Mambo ya mazoea ambayo yakageuka kuwa kama sheria

Mambo ya mazoea ambayo yakageuka kuwa kama sheria

Mkuu ulishawahi kufanya kazi ambayo pesa yake ulishakula tayari? Yaani unahisi kama unafanya kazi bure.
Hivyo ndivyo huwa nahisi nikianza na nyama, happy ending ni muhimu so mimi nyama ni lazima ziwe za mwisho.
😀😀😀😀😀
Huwa napata raha sana na napenda ile ladha navyo saga nyama na wali zikiwa mdomoni.
 
Kuwapigia watu simu hata kama hauna cha kuwaambia ili uonekane unawajali sana
Hii hufanyika sana hasa pale muda wa kifurushi unakaribia kwisha na bado kuna dakika nyingi. Ukipigiwa unafurahi kumbe yeye alikuwa anaokoa dakika zake zisimezwe bure.
😀😀😀😀😀
 
1. Chai na chapati mbili; yaani ukiwa mgahawani ukiagiza chai na chapati moja au zaidi ya mbili watu lazima wageuke kukuangalia, ni kama wamesikia wewe una ugonjwa wa corona bile.

2. Ukikaribishwa chakula sehemu ni lazima ukatae katae kidogo, wakikukazania kidogo ndipo unaenda kula; yaani ukaribishwe mara moja tu na uende kula! Hata aliyekukaribisha lazima ajiulize maswali, na kama alikukaribisha kwa kutania ni lazima ajutie kauli yake.

3. Mwanaume na mwanamke wanapolala kitanda kimoja, mwananamke lazima alale upande wa ukuta; yaani ikitokea mwanaume ukalala upande wa ukuta unajihisi kama umelala selo vile. Kwanza mwanaume unaanzaje kulala upande wa ukutani!??

4. Wali na maharage; binafsi huwa nikila wali ambao hauna maharage hua naona huo mchele umepotea bure kabisa.

5. Mgeni akija nyumbani akitaka kuvua viatu unamwambia haina haja ya kuvua viatu, aingie navyo tu. Najua wengi huwa hawamaanishi na kama wageni wakiingia na viatu ndani huwa wanaumia kimoyomoyo.

6.

7.
100% true [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Watu kutohoji vitu vya msingi kwenye timu au wasanii anao wakubali mf km mt ni shabiki wa yanga atawapongeza tu kwa chochote hata kama ni kibaya au km n shabiki wa Kiba atampongeza Kiba na Kumponda mond pasipo hoja ya msingi mradi aoneshe chuki au dharau
 
Kuna lile kochi linakuaga spesho kwa ajili ya baba, akiwepo hakalii lingne tofauti.
Hata ukiwa umekalia, ukimskia tu anarud bas automatically unajikuta ushanyanyuka umehamia kochi lingine
Sio tu kochi, unakabidhi na remote ya Tv..
Mzee bhana [emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom