Mambo ya Msingi Sana katika maisha

Mambo ya Msingi Sana katika maisha

Ukibahatika kupata maisha mazuri usisahau ulikotoka, kwenye maisha kuna kupanda na kushuka.
Hakika....wapo wawaonao ndugu zao ambao hawajafanikiwa kama hawana akili na kuekti wanampenda Mungu sana... kumbuka usipompenda ndugu yako unayemuona utampendaje Mungu usiyemuona... mnafiki wewe...kutokumjali ndugu yako ni kumchukia dhahiri....wapo wasiopenda hata kuwasiliana na ndugu zao na akijua una namba yake anabadilisha nyingine.... wanafiki wakubwa
 
Ukienda stationary kutoa photocopy au kazi yoyote ile, kisha mhusika akatoka nje kwenye kufanya jambo lolote kama vile kutafuta chenchi, basi na wewe Toka ukae nje. Usibaki mule mule ndani kwa maana kuna kitu kinaweza kupotea kisha wakasema kuwa ni wewe ndiye uliyekichukua.
Kuna kipindi kilikuwa kinarushawa TBC cha bongo Dar es Salaam kinaonyesha matukio ya wizi ,kinarudi tenah ITV kwanzia wiki hii Jumapili,ukikifatilia vizuri kile kipindi utanielewa vizuri kwann mm nakusihi usiondoke stationary kwa mawazo yangu ...unaweza ukapigwa kote kote ww jiamini Tu Baki ndani ya ofisi kama mfalme
 
Hapana mkuu. Busara ni kukaa nje ya ofisi ya mtu kama mhusika hayupo.
 
Hakika....wapo wawaonao ndugu zao ambao hawajafanikiwa kama hawana akili na kuekti wanampenda Mungu sana... kumbuka usipompenda ndugu yako unayemuona utampendaje Mungu usiyemuona... mnafiki wewe...kutokumjali ndugu yako ni kumchukia dhahiri....wapo wasiopenda hata kuwasiliana na ndugu zao na akijua una namba yake anabadilisha nyingine.... wanafiki wakubwa
Umenena vema sana mkuu
 
(1) Ukipiga mihayo (yawning), chafya au kukohoa, funika mdomo na pua kwa mikono yote miwili.

(2) Usiteme mate, kutapika, kupenga kamasi, wenzako wakiwa wanakula.

(3) Ukienda nyumbani kwa mtu, hususan rafiki, usitangaze madhaifu utakayoyaona. Mfano: Watoto wao wanashindia nguo zilizochanika.

(4) Rafiki yako unayeheshimiana naye, usiwe na namba ya simu ya mkewe ili kuepuka kutembea naye.

(5) Ukiacha kazi ofisini, usiwatukane former employers wako kwa maana katika maisha kuna leo na kesho.

(6) Ni vema ukapakua chakula kidogo kisha ukaongeza kuliko kupakua kingi alafu ukashindwa kukimaliza.

(7) Ukienda kwenye sherehe, hata kama wewe ni ndugu za karibu, usikae sehemu za VIP bila kukaribishwa. Ni aibu sana kuambiwa uondoke kwenye seat za VIP uende kwa wageni wa kawaida.

(8) Ukigundua spouse wa rafiki yako ana uhusiano wa nje ya ndoa, mfuate na mkanye ila usimwambie mumewe/mkewe.

(9) Mtu akikusaidia mara moja, usimgeuzi kitega uchumi cha kumuomba mara kwa mara. Kumbuka yeye pia ana majukumu yake binafsi.

(10) Ukiongea kwenye simu na mtu wa mbali sio vizuri kusema "fulani (Alex) nipo naye hapa ongea naye pia. Kama huyo Alex hajakuomba kuongea na mhusika basi kaa kimya.

(11) Ukipata mshahara mwisho wa mwezi, wape kidogo mfanya usafi pamoja na mpika chai hapo ofisini kwenu. Hao ndio informers na wanajua mengi ya hapo ofisini kwenu.

(12) Usiache kwenda likizo ya mapumziko kwa kuambiwa eti "tutakufidia kwa fedha hizo siku 28 za mapumziko". Afya yako ya akili ni kitu cha msingi sana.

(13) Ukienda ugenini kisha ukaachwa peke yako sebuleni, usishike chochote kama mwenyeji wako hayupo (ameenda kunununulia soda kwa mfano). Hata kama ni gazeti umelikuta hapo, subiri akirudi ndio umuombe.

ONGEZEA NA WEWE NDUGU YANGU......
Usiulize sana ishu kama ,vp unaolewa lini,unaoa lini,vp una watoto wangapi maana mwingine anatafùta mtoto hapati,maswali haya yanaumiza watu kihisia
 
Back
Top Bottom