Mambo yanayoweza kufanya Ukishinda Beti (Mkeka usilipwe)

Mstahiki Mea

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2018
Posts
6,559
Reaction score
12,518
Kwenye tasnia ya betting malalamiko hayaishi pengine ni kutokuwa na uelewa wa wahusika na wadau leo naona niorodheshe mambo ambayo yanaweza kusababisha usilipwe mkeka hata kama umeshinda na nihatua gani ya kuchukua ,, vile vile nitaeleza mambo yanayochelewesha malipo.

UKIFANYA MAMBO HAYA HUTALIPWA
1. Kutofuata masharti ya bonasi uliyopewa (pending bonus) kama umekubali kupokea bonasi nimuhimu kusoma vigezo,na masharti yake ili ikitokea umeshinda milion 5 kwa bonasi usipotimiza vigezo ukinyimwa usi kalamike. Ndio kuna bonasi mpaka uzibetie mara 5 mfululizo , zipo nyingine kazima ubetie kiasi chote kwahiyo ni muhimu kutimiza masharti kabla ya kujaribu kutoa. Ili kulipwa unatakiwa kutimiza Sharti la bonasi
2. Baadhi ya kampuni nilazima utumie 100% ya kiasi ulichodeposit iliuweze kulipwa au kuruhusiwa kutoa . Ili kulipwa nilazima utimize sharti hilo.

3. Kushindwa kuthibitisha KYC
Kampuni ya betting ina haki ya kukufahamu wewe mteja wao kwa wewe kutuma document zako za uthibitisho hasa unapopata ushindi mkubwa au wanapolazimika kufanya hivyo hii nikwa mujibu wa sheria . Ili kuliowa unatakiwa kutimiza kigezo hiki.
4. Kubadilisha njia uliyotumia kuwekea pesa na ukataka kutoa kwa njia nyingine . Baadhi ya kampuni njia uliyotumia kuweka pesa ndio njia hiyo hiyo unatakiwa kutumia kutolea.

5. Kutoa pesa kwa njia ya bank Tanzania. Bank za tanzania hazipokei pesa za betting kwahiyo unaweza kudeposit kwa bank card lakini hutaruhusiwa kutoa kwa bank card so kuwa makini usitumie bank ku deposit.

Mambo ambayo unaweza kupoteza ushindi na kutolipwa kabisa

1. Bonus fraud ,, kuwa na account zaidi ya moja kwa lengo la kufaidi bonasi ,, hii inaweza kusababisha kufungiwa account moja kwa moja,, wakikuhurumia watakuomba KYC na kututa ubaki na moja lakini adhabu yake huwa nikufutiwa account (Block)
2. Fixed game : ukiambatanisha fixed game kwenye mkeka wako hautalipwa. Fixed game ni mechi zilizonunuliwa halafu zikasambaa wewe ukaipata au kwa bahati mbaya umeichagua. Mara nyingi dau linarudishwa
3. System error bookmaker anaweza kukosea odds au mtandao umezingua kwamfano Man u Vs man city Dk ya 80 wapo 0–0 halafu odds za draw ni 4.0 yani kwa ufupi ni odds kukosa uhalisia ukikimbilia ukabeti hutalipwa.
4. Kubetia kampuni ambazo hazina leseni ,, hata kama ni kampuni ya nje hakikisha ina leseni iwe ni curacao , anjuan leseni za bodi za michezo ya bahati nasibu n.k na ujiridhishe.

Mambo yanayoweza kuchelewesha Malipo
Unaweza kushinda na kulipwa lakini malipo yakachelewa
1. Mkeka unahakikiwa
2. Tatizo la kimtandao
3. Kama kuna washindi wengi walioshinda fedha nyingi. Hii inatokana ma sababu kuwa kwa mujibu wa BOT na sheria za fedha kika kampuni ina transaction limit hivyo ningumu kwa kampuni kufanya transaction kubwa kwa siku 1 , wiki 1 au wiki kadhaa,, mfano kampuni ina transaction limit ya bilion 1 kwa siku halafu wateja wameshinda bilion 10 lazima mtalipwa kwa awamu kwa siku 10 kwahiyo kabla ya kulalamika nimuhimu kujua sababu

Kama hujalipwa ufanyeje?
Kwanza wasiliana na huduma kwa wateja kampuni husika wakwambie tatizo nini na jinsi ya kutatua. Kama hujaridhika
Wasilisha malalamiko yako bodi ya michezo ya bahati nasibu kama itashindikana kwa mwongozo wa bodi ya michezo ya bahati nasibu unaweza kufungua shauri. Nimuhimu kujihakikishia kuwa hujavunja vigezo vyao . Vilevile ni muhimu kusoma vigezo na masharti kabla ya kujiunga na kampuni yeyote ile ya michezo ya bahati nasibu.
Mwisho cheza kistaarab mu na hakikisha una miaka 18 na kuendelea
 
Ajabu ni kua hilo zengwe lote unaletewa baada ya kushinda tu. Hasa pesa nyingi hizi ndogo ndogo wala hutoona ukipata shida kutoa.

Ukweli ni kua kumpuni zinataka na zimetengenezwa ww uliwe. Ukila mambo ndipo yanakua tofauti.
Ndio hivyo mkuu. 🤣 hujawahi kununua kitu wanavyokuita vizuri na kukuchekea ,, kikiwa na shida ukirudisha unaona wamenuna nikawaida hiyo
 
Kwenye tasnia ya betting malalamiko hayaishi pengine ni kutokuwa na uelewa wa wahusika na wadau leo naona niorodheshe mambo ambayo yanaweza kusababisha usilipwe mkeka hata kama umeshinda na nihatua gani ya kuchukua ,, vile vile nitaeleza mambo yanayochelewesha malipo.

UKIFANYA MAMBO HAYA HUTALIPWA
1. Kutofuata masharti ya bonasi uliyopewa (pending bonus) kama umekubali kupokea bonasi nimuhimu kusoma vigezo,na masharti yake ili ikitokea umeshinda milion 5 kwa bonasi usipotimiza vigezo ukinyimwa usi kalamike. Ndio kuna bonasi mpaka uzibetie mara 5 mfululizo , zipo nyingine kazima ubetie kiasi chote kwahiyo ni muhimu kutimiza masharti kabla ya kujaribu kutoa. Ili kulipwa unatakiwa kutimiza Sharti la bonasi
2. Baadhi ya kampuni nilazima utumie 100% ya kiasi ulichodeposit iliuweze kulipwa au kuruhusiwa kutoa . Ili kulipwa nilazima utimize sharti hilo.

3. Kushindwa kuthibitisha KYC
Kampuni ya betting ina haki ya kukufahamu wewe mteja wao kwa wewe kutuma document zako za uthibitisho hasa unapopata ushindi mkubwa au wanapolazimika kufanya hivyo hii nikwa mujibu wa sheria . Ili kuliowa unatakiwa kutimiza kigezo hiki.
4. Kubadilisha njia uliyotumia kuwekea pesa na ukataka kutoa kwa njia nyingine . Baadhi ya kampuni njia uliyotumia kuweka pesa ndio njia hiyo hiyo unatakiwa kutumia kutolea.

5. Kutoa pesa kwa njia ya bank Tanzania. Bank za tanzania hazipokei pesa za betting kwahiyo unaweza kudeposit kwa bank card lakini hutaruhusiwa kutoa kwa bank card so kuwa makini usitumie bank ku deposit.

Mambo ambayo unaweza kupoteza ushindi na kutolipwa kabisa

1. Bonus fraud ,, kuwa na account zaidi ya moja kwa lengo la kufaidi bonasi ,, hii inaweza kusababisha kufungiwa account moja kwa moja,, wakikuhurumia watakuomba KYC na kututa ubaki na moja lakini adhabu yake huwa nikufutiwa account (Block)
2. Fixed game : ukiambatanisha fixed game kwenye mkeka wako hautalipwa. Fixed game ni mechi zilizonunuliwa halafu zikasambaa wewe ukaipata au kwa bahati mbaya umeichagua. Mara nyingi dau linarudishwa
3. System error bookmaker anaweza kukosea odds au mtandao umezingua kwamfano Man u Vs man city Dk ya 80 wapo 0–0 halafu odds za draw ni 4.0 yani kwa ufupi ni odds kukosa uhalisia ukikimbilia ukabeti hutalipwa.
4. Kubetia kampuni ambazo hazina leseni ,, hata kama ni kampuni ya nje hakikisha ina leseni iwe ni curacao , anjuan leseni za bodi za michezo ya bahati nasibu n.k na ujiridhishe.

Mambo yanayoweza kuchelewesha Malipo
Unaweza kushinda na kulipwa lakini malipo yakachelewa
1. Mkeka unahakikiwa
2. Tatizo la kimtandao
3. Kama kuna washindi wengi walioshinda fedha nyingi. Hii inatokana ma sababu kuwa kwa mujibu wa BOT na sheria za fedha kika kampuni ina transaction limit hivyo ningumu kwa kampuni kufanya transaction kubwa kwa siku 1 , wiki 1 au wiki kadhaa,, mfano kampuni ina transaction limit ya bilion 1 kwa siku halafu wateja wameshinda bilion 10 lazima mtalipwa kwa awamu kwa siku 10 kwahiyo kabla ya kulalamika nimuhimu kujua sababu

Kama hujalipwa ufanyeje?
Kwanza wasiliana na huduma kwa wateja kampuni husika wakwambie tatizo nini na jinsi ya kutatua. Kama hujaridhika
Wasilisha malalamiko yako bodi ya michezo ya bahati nasibu kama itashindikana kwa mwongozo wa bodi ya michezo ya bahati nasibu unaweza kufungua shauri. Nimuhimu kujihakikishia kuwa hujavunja vigezo vyao . Vilevile ni muhimu kusoma vigezo na masharti kabla ya kujiunga na kampuni yeyote ile ya michezo ya bahati nasibu.
Mwisho cheza kistaarab mu na hakikisha una miaka 18 na kuendelea
Kama kampuni ilikuruhusu kufungua account kwa namba ya simu au email pekee, kwa nini haikukudai KYC kabla ya kukuruhusu kuweka pesa na kubeti? Kama KYC ni muhimu kwa malipo, kwa nini mfumo haukuzuia betting mpaka ukamilishe taarifa zako? Kama nimeweka pesa zangu mwenyewe, kwa nini nilazimishwe kuzicheza zote kabla ya kutoa? Je, hilo ni sharti la kisheria au ni sera ya kampuni tu?

Kama kampuni inaruhusu mteja kushinda milioni 5 kwa bonasi, kwa nini isionyeshe wazi kabla ya kubeti kwamba fedha hizo hazitatolewa mpaka masharti yote yatimizwe? Kama nimeweka pesa kwa njia fulani, kwa nini nilazimishwe kutoa kwa njia hiyo hiyo? Kama njia ya deposit haikubali withdrawal, kwa nini kampuni iliiruhusu wakati wa kuweka pesa?

Umesema benki za Tanzania hazipokei pesa za betting, una ushahidi gani wa kauli hiyo? Je, ni benki zote au baadhi ya benki? Kama kampuni inaruhusu mtu kufungua account kwa namba tofauti, kwa nini mfumo wake usigundue mapema badala ya kumfungia baada ya kushinda?

Kama mechi ni fixed, mteja wa kawaida anajuaje kabla ya kubeti? Kama kampuni ilijua mechi ni fixed, kwa nini iliweka mechi hiyo kwenye mfumo? Je, kuna ushahidi wa mechi kuwa fixed au ni madai tu? Kama kampuni imekosea odds, kwa nini mteja awajibike kwa kosa la mfumo? Je, kampuni inaweza kubatilisha ushindi wowote kwa kudai system error bila ushahidi? Ni nani anathibitisha kwamba kulikuwa na system error?

Umesema kampuni inaweza kuchelewesha malipo kwa sababu washindi ni wengi na kuna transaction limit, una ushahidi wa limit hiyo? Je, hiyo ni limit ya kisheria, benki au kampuni yenyewe? Kwa nini mteja apewe adhabu ya kusubiri kwa sababu kampuni haikujipanga kifedha?

Kama kampuni inaruhusu mteja kuweka pesa, kubeti na kushinda, lakini baada ya kushinda inatafuta sababu mbalimbali za kumzuia kutoa pesa, je, tatizo ni kutokujua masharti kwa mteja au ni kampuni kutokuwa wazi tangu mwanzo?

WEWE NI MSHENZI UMETUMWA NA PIGA BETI MPENI PESA ZAKE 27.7 MILIONI

JITU BANDIA Lwiva Joanah
 
Pamoja na kwamba umeuliza maswali mengi ngoja nikujibu ifuatavyo.

1. KYC ni sheria kutoka bodi ya michezo nasibu , nimuhimu kwasababu inailinda kampuni na inaweza kusaidia kuzuia utakatishaji. Kuhusu ulinzi kuna mtu anaweza kuhack mfumo akatoa pesa hasa inapokuwa ushindi wa fedha nyingi nimuhimu mtoa huduma awe na taarifa zako.
2. Ukiona kampuni haina KYC wakati wa kujisajili inakiuka vigezo, na kampuni nyingi wanaondoa kwasababu wanajua watu wanaobeti hawataki usumbufu lakini kama umeshinda lazima utalazimika kutafuta KYC

3. Sheria na vigezo vya kampuni huandikwa kwenye terms and condition unatakiwa kusoma kwanza kabla ya kujiunga
4. Sheria za bonasi zipo wazi kila bonasi unaweza kusoma na kuona vigezo vilevile unaweza kuikataa au kuikubali (sio kila kampuni ina bonasi)
5. Kuhusu kucheza pesa zote ulizobetia ni sharti la kampuni hii inasaidia kuzuia kampuni husika kutumika kama njia ya transaction. Kwamfano mtu aliyepo USA anaweza kudeposit 100$ halafu akampa login details mtu aliyepo Tanzania akaitoa hiyo 100$ kwahiyo inakuwa imetumika kama transaction method, pia kwenye utakatishaji mtu anaweza kuamua kudeposit halafu akaitoa ili hiyo hela ionekanw imetoka kwenye betting kumbe haijatumika. Kampuni za kimataifa nyingi zina hii sharti na hata za ndani kuna zenye sharti la kuikata 6% kama hujaitumia.
6. Njia uliyotumia kuweka ndio hiyo hiyo utatumia kutoa kwa kampuni nyingi za kimataifa hii inawawezesha wao kubalance njia zao walizoweka . Kubalance foti. Deposit methods sio zao wanaingia partneship
7. Kufungua account tofauti . Sio kila kampuni ina hiyo sheria ukisoma masharti yao utakuta wanaruhusu ama laa, mara nyingi mifumo haina uwezo wa kugundua yenyewe mpaka wao wafuatilie na watafwatilia endapo una issue. Ila hii kampuni nyingi wanatumia busara endapo hukufanya bonus fraud.
8. Kuhusu fixed kwanza utambue kampuni sio inayotengeneza odds wao wananunua au tuseme wanalipia kutoka kwa bookmaker mfano altenar n.k kampuni wao wana watu wa risk management na odds analytics ambao wanafwatilia mwenendo mzima ,, kupitia mifumo ya kampuni wanaweza kugundua fixed game kutokana na jinsi odds zinavyobadilika, customer behavior na mambo mengine wakigundua mapema mechi ni fixed wanaifunga wakigundua wakati unaendelea utarudishiwa dau lako na hutapewa ushindi. Nilazima waeleze kwenye sheria zao lakini pia kama wewe utafungua madai watashirikiana ma shirikisho husika kuchunguza na kudhibitisha zaidi lakini mara nyingi fixed ipo wazi . Na utakuta imeondolewa au imesitishwa kwenye kampuni zote.
9. System error ikitokea huwa kuna ushahidi wa wazi na dau linarudishwa lakini hupewi ushindi ,, kampuni inaweza kurhibitisha system error .
10. Transaction limit ,, ipo hata wewe una transaction limit katika simu yako kuna kiwango huwezi kutuma wala kutoa kwa siku. Account zote za transaction Zipo hivyo. Hata kusingekuwa na limit, ukienda bank umeweka pesa ukataka kutoa bilion 300 hela huwa inakuwa kwenye mzunguko.
Kwahiyo kama wateja jumla mmeshinda trilion moja haiwezekani transaction ya trilion moja ndani ya siku moja au mbili lazima mtalipwa kwa awamu. Wateja wa betpawa 2024 october watakuwa wanajua ninachokisema. Siku hiyo betpawa walipata washindi wa bilion 300 ilichukua zaidi ya wiki kulipwa wote. Kwa taarifa zaidi ulizia transaction limit BOT.
11. Bank za Tanzania hazipokei pesa za betting kampuni itazituma lakini usser atazuia hivyo itarudi kwenye account. So kama umetumia njia hiyo labda ufuate altenative nyingine.

Suala la mwisho kampuni sheria na masharti huwa vipo wazi . Tatizo sisi hatusomi. Pia kumbuka wao ni wawekezaji na wanatakiwa kufuata sheria walizoweka. Wewe unaweka jero wao wanaweza kukulipa mpaka bilion na zaidi kwa jero yako kwahiyo nilazima wachunguze pia kuna suala la ugaidi nilazima wahakikishe fedha zinaenda mahala sahihi hasa kwenye ushindi wa pesa nyingi.
 
Mkuu, majibu yako mengi yanaeleza sababu zinazoweza kufanya kampuni iwe na masharti, lakini bado hayajajibu hoja yangu ya msingi. Kama KYC ni sheria na ni muhimu kwa usalama wa fedha, kwa nini kampuni iliniruhusu kufungua account, kuweka pesa na kubeti bila kunikamilisha KYC? Kama kampuni inajua kwamba bila KYC siwezi kulipwa, kwa nini isizuie deposit na betting mpaka nikamilishe taarifa? Kwa nini mteja ndiye abebe madhara ya kampuni kumruhusu kutumia huduma kabla ya kukamilisha masharti muhimu?

Kuhusu terms and conditions, kusoma masharti ni wajibu wa mteja, lakini kuwepo kwa sharti kwenye terms hakumaanishi kila sharti ni la haki au kampuni inaweza kujiondoa kwenye wajibu wake. Swali ni je, kampuni ilimweleza mteja wazi kabla ya deposit kwamba anaweza kuzuiwa kutoa pesa zake mwenyewe kwa sababu hajacheza kiasi fulani? Kama bonasi ina masharti, hilo linaeleweka, lakini kwa nini pesa za mteja mwenyewe zichanganywe na bonasi mpaka ashindwe kuzitoa?

Kuhusu transaction limit, umesema kampuni inaweza kuchelewesha malipo kwa sababu washindi ni wengi. Sawa, lakini je, kuna muda maalumu ambao kampuni inapaswa kumlipa mteja? Kama kampuni inajua ina uwezo mdogo wa kufanya malipo, kwa nini iruhusu watu kuweka dau kubwa kuliko uwezo wake wa kulipa? Na kama malipo yamechelewa, mteja anapewa taarifa rasmi, sababu na ratiba ya malipo, au anaambiwa tu subiri? Mfano wa BetPawa wa mwaka 2024 unahitaji ushahidi wa taarifa rasmi za kampuni au chanzo kingine, si kutajwa tu.

Kuhusu fixed games na system error, nimeuliza kwa nini mteja awajibike kwa kosa ambalo hakulifanya. Umesema kampuni ina risk management na inaweza kuthibitisha kosa. Sawa, lakini je, mteja anapewa ushahidi wa kosa hilo na utaratibu wa kukata rufaa? Kwa sababu kampuni kusema tu “system error” au “fixed game” hakutoshi kumaliza mjadala bila maelezo.

Kuhusu benki, kusema benki za Tanzania hazipokei pesa za betting ni kauli kubwa. Je, ni benki zote? Ni sheria gani au sera gani ya benki inasema hivyo? Na kama njia ya deposit inaruhusiwa lakini withdrawal haikubali, kwa nini mteja asielezwe hilo kabla ya kuweka pesa?

Mwisho, mimi sikatai kwamba kampuni zina wajibu wa kuzuia utakatishaji wa fedha, fraud na matumizi mabaya ya mifumo. Ninachouliza ni hiki: Kama kampuni ina uwezo wa kukagua account, kuthibitisha KYC, kugundua bonus fraud, system error na transaction limits, kwa nini ukaguzi huo usifanyike kwa wakati unaofaa kabla ya mteja kuweka pesa na kubeti, badala ya kusubiri mpaka ashinde ndipo aanze kuwekewa vikwazo? Hapo ndipo uwajibikaji wa kampuni unapopaswa kujadiliwa, si kumwambia mteja tu kwamba hakusoma terms.
 
Suala la kukamilisha KYC Nilako wewe mteja kwasababu mfumo unaruhusu kufanya kyc hata kabla hujashinda. Kampuni nyingi ziko hivyo angalia sehemu ya document au Kyc . Sasa inapotokea umeshinda hasa kiasi kikubwa nilazima watake kuona hizo taarifa kama hukujaza watakuomba ujaze. Kwahiyo unapojiunga nimuhimu kujaza jina Rasmi na ukamilishe michakato yote ,,kama kampuni husika haina jua kuna wakati zinaweza kuhitajika kama ukishinda ushindi mkubwa.

2. Kuhusu bank kutopokea hela za betting huwa hazipokei kaangalie kama ni sheria za fedha au ni matakwa yao binafsi. Altenative unaweza kutumia njia za malipo nyingine kama skrill au binance, ambazo hela ikishaingia huko unaweza kuhamiahia bank lakini sio kutoa direct kutoka kwenye operator kwenda bank.

3. Kuhusu kuchelewa malipo kunakosababishwa na ushindi mkubwa. Hilo ni jambo la kawaida. Hakuna kampuni unayoweza kushinda milion 20 au zaidi na ukaipata siku hiyo hiyo kwenye simu yako. Digit zitakwekwa kwenye player account yako lakini ku withdraw huwa kuna withdraw limit na hata simu yako ina kiwango cha mwisho cha kupokea hela kwa siku. Kwahiyo ni either utatoa kidogo kidogo au kama kuna option ya kwenda kuwakewa cash kwa bank au vinginevyo mtakavyo kubaliana.

Hilo moja lapili. Nimesema kuna transaction limit betpawa walitoa taarifa ya kuchelewa malipo kutokana na jambo hilo. Fuatilia taarifa mtandaoni lakini haikuchukua mda mrefu sana. Sio kuwa hawakujipanga kwa ushindi huo kutokea bali haiwezekani kufanya malipo zaidi ya transaction limit iliyopo, kama kwasiku wanaweza kulipa bilion 100 halafu washindi mmeshinda jumla bilion 600 mtalipwa kwa siku sita. fedha inakuwa katika mizunguko mbalimbali hata bank huwezi kwenda ukakuta bilion au trilion zimekaa zinasubiri in Digit sawa kitasoma kiasi hicho lakini fedha halisi inakuwa kwenye mizunguko. Hata ukiwaambia voda walipe wateja walioshinda mikeka bilion 50 kwa siku watakuwa na hiyo flot?
 
Sawa, lakini bado kuna maswali kadhaa hujajibu.

Kama KYC ni wajibu wa mteja na kampuni inaruhusu kuikamilisha kabla ya kushinda, kwa nini mfumo usimzuie kuweka pesa na kubeti mpaka akamilishe? Na kama kampuni ilimruhusu bila KYC, kwa nini mteja ndiye abebe madhara ya hilo?

Kuhusu masharti ya bonasi, je, kampuni inaweza kutumia sharti la bonasi kumzuia mteja kutoa pesa zake mwenyewe ambazo hazikutokana na bonasi? Kama ndiyo, ni kwa msingi gani?

Kuhusu transaction limit, kama kampuni inajua uwezo wake wa malipo kwa siku ni mdogo, kwa nini iruhusu wateja kuweka dau kubwa kuliko uwezo huo? Na kama mteja ameshinda, kwa nini asipewe muda rasmi wa kulipwa badala ya kuambiwa asubiri mpaka fedha zirudi kwenye mzunguko?

kampuni kuwa na masharti haimaanishi kila sharti ni la haki. Swali ni je, kampuni inawajibikaje inapomruhusu mteja kuweka pesa, kubeti na kushinda, halafu inamzuia kutoa kwa sababu ambazo zingeweza kuzuilika kabla ya betting?
 
zipo kampuni huwezi kuendelea na usajili lazima ufanyw KYC kwanza ili kukamilisha usajili kabla ya kufanya chochote. Nyingine unaweza kuendelea na mambo mengine mpaka KYC ikihitajika mfano kushinda kiasi kikubwa au kudeposit kiasi kikubwa. Kwahiyo inategemea na kampuni. Mimi ningependekeza kampuni zote ziwe na KYC kabla ya kufanya chochote japo nayo ina usumbufu kwa wateja na pia kuna wateja ambao walishajiunga bila Hiyo KYC kwahiyo hiyo labda kwa kampuni mpya inaweza kufanya kazi. Kuhusu Bonasi mfano umedeposit 500,000 ukapewa bonasi 1,000,000 na sharti la bonasi ni kubetia pesa ya bonasi mara nne ndipo unufaike nayo so kama utabeto mara moja na ukashinda huwezi kunufaika nayo mpaka uibetie mara zote nne ,, so hiy9 mara moja hutaweza kutoa ni either u timize sharti la bonasi au usubiri bonus iexpire , kila bonasi masharti yake huwekwa.

Kuhusu ushindi mkubwa kwa watu wengi kampuni inao uwezo wakulipa. Isipokuwa limit kwa mujibu wa sheria za nchi. Huwezi kampuni kufanya yransaction y bilion 50 kwa siku moja. Hata mifumo ya kifedha haiwezi kuhimili hiyo. Pia ushindi mkubwa kwa watu wengi ni jambo nadra. Kwamfano Tanzania tangu kuanza kwa betting imetokea mara moja tu ,,
 
HUYU AMETUMWA ILI TU YULE JAMAA WA 27ML ASILIPWE,BILA SHAKA!
Sawa endelea kusema nimetumwa. Hakuna anayeweza kunituma. Huyo jamaa wa milion 27 aripoti bodi ya michezo ya bahati nasibu wakishindwa aende mahakamani. Ila nilichoandika mimi ni uhalisia kama kunasehemu nimepotosha utasema
 
Nimeweka milioni moja kupitia tigo pesa, nime bet nikashinda milioni 60 unataka nitoe milioni 60 kupitia tigo pesa?
 
Sawa, lakini bado kuna maswali kadhaa hujajibu.

Kama KYC ni wajibu wa mteja na kampuni inaruhusu kuikamilisha kabla ya kushinda, kwa nini mfumo usimzuie kuweka pesa na kubeti mpaka akamilishe?
Kwasababu inawapendeza zaidi kuwa na urahisi wa kula pesa zako huku pakiwa na ugumu kula pesa zao.
 
Back
Top Bottom