Mambo yaliyokuwa yanakuudhi nyumbani ulipokuwa mdogo...

Mambo yaliyokuwa yanakuudhi nyumbani ulipokuwa mdogo...

Ile nimeludi home kutoka shule mama ananiita nikiitika ananiuliza umeshaludi?kuna siku nilimwambia bado na hiyo ndo ikawa siku ya kwanza mimi kufunga kula
 
Kuamka asubuhi ilikua mbinde.... Mzee anakuja na kopo la maji mwa.... Usingizi wote unakata..... Kuna mda hadi tunafukuzana ndani kisa kuchelewa kuamka.
 
mimi tulikuwa tunashindana kuwahi shule ya msingi na rafiki yangu siku moja nikawahi kulala saa moja nikashtuka baadae kidogo kwa kuwa nilikuwa nishavaa sale ya shule kabisa nikavaa viatu huyo nikawaacha hom wamelala mi nikasepa,
ashukuliwe yule mlevi aliyeniludisha mpaka nyumbani,ilikuwa saa tano usiku ye ndo katoka bar.
[emoji23] [emoji23] [emoji23]Duh! Hiyo sifa
 
Kuamka asubuhi ilikua mbinde.... Mzee anakuja na kopo la maji mwa.... Usingizi wote unakata..... Kuna mda hadi tunafukuzana ndani kisa kuchelewa kuamka.
utasikia matajiri wote walisha amka we ndo bado unajinyosha kama una hela pumba*u
 
1.Mimi nilikua nikienda kuzurura mchana nikirudi sikuti chakula
2.kuamsha alfajiri halafu naambiwa nikaoge niende shule
3.kumegewa nyama wakati wa kula
 
Tukipewa vitu vitamu tamu vya kula,mdogo wangu akimaliza chake,akililia changu,Mama akinikata jicho tu lazima apewe kabla hajalia ng'wiiiii!!
Mdogo angu alkua anapenda sana wali sasa kila mtu na sahani yake, mama alkua akitujazia msahani mkubwa, mi nakula nabakisha cha kula na chai asubuh dogo akimaliza chake mama anachukua changu anampa, nilikua nakasirika balaa, siku moja ili kumkomoa nikamaliza chote nilivimbiwa usiku sikulala ni kugugumia tu
 
Kupaka mafuta ya kula badala ya mafuta ya ngozi maana hali ya maisha ilikuwa ngumu sana kikopo cha laser kilikuwa ni mpaka sikukuu
mkuu hiyo hata mm ilishawah nikuta mda wa kwenda shule ndo nikagundua mafuta yameisha na wazaz wameenda kazini ili bidi nipite na sunflower oil
 
Siku binamu yetu wa kike akija kulala kwetu mama alkua analalanae, au nikienda lala kwao bibi anataka nilalenae nilikua nakasrika sana hawajui tuu, alkua mchumba angu.
 
kuna siku niliona wanapika ugali na nyanya chungu nikasema nimeshiba ule mda wapo wanakula nikapita sebleni nikakuta tobaa!kumbe mzee aliludi na nyama choma,machozi yakaanza kutoka nikaulizwa nini nikasema kichwa kinauma nilipelekwa mpaka dispensar kuchomwa sindano za bure,nyama hajawai niacha salama

[emoji3][emoji3]
 
Dada wa kazi alinitesa sana kuhusu kulala mchana natandka mito naenda kucheza anakuja kunifata mbinu zote alikuwa anazijua hahaha da Happy popote ulipo nakusalimia ulinitesa sana mshenz ww
Teh teh teh.....
 
Back
Top Bottom