Alex Muuza Maembe
JF-Expert Member
- Dec 13, 2024
- 655
- 1,413
- Thread starter
- #41
But this sounds dirty.Ukishikwa tako ukiwa kwenye foleni usipige kelele muache anaekushika tako hata akikupiga kidole tulia usifanye fujo
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
But this sounds dirty.Ukishikwa tako ukiwa kwenye foleni usipige kelele muache anaekushika tako hata akikupiga kidole tulia usifanye fujo
Ukiwa ugenini Usipende kupondaponda mambo ya watu.(1) Ukipiga mihayo (yawning), chafya au kukohoa, funika mdomo na pua kwa mikono.
(2) Usiteme mate, kutapika, kupenga kamasi, wenzako wakiwa wanakula.
(3) Ukienda nyumbani kwa mtu, hususan rafiki, usitangaze madhaifu utakayoyaona. Mfano: Watoto wao wanashindia nguo zilizochanika.
(4) Rafiki yako unayeheshimiana naye, usiwe na namba ya simu ya mkewe ili kuepuka kutembea naye.
(5) Ukiacha kazi ofisini, usiwatukane former employers wako kwa maana katika maisha kuna leo na kesho.
(6) Ni vema ukapakua chakula kidogo kisha ukaongeza kuliko kupakua kingi alafu ukashindwa kukimaliza.
(7) Ukienda kwenye sherehe, hata kama wewe ni ndugu za karibu, usikae sehemu za VIP bila kukaribishwa. Ni aibu sana kuambiwa uondoke kwenye seat za VIP uende kwa wageni wa kawaida.
(8) Ukigundua spouse wa rafiki yako ana uhusiano wa nje ya ndoa, mfuate na mkanye ila usimwambie mumewe/mkewe.
(9) Mtu akikusaidia mara moja, usimgeuzi kitega uchumi cha kumuomba mara kwa mara. Kumbuka yeye pia ana majukumu yake binafsi.
(10) Ukiongea kwenye simu na mtu wa mbali sio vizuri kusema "fulani (Alex) nipo naye hapa ongea naye pia. Kama huyo Alex hajakuomba kuongea na mhusika basi kaa kimya.
(11) Ukipata mshahara mwisho wa mwezi, wape kidogo mfanya usafi pamoja na mpika chai hapo ofisini kwenu. Hao ndio informers na wanajua mengi ya hapo ofisini kwenu.
(12) Usiache kwenda likizo ya mapumziko kwa kuambiwa eti "tutakufidia kwa fedha hizo siku 28 za mapumziko". Afya yako ya akili ni kitu cha msingi sana.
(13) Ukienda ugenini kisha ukaachwa peke yako sebuleni, usishike chochote kama mwenyeji wako hayupo (ameenda kunununulia soda kwa mfano). Hata kama ni gazeti umelikuta hapo, subiri akirudi ndio umuombe.
ONGEZEA NA WEWE NDUGU YANGU......
Hakika mkuu. Ni vema tuwe na vifua vya kuhifadhi mambo.Ukiwa ugenini Usipende kupondaponda mambo ya watu.
Ukichelewa kufika piga simu kwa mhusika. Mjulishe kisha muombe radhi.4.Uwe mtu wa maneno yako, ukiahidi tekeleza, ukisema nafika saa2 fika saa2.
Kuwa mzuri kwa watu wengi na sio kwa kila mtu. Kuna watu ni lazima kuwa wakali kwao.6.Usiwe mtu mwema kwa kila mtu bali kuwa mtu mzuri kwa kila mtu.
✊🏿✊🏿Ukichelewa kufika piga simu kwa mhusika. Mjulishe kisha muombe radhi.
Ni jambo jema sana mkuu.8.Mshkaji wako akinunua soda mgawane ongezea na karanga za kushushia.
Good. Huu ndio urafiki wa kweli.8.Mshkaji wako akinunua soda mgawane ongezea na karanga za kushushia.
Mkuu, una hekima nyingi mnoooUsinunue chakula ukala peke yako mbele ya watu wengi kisha wenzio wanakutazama tu. Huu sio uungwana. Kama mpo kijiweni watu 10 alafu wewe una hela ya kununua soda moja tu, basi tulia tu hivyo hivyo utanunua soda ukirudi ghetto/home kwako.
Yaani hotelini kabisa nimelipia hela halafu nibakishe chakula?2.Ukipakuliwa chakula ugenini bakiza kidogo kuonyesha umeshiba hadi ukashindwa kumaliza, uki Empty plate utawafanya wahisi wamekupunja, ukiiweza hii fanya hotelini pia, Inaleta respect.
Yaani hotelini kabisa nimelipia hela halafu nibakishe chakula?
Mi hua nasafisha kila kitu, respect itakuja kwa ustaarabu mwingine
Asante sana mkuu. Binadamu hatujakamilika, ila tujitahidi sana kuwa watu wema kadri ya uwezo wetu.Mkuu, una hekima nyingi mnooo
Hakika.Asante sana mkuu. Binadamu hatujakamilika, ila tujitahidi sana kuwa watu wema kadri ya uwezo wetu.
Hahahahaaa, mkuu, umenichekesha sana.Yaani hotelini kabisa nimelipia hela halafu nibakishe chakula?
Mi hua nasafisha kila kitu, respect itakuja kwa ustaarabu mwingine
Ukiwa unakula au muda wowote??Kupenga mafua ni kero yangu kubwa mno...