wa Mungu aliye uweka katika gazeti la mwananchi,kiimani tunaambiwa tuamini chochote kilicho katika kitabu Kitakatifu (biblia),...huyu babu yuko kinyume kabisa na biblia,.....tusikimbilie huko,na kama hatujaona huzi ni nyakati za mwisho!!


Tunaishi nyakati za mwisho.
Neno la Mungu linasema waziwazi kuwa nyakati za mwisho zitakuwa ni siku za hatari, hatari kubwa inayomaanishwa hapa ni watu kujitenga na imani na kufuata roho zidanganyazo – 1Tim. 4:1.

Biblia pia inasema, nyakati hizi za mwisho watatokea makristo wa uongo, na manabii wa uongo, nao watatoa ishara kubwa na maajabu; wapate kuwapoteza, kama inawezekana, hata walio wateule – Mt.24:23-24.

Ibilisi anahangaika kuwapeleka watumishi wake wengi kwa lengo na kuwavuta na kuwapoteza watu wasikae katika mapenzi ya Mungu, ili hatimaye wakataliwe na Mungu. Kwa sababu hiyo basi, tunapaswa kuwa makini sana na mambo yote yanayotokea nyakati hizi.

Kwa sasa hivi, kwa sababu kanisa bado halijanyakuliwa , mpinga kristo bado hajafunuliwa. Lakini roho yake tayari inatenda kazi.
Neno la Mungu linasema kuwa kutenda kazi kwa roho ya mpinga kristo kunaambatana na ishara na ajabu za uongo ili kuwavuta na kuwapoteza wanadamu – 2Thes. 2:7-12, Uf.13:11-14.

Kwa hiyo ndugu zangu, tunapaswa kuwa makini sana katika kila jambo, tusiwe wepesi wa kuchulikwa na kila upepo unaovuma. Hata kama mtu atasema kuwa anatumiwa na Mungu, bado hatupaswi kuwa wepesi wa kukubaliana naye. Kumbuka Yesu alisema wengi watasema siku ile bwana bwana tulifanya miujiza kwa jina lako naye atasema ondokeni sikuwajua ninyi kamwe.

Ninaposema hivyo simaanishi kuwa miujiza yote inatokana na ibilisi, iko miujiza mingi tu inayotokana na Mungu mwenyewe na haina tatizo kabisa.

Kitu cha msingi hapa ni kuwa tunapaswa kuwa na uwezo wa kutofautisha kipi ni kipi ili tusiingie kwenye mtego wa ibilisi.

Mungu wetu ametupa nafasi wa kuyapima na kuyajaribu mambo yote ili tuweze kutofautisha – 1Thes. 5:20-22, hatupaswi kuudharau unabii wowote bali kwanza tunapaswa kuupima na kuona kama unatoka kwa Mungu au la. Ikiwa ni wa Mungu tutaushika, la sivyo tutautupilia mbali.

Tunaupima unabii kwa namna gani?

Ni kwa kutumia Neno la Mungu pekee.
Biblia inasema katika Isaya 8:20 kuwa ikiwa watu hawaendi sawasawa na Neno la Mungu, kwao hakuna asubuhi. Asubuhi inamaanisha nuru, na kinyume cha nuru ni giza na giza maana yake ni dhambi. Chochote kile ambacho hakipo sawasawa na Neno la Mungu ni giza, ni dhambi.

Tena Neno la Mungu linasema katika 2Kor.13:8 kuwa hatuwezi tukafanya jambo lolote lililo kinyume na kweli ya Neno la Mungu.

Kuna alama zinazoweza kutusaidia kutambua miujiza ya Mungu.

I. Ishara na miujiza ya Mungu inaambatana na hao waaminio – Marko 16:17-18, Luka 10: 17-20. Waaminio ni wale waliompokea Yesu na kumfanya kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yao, ni wale waliookoka. Kama mtu hajaokoka kamwe hawezi akatumiwa na Mungu kufanya ishara yeyote. Swali jepesi sasa, huyu babu wa Loliondo ameokoka? (anajua babu mwenyewe yuko upande gani lakini hatu muhukumu kwa hili)

II. Ishara na miujiza huthibitisha Neno la Mungu linalohubiriwa – Marko 16:20. Tujiulize, huyu babu anahubiri Neno lolote la Mungu au anagawa dawa tu? Tukumbuke kuwa Mungu wetu anataka kwanza watu wapone roho zao kabla hata ya kuwaza kupona miili yao. Ndio maana akasema utafuteni kwanza ufalme wa mbinguni na mengine mtazidishiwa. Hata kama mtu atapewa hiyo dawa akapona lakini lazima iko siku atakufa tu, sasa akifa atakwenda wapi? Ndio maana Mungu nahitaji kwanza roho zetu zipone. Huyu babu ni sawa na mganga wa kienyeji tu, hana injili yeyote anyohubiri. Anawaza kuponya miili tu wakati Mungu anahitaji tuanze kwanza kuponya roho zetu.

III. Miujiza ya Mungu wa kweli lazima ifanyike kwa jina la Yesu tu – Marko 16:17, Luka 10:17, Mdo. 3;1-10. Miujiza ya Mungu haifanyike kwa kutumia mizizi ya miti, ni kwa Neno, ambaye ndiye Yesu Kristo.

IV. Neno linalohubiriwa lazima liwaongoze watu kutubu dhambi zao ili wamgeukie Mungu wao – Mdo. 3:19. Sasa pale Loliondo mmesikia kama watu wanatubu dhambi zao na kumrudia Mungu wao au wanapewa dawa tu. Hakuna Mungu hapo, ni uganga tu ndio unaoendelea hapo.

V. Toba ya kweli lazima iwaelekeze watu kwa Yesu – Hes. 21:4-9, Yoh. 3:14-15

VI. Mungu hulituma Neno lake ili kuwaponya watu – Zab. 107:18-20. Mungu anaponya kwa Neno tu, sio kwa mizizi ya miti au chochote kile.

VII. Yesu Kristo alipokuwa anawatuma wanafunzi wake kwenda kuhubiri na kuponya magonjwa aliwaagiza kuwa “mmpewa bure toeni bure” – Mt. 10:8. Sasa mambo ya watu kutoa mia tano yanatoka wapi sasa? Uzima wa Mungu ni bure kabisa, hakuna biashara yeyote inayofanyika, ni karama ya Mungu tu. Kinachoendelea Loliondo hakipo kabisa katika mapenzi ya Mungu, hata kama duniani nzima ingelihamia hapo.

VIII. Karama za Mungu haziwekwi kwa mtu mmoja tu, dunia hii ni kubwa na Mungu hawezi akaweka mtu mmoja tu kwa ajili ya kazi yake – 1Falme 18:20, 19:18. Yule babu kusema kuwa ni yeye peke yake aliyechaguliwa na Mungu kuleta uponyaji, huu ni uongo ulio wazi kabisa, hayo ni masharti ya waganga wa kienyeji kabisa. Karama za Mungu wa Biblia zinaambatana na kuwafundisha wengine jinsi ya kutumiwa na Mungu kama Yesu alivyofanya, sio mtu mmoja tu. Tena, karama za Mungu hazifungiwi na sehemu moja tu. Eti dawa itolewe hapo kijijini tu, hayo ni masharti ya mizimu tu, Mungu hayupo hapo. Yesu alisema enendeni ulimwenguni wote, sio mkae kwenye kijiji kimoja ambacho hata hakifikiki kirahisi – Marko 16:15

Ndugu zangu, nawasihi kwa jina la Bwana na mwokozi wetu Kristo Yesu, tusiwaze tu juu ya uponyaji wa miili yetu na tukasahau uponyaji wa roho ambao ndio wa muhimu zaidi. Hata kama tukipona leo, iko siku tutakufa tu. Kwa hiyo lolote tunalolifanya leo ni muhimu tuhakikishe kuwa linakubalika mbele za Mungu wetu.

Suala hapa sio kupona tu, lakini lazima tujue huo uponyaji unatoka wapi. Wagonjwa wengi tu wa ukimwi na magonjwa mengine sugu wameshapata kuponywa kwa njia ya maombezi tu katika jina la Yesu, lakini ajabu ni kwamba habari zao hazikuvumisha kama hili la Loliondo. Wakati wote imekuwa ni vigumu sana kwa vyombo vya habari kutangaza habari njema kama hizo zinatokea makanisani kwa sababu ibilisi hataki watu waufahamu ukweli huo. Hata zinapotangazwa bado, mwitikio unakuwa ni mdogo sana. Lakini hili kwa kuwa ni la kwake mwenyewe ibilisi ndio maana limepigiwa kelele na vyombo vyote vya habari, hata na viongozi wa ngazi mbalimbali serikalini wamekuwa mstari wa mbele kulishabikia na kulienzi. Ni kama upepo fulani unawachukua watu wote bila kujijua na kila mtu anawaza kuwahi kunywa hiyo dawa tu. Tusiwe hivyo ndugu zangu, bali tutafakari na kuyapima yote kwa Neno la Mungu.

Mwisho, Mungu akubariki sana na washirikishe wengine ujumbe huu.

Note:Being an anti-christ does not only mean being against christ,but also imitating to be like christ
 
Reactions: len
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…