Mambo ya Msingi Sana katika maisha

Mambo ya Msingi Sana katika maisha

(1) Ukipiga mihayo (yawning), chafya au kukohoa, funika mdomo na pua kwa mikono.

(2) Usiteme mate, kutapika, kupenga kamasi, wenzako wakiwa wanakula.

(3) Ukienda nyumbani kwa mtu, hususan rafiki, usitangaze madhaifu utakayoyaona. Mfano: Watoto wao wanashindia nguo zilizochanika.

(4) Rafiki yako unayeheshimiana naye, usiwe na namba ya simu ya mkewe ili kuepuka kutembea naye.

(5) Ukiacha kazi ofisini, usiwatukane former employers wako kwa maana katika maisha kuna leo na kesho.

(6) Ni vema ukapakua chakula kidogo kisha ukaongeza kuliko kupakua kingi alafu ukashindwa kukimaliza.

(7) Ukienda kwenye sherehe, hata kama wewe ni ndugu za karibu, usikae sehemu za VIP bila kukaribishwa. Ni aibu sana kuambiwa uondoke kwenye seat za VIP uende kwa wageni wa kawaida.

(8) Ukigundua spouse wa rafiki yako ana uhusiano wa nje ya ndoa, mfuate na mkanye ila usimwambie mumewe/mkewe.

(9) Mtu akikusaidia mara moja, usimgeuzi kitega uchumi cha kumuomba mara kwa mara. Kumbuka yeye pia ana majukumu yake binafsi.

(10) Ukiongea kwenye simu na mtu wa mbali sio vizuri kusema "fulani (Alex) nipo naye hapa ongea naye pia. Kama huyo Alex hajakuomba kuongea na mhusika basi kaa kimya.

(11) Ukipata mshahara mwisho wa mwezi, wape kidogo mfanya usafi pamoja na mpika chai hapo ofisini kwenu. Hao ndio informers na wanajua mengi ya hapo ofisini kwenu.

(12) Usiache kwenda likizo ya mapumziko kwa kuambiwa eti "tutakufidia kwa fedha hizo siku 28 za mapumziko". Afya yako ya akili ni kitu cha msingi sana.

(13) Ukienda ugenini kisha ukaachwa peke yako sebuleni, usishike chochote kama mwenyeji wako hayupo (ameenda kunununulia soda kwa mfano). Hata kama ni gazeti umelikuta hapo, subiri akirudi ndio umuombe.

ONGEZEA NA WEWE NDUGU YANGU......
Ukiwa ugenini Usipende kupondaponda mambo ya watu.
 
Chukua Tano kwanza 🤜🏾🔥🤛🏾

1.Jifunze kuwasikiliza watu mpaka wamalize kuongea ndipo ujibu, usidakie dakie au kung'ang'ana uwe muongeaji mkuu, Sikiliza zaidi ya kuongea.

2.Ukipakuliwa chakula ugenini bakiza kidogo kuonyesha umeshiba hadi ukashindwa kumaliza.

Ila ukijipakulia hakikisha unamaliza.

3.Uwe mtu wa maneno yako, ukiahidi tekeleza, ukisema nafika saa2 fika saa2.

4.Ukikosea kubali, usikimbilie kujitetea tetea, ahidi kubadilika, inaonyesha unekomaa kihisia.

5.Usiwe mtu mwema kwa kila mtu bali kuwa mtu mzuri kwa watu sahihi.

6.Hata uwe na maarifa makubwa vipi na ujuzi vipi usijisifie, viongee vitendo.

7.Mshkaji wako akinunua soda mgawane ongezea na karanga za kushushia.

I'm Out.
 
NAKAZIA NUMBER 3: Ukiona mtu amekukaribisha nyumbani kwake, ujue amekuheshimu na kukuamini sana, hivyo na wewe muoneshe uaminifu kwa kutomdhalilisha madhaifu ya nyumbani kwake.

Sio vizuri kusema, "CDF/IGP/Waziri fulani alinikaribisha nyumbani kwake kumbe hana lolote. Makochi yake yamechanika na tena mchana niliwakuta wanakula dagaa.

Hapana, huu sio uungwana.
 
8.Mshkaji wako akinunua soda mgawane ongezea na karanga za kushushia.
Ni jambo jema sana mkuu.

Vile vile, Usinunue chakula ukala peke yako mbele ya watu wengi kisha wenzio wanakutazama tu. Huu sio uungwana. Kama mpo kijiweni watu 10 alafu wewe una hela ya kununua soda moja tu, basi tulia tu hivyo hivyo utanunua soda ukirudi ghetto/home kwako.
 
2.Ukipakuliwa chakula ugenini bakiza kidogo kuonyesha umeshiba hadi ukashindwa kumaliza, uki Empty plate utawafanya wahisi wamekupunja, ukiiweza hii fanya hotelini pia, Inaleta respect.
Yaani hotelini kabisa nimelipia hela halafu nibakishe chakula?
Mi hua nasafisha kila kitu, respect itakuja kwa ustaarabu mwingine
 
Yaani hotelini kabisa nimelipia hela halafu nibakishe chakula?
Mi hua nasafisha kila kitu, respect itakuja kwa ustaarabu mwingine
Screenshot_20241215-195235.png
 
Back
Top Bottom