Mambo yanayoweza kusababisha mahari ya unayemuoa kuwa juu

Mambo yanayoweza kusababisha mahari ya unayemuoa kuwa juu

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
MAMBO YANAYOWEZA KUSABABISHA MAHARI KUWA KUBWA

Na, Robert Heriel

Baada ya huyu msanii Kudai kuwa mahari yake ni zaidi ya 500Mil(Milioni Mia tano) kwa anayetaka kumuoa. Nimeona tujadili kidogo kuhusu suala la mahari

Mahari ni zawadi itolewayo wakati wa kuposa au kuposwa kwa lengo la shukrani. Mahari kwa jamii nyingi hutolewa kwa Muolewaji(mwanamke) hata hivyo zipo jamii chache ambazo wanaume hulipiwa mahari.

Mahari ni suala la utamaduni/ mapokeo ndani ya jamii.
Kiimani na Kiroho hakuna amri ya lazima kutoa Mahari.
Ni suala la utamaduni zaidi.
Hata hivyo ni vizuri kutoa mahari ikiwa utamaduni wako unataka hivyo.

Mahari ni zawadi, zawadi Hiyo huweza kuzingatia Zaidi mila na desturi ya jamii husika. Zipo jamii mahari ni ng’ombe, zingine Mbuzi, ngamia, Dhahabu, Fedha nk

Hata hivyo mahari inaweza isiwe kitu kinachoonekana pia, mathalani mtu anaweza pewa sharti fulani akilitekeleza Hiyo ndio mahari yake. Kama vile kuondoa tatizo fulani ndani ya nyumba anayochumbia kama vile ugonjwa, au kulipa kisasi kwa adui anayeitesa familia, n.k.

Mahari hubadilika kulingana na nyakati na zama. Kwani kama nilivyosema ni mapokeo ya wazee na wala sio amri ya Mungu.

Mahari ikiendekezwa wakati mwingine huleta dhana ya biashara. Yaani mtolewa mahari huwa kama bidhaa ya kununuliwa sokoni. Ndio maana baadhi ya jamii katika Ulimwengu wa kwanza kama nchi za Ulaya na Marekani.Ambazo wanawake hawataki kutolewa mahari

Hata hivyo Haifurahishi kuoa bila mahari. Wala haipendezi bila kutolewa mahari.

Mahari ni muhimu kuliko Harusi

Kwani mahari yenyewe wakati mwingine ndio huweza kuwa Harusi.
Hii ni kusema kiutaratibu huwezi kufanya Harusi pasipo kutoa Mahari.

Mahari huweza kuwa urithi kwa mwanamke aliyeolewa hasa kwenye koo zisizo na urithi kwa wanawakike.
Nisifanye andiko kuwa Refu; tuone ni mambo gani yanayofanya Mahari iwe kubwa?

Mambo yanayofanya Mahari iwe Kubwa kwa Mwanamke Aolewapo;

1. HADHI YA FAMILIA MWANAMKE ATOKAPO

Hii ni sababu namba moja
Kama familia ni yahadhi ya juu basi kuna uwezekano mahari ya mwanamke nayo ikawa kubwa.
Familia yenye hadhi ya juu inamatumizi ya juu pia. Kuanzia Mahali wanapoishi, vyakula wanavyokula, mavazi, Vyombo vya usafiri kama magari, Vyombo vya mawasiliano kama simu nk

Sio Unataja mahari ambayo Baba yako mwemyewe hajawahi kuishika hiyo pesa🤣🤣🤣
Huko tunaita kuchanganyikiwa

Wewe unataja milioni 500 wakati ukoo wenu wote hakuna aliyewahi kuishi hiyo pesa. Kama sio wehu huo ni nini?

Familia za hadhi ya juu kutokana na matumizi yao huweza kutaka mahari ambayo wao huona ni pesa ya kawaida lakini Kumbe Kwa upande wa masikini ni mahari kubwa.

Mfano wanaweza taja mahari million 20 ambapo kimaisha ya Kitanzania hiyo pesa ni nyingi mno.
Nakumbuka wakati Nasoma Udsm Rafiki yangu wa kike alishindwa kuolewa kisa wazazi wake walisema mahari yake ni million 25,
Miuoaji alishindwa licha ya mahari kupunguzwa mpaka milioni 15. Na alipaswa kutanguliza walau nusu yake(7.5mil)

Kama hadhi ya familia ipo chini ni ngumu mahari kuwa juu.
Sio ajabu Vijana pindi wapatapo wachumba wa kike watokao familia zenye vipato vya juu kutishiwa Na Wazazi wao kuwa wasioe huko kwani gharama zao zipo juu

2. UZURI WA MWANAMKE
Hii ni Sababu namba mbili ambayo ni kubwa.
Uzuri wa mwanamke unachangia kwa kiasi kikubwa mahari kuwa kubwa.
Na hapa nazungumzia uzuri kamili wa mwanamke sio uzuri nusu nusu

Mwanamke mwenye sura nzuri
Umbo zuri lililogawanyika
Kimo kizuri cha kati yaani sio mrefu wala sio mfupi
Sauti nzuri ya kike haswa
Rangi nzuri iliyokolea na kuteleza
Nywele nzuri
Joto la mwili nzuri na mara zote huchangiwa na rangi yake.

Mwanamke wa hivi mahari zao ni kubwa.
Sio mwanamke mwenye uzuri nusu nusu.
Jambo moja ambalo wanaume tutaringa Lao ni kuwa wanawake wazuri kamili ni wachache mno. Hivyo hiyo kwetu ni advantage
Sasa wewe uzuri hauna unataka milioni 50 wakati hata milioni 2 hutapewa 😀😀

3. USAFI WA MWANAMKE/ UBIKIRA

Sababu namba tatu ni usafi wa mwanamke yaani ubikira wake.
Ubikra ni alama ya usafi na upya wa mwanamke
Ubikra huweza kufanya mahari kuwa juu.
Mwanamke bikra hana utofauti na mtoto aliyezaliwa leo kwa habari ya usafi wa tendo la ndoa

Bei ya Kitu kipya na kitu used/mtumba ni tofauti.
Kitu kipya huzwa kwa bei kubwa wakati kitu cha mtumba huuzwa kwa bei ya hasara
Sasa mtu hana bikra na anataka mahari milioni 10 😂😂😂 Labda kama ni Vichekesho au labda kwa mshamba
Huna bikra sana sana ukipendelewa na Mungu mahari ya juu milion 1.5 au 2mil mwisho

4. UMRI

Gazeti la jana bei yake ni tofauti na Gazeti la leo. Hapa tunazungumzia uhalisia sipo kukandia mtu hapa maana najua kuna watu wanamihemko😄😄

Mahari ya Binti wa miaka 18 - 25 huwa ni kubwa mno. Tofauti na mahari ya mtu mwenye zaidi ya miaka 30+
Kimahusiano mwanamke mwenye 30+ ameshazeeka(inauma ila ndio ukweli)

Ndio maana wazazi hulazimisha Binti zao wakiwa 20-25 waolewe ili isije wasumbua baadaya ya umri huo. Lakini Baadhi ya vitoto vya kike hujitia ujuaji mwingi na kudharau wazazi.
Kinachotokea kwa wengi wao wakishafikisha 30+ ndio huelewa walichoambiwa. Hapo wamegeuka Gazeti la jana wakisubiri kufungia maandazi na kalmati.😢😢😢

Umri 18-25 ndio umri pekee mwanamke ataringia maumbile yake na kumpata mwanaume amtakaye hasa wale wanaomtongoza.

5. KAZI
Mahari ya mwanamke mwenye kazi ipo juu tofauti na yule asiyejishughulisha Yaani Golikipa.

Mwanamke mwenye kazi kama Mwalimu, Daktari, mhasibu, hakimu au Jaji, Mfanyabiashara, Mama Lishe, Muuza genge, Fundi nguo n.k mahari zao ni tofauti na Golikipa mwanamke anayemtegemea Mume wak amhudumie kama mdoli

Wanaume wa siku hizi wanatafuta wake wa kujenga wote familia. Hakuna asiyejua maisha yamebadilika na yamekuwa Magumu .
Hakuna mwanaume anayetafuta Mdoli aupeleke nyumbani watu humtafuta mke aliyeandikwa kwenye mithali 31

Kama vile wanawake wapendavyo wanaume wachapakazi ndivyo ilivyo kwa wanaume wa siku hizi. Hatutaki midoli
Ni bora ufuge Mbuzi utakula nyama au ufuge kuku utakula mayai na nyama kuliko kuoa au kuolewa na mtu asiyefanya kazi.
Ukibisha sawa

6. ELIMU
Elimu ya dini na elimu ya Dunia
Mahari huwa kubwa kama mtu Anaelimu kubwa; ya Dini na yakidunia.

Sasa wewe Ekaristi ulikimbia
PF na AY hukuitaka
Madrasa kusoma juzuu uliona ni ushamba
Shule ya msingi ulikimbia umande
Secondary ukaendekeza Balehe na kuvunja ungo ukaishia kidato cha tatu.
Veta ukapelekwa ukakataa fani ya kushona nguo huku ukijua hakuna asiyevaa nguo😀😀😀

Alafu unategemea mahari yako iwe juu 😢😢😢 ajabu hii.

Dunia uliopo hujaisoma wala pepo na kuzimu uendako hujasoma. Niambie ipi tofauti yako na mnyama? Maana hata mnyama hajasoma hayo Ila anaishi.

Sizungumzi haya kwa nia mbaya ila kama sisi tulikosea basi tuhakikishe watoto wetu hawakosea kama wafanyavyo baadhi ya watu ambao walishindwa wao ila wanajitahidi kuwapeleka watoto wao shule wapate Elimu ya Dunia Na Elimu ya kidini. Ili wasiwe kama wanyama

Ukimaindi kwa upumbavu wako Fresh
Ila ukiichukua kama Changamoto ni sawa.pia

Kwa leo hii ndio tamati

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa Morogoro
 
Dah. Umeandika ndefu sana.

Yote ni pingamizi ya mahari?

Sasa usimuangalie huyo wa 500m tafuta kabinti ambako unahisi ni size yako, mueleze nia Yako, watembelee wazee wake ufate utaratibu wa kummiliki na umuweke ndani.

Mfundishe mapenzi na mjenge kuwa mama bora kwa watoto wako.

Hawa wanawake wa mitandaoni watakupa msongo wa mawazo na kukufanya ujihisi hujakamilika.
 
Dah. Umeandika ndefu sana.

Yote ni pingamizi ya mahari?

Sasa usimuangalie huyo wa 500m tafuta kabinti ambako unahisi ni size yako, mueleze nia Yako, watembelee wazee wake ufate utaratibu wa kummiliki na umuweke ndani.

Mfundishe mapenzi na mjenge kuwa mama bora kwa watoto wako.

Hawa wanawake wa mitandaoni watakupa msongo wa mawazo na kukufanya ujihisi hujakamilika.

Hamna sehemu yoyote nimepinga Mahari Karucee

Nimejadili mambo yanayofanya Mahari iwe juu

Kuhusu mimi kutafuta mwanamke hilo sio la kushauriwa

Naweza kutafuta mwanamke popote pale iwe mtandaoni
Bar
Kanisani
Mtaani nk
 
Mwanamke hauzwi , masuala ya mahari sijui nini inategemea na umasikini ama utajiri wa familia husika , watu wamegeuza mahari kama kitega uchumi, kuna takataka moja limetredi sana kwenye mitandao ya kijamii eti mahari yake milioni 500, sasa ukiangalia hupati picha hiyo hela ni kwaajili tu ya papuchi ama kuna mengine yako nyuma ya pazia.

Kuna mzee mmoja alimtoa bintiye bureee kwakua alijua wamechaguana wenyewe na wamependana wenyewe, sasa sekeseke likaja kwa ndugu ooh mtoto sijui kaenda bure ooh sijui nini umasikini tu ndio tatizo hapa
 
Mwanamke hauzwi , masuala ya mahari sijui nini inategemea na umasikini ama utajiri wa familia husika , watu wamegeuza mahari kama kitega uchumi, kuna takataka moja limetredi sana kwenye mitandao ya kijamii eti mahari yake milioni 500, sasa ukiangalia hupati picha hiyo hela ni kwaajili tu ya papuchi ama kuna mengine yako nyuma ya pazia.

Kuna mzee mmoja alimtoa bintiye bureee kwakua alijua wamechaguana wenyewe na wamependana wenyewe, sasa sekeseke likaja kwa ndugu ooh mtoto sijui kaenda bure ooh sijui nini umasikini tu ndio tatizo hapa
🤣🤣🤣🤣

Mambo ya Mila hayo Mkuu
 
Hiyo ni kawaida ya wanawake wa huko Dar kuropoka kauli hizo nakumbuka miaka ya nyuma hata Diva wa Clouz naye aliropokaga mahari ya bei kubwa hivyohivyo
 
Ukiona mdada unaruhusu mchumba wako achajiwe mahari kubwa kuna akili flani zimekupungua
 
Back
Top Bottom