Mambo ya Msingi Sana katika maisha

Ukiwa ugenini Usipende kupondaponda mambo ya watu.
 
Chukua Tano kwanza 🤜🏾🔥🤛🏾

1.Jifunze kuwasikiliza watu mpaka wamalize kuongea ndipo ujibu, usidakie dakie au kung'ang'ana uwe muongeaji mkuu, Sikiliza zaidi ya kuongea.

2.Ukipakuliwa chakula ugenini bakiza kidogo kuonyesha umeshiba hadi ukashindwa kumaliza.

Ila ukijipakulia hakikisha unamaliza.

3.Uwe mtu wa maneno yako, ukiahidi tekeleza, ukisema nafika saa2 fika saa2.

4.Ukikosea kubali, usikimbilie kujitetea tetea, ahidi kubadilika, inaonyesha unekomaa kihisia.

5.Usiwe mtu mwema kwa kila mtu bali kuwa mtu mzuri kwa watu sahihi.

6.Hata uwe na maarifa makubwa vipi na ujuzi vipi usijisifie, viongee vitendo.

7.Mshkaji wako akinunua soda mgawane ongezea na karanga za kushushia.

I'm Out.
 
NAKAZIA NUMBER 3: Ukiona mtu amekukaribisha nyumbani kwake, ujue amekuheshimu na kukuamini sana, hivyo na wewe muoneshe uaminifu kwa kutomdhalilisha madhaifu ya nyumbani kwake.

Sio vizuri kusema, "CDF/IGP/Waziri fulani alinikaribisha nyumbani kwake kumbe hana lolote. Makochi yake yamechanika na tena mchana niliwakuta wanakula dagaa.

Hapana, huu sio uungwana.
 
8.Mshkaji wako akinunua soda mgawane ongezea na karanga za kushushia.
Ni jambo jema sana mkuu.

Vile vile, Usinunue chakula ukala peke yako mbele ya watu wengi kisha wenzio wanakutazama tu. Huu sio uungwana. Kama mpo kijiweni watu 10 alafu wewe una hela ya kununua soda moja tu, basi tulia tu hivyo hivyo utanunua soda ukirudi ghetto/home kwako.
 
2.Ukipakuliwa chakula ugenini bakiza kidogo kuonyesha umeshiba hadi ukashindwa kumaliza, uki Empty plate utawafanya wahisi wamekupunja, ukiiweza hii fanya hotelini pia, Inaleta respect.
Yaani hotelini kabisa nimelipia hela halafu nibakishe chakula?
Mi hua nasafisha kila kitu, respect itakuja kwa ustaarabu mwingine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…