Kama kampuni ilikuruhusu kufungua account kwa namba ya simu au email pekee, kwa nini haikukudai KYC kabla ya kukuruhusu kuweka pesa na kubeti? Kama KYC ni muhimu kwa malipo, kwa nini mfumo haukuzuia betting mpaka ukamilishe taarifa zako? Kama nimeweka pesa zangu mwenyewe, kwa nini nilazimishwe kuzicheza zote kabla ya kutoa? Je, hilo ni sharti la kisheria au ni sera ya kampuni tu?
Kama kampuni inaruhusu mteja kushinda milioni 5 kwa bonasi, kwa nini isionyeshe wazi kabla ya kubeti kwamba fedha hizo hazitatolewa mpaka masharti yote yatimizwe? Kama nimeweka pesa kwa njia fulani, kwa nini nilazimishwe kutoa kwa njia hiyo hiyo? Kama njia ya deposit haikubali withdrawal, kwa nini kampuni iliiruhusu wakati wa kuweka pesa?
Umesema benki za Tanzania hazipokei pesa za betting, una ushahidi gani wa kauli hiyo? Je, ni benki zote au baadhi ya benki? Kama kampuni inaruhusu mtu kufungua account kwa namba tofauti, kwa nini mfumo wake usigundue mapema badala ya kumfungia baada ya kushinda?
Kama mechi ni fixed, mteja wa kawaida anajuaje kabla ya kubeti? Kama kampuni ilijua mechi ni fixed, kwa nini iliweka mechi hiyo kwenye mfumo? Je, kuna ushahidi wa mechi kuwa fixed au ni madai tu? Kama kampuni imekosea odds, kwa nini mteja awajibike kwa kosa la mfumo? Je, kampuni inaweza kubatilisha ushindi wowote kwa kudai system error bila ushahidi? Ni nani anathibitisha kwamba kulikuwa na system error?
Umesema kampuni inaweza kuchelewesha malipo kwa sababu washindi ni wengi na kuna transaction limit, una ushahidi wa limit hiyo? Je, hiyo ni limit ya kisheria, benki au kampuni yenyewe? Kwa nini mteja apewe adhabu ya kusubiri kwa sababu kampuni haikujipanga kifedha?
Kama kampuni inaruhusu mteja kuweka pesa, kubeti na kushinda, lakini baada ya kushinda inatafuta sababu mbalimbali za kumzuia kutoa pesa, je, tatizo ni kutokujua masharti kwa mteja au ni kampuni kutokuwa wazi tangu mwanzo?
WEWE NI MSHENZI UMETUMWA NA PIGA BETI MPENI PESA ZAKE 27.7 MILIONI
JITU BANDIA Lwiva Joanah