1. Chai na chapati mbili; yaani ukiwa mgahawani ukiagiza chai na chapati moja au zaidi ya mbili watu lazima wageuke kukuangalia, ni kama wamesikia wewe una ugonjwa wa corona bile.
2. Ukikaribishwa chakula sehemu ni lazima ukatae katae kidogo, wakikukazania kidogo ndipo unaenda kula; yaani ukaribishwe mara moja tu na uende kula! Hata aliyekukaribisha lazima ajiulize maswali, na kama alikukaribisha kwa kutania ni lazima ajutie kauli yake.
3. Mwanaume na mwanamke wanapolala kitanda kimoja, mwananamke lazima alale upande wa ukuta; yaani ikitokea mwanaume ukalala upande wa ukuta unajihisi kama umelala selo vile. Kwanza mwanaume unaanzaje kulala upande wa ukutani!??
4. Wali na maharage; binafsi huwa nikila wali ambao hauna maharage hua naona huo mchele umepotea bure kabisa.
5. Mgeni akija nyumbani akitaka kuvua viatu unamwambia haina haja ya kuvua viatu, aingie navyo tu. Najua wengi huwa hawamaanishi na kama wageni wakiingia na viatu ndani huwa wanaumia kimoyomoyo.
6.
7.