princess ariana
JF-Expert Member
- Aug 19, 2016
- 9,245
- 18,347
Yani ile sauti ya pyeee pyuuu! Ni kichefuchefu sanaVipi kama akitumia leso (handkerchief)??
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Yani ile sauti ya pyeee pyuuu! Ni kichefuchefu sanaVipi kama akitumia leso (handkerchief)??
Hata refa akiwa anachezesha mechi unakereka kisa anapuliza kipenga siyoYani ile sauti ya pyeee pyuuu! Ni kichefuchefu sana
Hakika....wapo wawaonao ndugu zao ambao hawajafanikiwa kama hawana akili na kuekti wanampenda Mungu sana... kumbuka usipompenda ndugu yako unayemuona utampendaje Mungu usiyemuona... mnafiki wewe...kutokumjali ndugu yako ni kumchukia dhahiri....wapo wasiopenda hata kuwasiliana na ndugu zao na akijua una namba yake anabadilisha nyingine.... wanafiki wakubwaUkibahatika kupata maisha mazuri usisahau ulikotoka, kwenye maisha kuna kupanda na kushuka.
Kuna kipindi kilikuwa kinarushawa TBC cha bongo Dar es Salaam kinaonyesha matukio ya wizi ,kinarudi tenah ITV kwanzia wiki hii Jumapili,ukikifatilia vizuri kile kipindi utanielewa vizuri kwann mm nakusihi usiondoke stationary kwa mawazo yangu ...unaweza ukapigwa kote kote ww jiamini Tu Baki ndani ya ofisi kama mfalmeUkienda stationary kutoa photocopy au kazi yoyote ile, kisha mhusika akatoka nje kwenye kufanya jambo lolote kama vile kutafuta chenchi, basi na wewe Toka ukae nje. Usibaki mule mule ndani kwa maana kuna kitu kinaweza kupotea kisha wakasema kuwa ni wewe ndiye uliyekichukua.
Hapana mkuu. Busara ni kukaa nje ya ofisi ya mtu kama mhusika hayupo.Kuna kipindi kilikuwa kinarushawa TBC cha bongo Dar es Salaam kinaonyesha matukio ya wizi ,kinarudi tenah ITV kwanzia wiki hii Jumapili,ukikifatilia vizuri kile kipindi utanielewa vizuri kwann mm nakusihi usiondoke stationary kwa mawazo yangu ...unaweza ukapigwa kote kote ww jiamini Tu Baki ndani ya ofisi kama mfalme
Thanks.Uzi mzuri
Ouky ngoja nikubali ,ila umakini unaanza na ww mwenyewe kwanzaHapana mkuu. Busara ni kukaa nje ya ofisi ya mtu kama mhusika hayupo.
Umenena vema sana mkuuHakika....wapo wawaonao ndugu zao ambao hawajafanikiwa kama hawana akili na kuekti wanampenda Mungu sana... kumbuka usipompenda ndugu yako unayemuona utampendaje Mungu usiyemuona... mnafiki wewe...kutokumjali ndugu yako ni kumchukia dhahiri....wapo wasiopenda hata kuwasiliana na ndugu zao na akijua una namba yake anabadilisha nyingine.... wanafiki wakubwa
Mkuu, hapa unamaanisha wale wanaokula wali katika sinia moja kubwa kama kule pwani??Ukikuta wanakula kwa pamoja... acha kutumbukiza mikono kinywani kwa kujilamba, unatulisha mate yako...hii hata kama ni kivyako haipendezi.
Duuuuh, pole sana mkuu.Yani ile sauti ya pyeee pyuuu! Ni kichefuchefu sana
Sijahalalisha mkuu, but that's the sad reality of juvenile life.Mkuu mbona unahalilisha jambo lenye kumchukiza manaani.
Tujitahidi sana kadri ya uwezo wetu tusisahau mkuu.uzi wa maana sana huu, ajabu ukishaingia mtaani unasahau yote
Kweli mtu akiudondosha chini anaurudisha halafu kesho unautumiaPia, usiache mswaki wako katika choo au bafu linalotumiwa na watu wengi
Asante sana mkuuUzi wa maana sana huu.
Sio ndio yule jamaa wa "job true true/kazi kweli kweli" au "cotton and more" pambana zaidi.Kuna jamaa humu jf huwa anasema "Humanity is a work" Kwamba ubinadamu kazi😀
Hakika mkuu. Wema unaweza kukutokea puani.Msaidie MTU yeyote km liko kwenye uwezo wako na umejihakikishia kuwa ni salama.( Kuna misaada unaweza kukuletea tabu)
Usiulize sana ishu kama ,vp unaolewa lini,unaoa lini,vp una watoto wangapi maana mwingine anatafùta mtoto hapati,maswali haya yanaumiza watu kihisia(1) Ukipiga mihayo (yawning), chafya au kukohoa, funika mdomo na pua kwa mikono yote miwili.
(2) Usiteme mate, kutapika, kupenga kamasi, wenzako wakiwa wanakula.
(3) Ukienda nyumbani kwa mtu, hususan rafiki, usitangaze madhaifu utakayoyaona. Mfano: Watoto wao wanashindia nguo zilizochanika.
(4) Rafiki yako unayeheshimiana naye, usiwe na namba ya simu ya mkewe ili kuepuka kutembea naye.
(5) Ukiacha kazi ofisini, usiwatukane former employers wako kwa maana katika maisha kuna leo na kesho.
(6) Ni vema ukapakua chakula kidogo kisha ukaongeza kuliko kupakua kingi alafu ukashindwa kukimaliza.
(7) Ukienda kwenye sherehe, hata kama wewe ni ndugu za karibu, usikae sehemu za VIP bila kukaribishwa. Ni aibu sana kuambiwa uondoke kwenye seat za VIP uende kwa wageni wa kawaida.
(8) Ukigundua spouse wa rafiki yako ana uhusiano wa nje ya ndoa, mfuate na mkanye ila usimwambie mumewe/mkewe.
(9) Mtu akikusaidia mara moja, usimgeuzi kitega uchumi cha kumuomba mara kwa mara. Kumbuka yeye pia ana majukumu yake binafsi.
(10) Ukiongea kwenye simu na mtu wa mbali sio vizuri kusema "fulani (Alex) nipo naye hapa ongea naye pia. Kama huyo Alex hajakuomba kuongea na mhusika basi kaa kimya.
(11) Ukipata mshahara mwisho wa mwezi, wape kidogo mfanya usafi pamoja na mpika chai hapo ofisini kwenu. Hao ndio informers na wanajua mengi ya hapo ofisini kwenu.
(12) Usiache kwenda likizo ya mapumziko kwa kuambiwa eti "tutakufidia kwa fedha hizo siku 28 za mapumziko". Afya yako ya akili ni kitu cha msingi sana.
(13) Ukienda ugenini kisha ukaachwa peke yako sebuleni, usishike chochote kama mwenyeji wako hayupo (ameenda kunununulia soda kwa mfano). Hata kama ni gazeti umelikuta hapo, subiri akirudi ndio umuombe.
ONGEZEA NA WEWE NDUGU YANGU......