Mamelodi Sundowns wako Overrated

Nasikitika kusema kwamba hakuna mwana simba mwenye kichwa kama chako.
 
Kwa hiyo Simba ni bora kuliko Raja?
Una kichwa kigumu sana mkuu, mpira ni mchezo wa kimbinu, Raja ni bora kuliko Simba ila Horoya waliingia na approach sahihi dhidi ya Raja na waka fanikiwa kupunguza idadi ya mabao,, Simba ina Quality kubwa mara mbili ya Horoya na mistake kubwa waliofanya ni kucheza kwa kufunguka wasijue kuwa kwa kufanya hivyo wanaingia kwenye mfumo wa mnyama. Mwisho wa siku scoreboard 7-0
 
Unataka kucheza na maswandana jaza viungo,waachie wakae na mpira,wajibu kwa kaunta kwa kutumia sakho na okrah wapitie pembeni,kwisha habari yao.
 
Mimi sio mbumbumbu kama nyie. Mwenzako amesema ivyo akizungumzia swala la ubora ndio maana akasema vile sasa unakuja kuanza kusafisha upuuzi wake.

Okay mpira ni swala la mbinu kama unavyosema. Kwa akili zako za kimbumbumbu unategemea Robertinho kwa mbinu zake ataweza kumzuia Mokwena? Tunapozungumzia ubora hatuongelei tu wachezaji hamna ubora wa mbinu kuizuia Masandawana. Mtapigwa kama chapati endelezeni ujinga.
 
Brother acha ushabiki kuwa realistic Simba hana uwezo wa Ku battle na Mamelodi Sundowns labda itokee tu maajabu ambayo kwenye football yapo lakini kwa quality, experience, technical bench hizi timu ni mbigu na aridhi
 
Umeandika personal feelings ndugu yangu ila naomba siku moja ukae uangalie mechi zote walizocheza CAFCL Huu msimu afu uje uedit thread
 
Niambie hio nafasi kubwa kwa Simba kumfunga Mamelodi umei determine vipi? sababu kama ni clubs ranking Mamelodi wapo juu, statistics wapo juu wewe ulisha wahi hata kutoa draw na Al Ahly pale Cairo? tuachieni ujinga
 
Brother acha ushabiki kuwa realistic Simba hana uwezo wa Ku battle na Mamelodi Sundowns labda itokee tu maajabu ambayo kwenye football yapo lakini kwa quality, experience, technical bench hizi timu ni mbigu na aridhi
Mimi ni Simba lialia ila kiukweli wale jamaa ukiwaangalia wanajua Kuna mtu anaitwa Maema ,Mailula na Peter wale jamaa ndo injini pale kwa huu mpira wanaocheza labda Raja kidogo msimu huu ndo wako sawa ila jamaa wako far beyond us.
 
Umeandika personal feelings ndugu yangu ila naomba siku moja ukae uangalie mechi zote walizocheza CAFCL Huu msimu afu uje uedit thread
game ya Al Ahly na Sundowns 2-2 Cairo ule mpira hakuna timu ya bongo inaweza kuweka mguu pale, mtu anajiita mtu wa mpira vitu vidogo kama hivi havioni
 
Niambie hio nafasi kubwa kwa Simba kumfunga Mamelodi umei determine vipi? sababu kama ni clubs ranking Mamelodi wapo juu, statistics wapo juu wewe ulisha wahi hata kutoa draw na Al Ahly pale Cairo? tuachieni ujinga

Sababu simba anacheza mpira wa matokeo. Hachezi mpira wa kuuza sura. Mamelodi ndie angalau mnyonge wa mipira hiyo kuliko wenzake waydad ama esperence


Timu zingine ambazo simba anaweza kukutana nazo kama asipopangiwa mamelodi ni mbili zilizoongoza makundi yao ambazo ni Esperence na waydad casablanca, pia raja casablanca kaongoza kundi ambalo simba alikuwepo hivyo hawezi pangiwa raja.

Style ya esperence ama waydad casablanca ni ngumu kwa simba kuzifunga sababu huwa hazichezi mpira wa possession. Zinakuachia mpira ucheze wewe huku wao wanapiga mipira mirefu na kukufunga kibabe

Na hizo timu zinatwaa ubingwa mara nyingi kuliko mamelodi. Na huwa zinafanya vizuri kuliko mamelodi. Hata mamelodi mwenyewe hajawai kuzitoa hizo timu anapokutana nazo kwenye mitoano ya caf.

Jiulize mamelodi mara ya mwisho kuvuka robo fainali ilikuwa lini ?

Pia jiulize mamelodi amewai kutwaa ubingwa wa caf mara ngapi ?

Kisha maswali hayo hayo jiulize pia kwa esperence na waydad casablanca. Utapata majibu timu gani ni hatari zaidi kwa simba kati ya hizo 3 zilizoongoza makundi

Kila msimu mamelodi ni mzuri sana kwenye hatua ya makundi. Huwa anaongoza kundi lake kwa point kibao. Shida ya mamelodi huwa kwenye hatua za mtoano hasa robo. Huwa anatolewa kirahisi sana
 
Okay poa huo mpira wa matokeo ulikwama kwa Raja Casablanca? kama Mamelodi wanacheza show game wamewezaje ku dominate ligi ngumu ya South Africa na Simba wameshindwa nini Ku dominate ligi dhaifu ya Tanzania? pili kuna timu inacheza objective football hapa Africa kama Al Ahly? jiulize kwanini anabondwa kila leo finally Mamelodi ana kombe kachukua msimu 2015/2016 je Simba kasha wahi fika hata semi final?
 

Raja anacheza kama waydad na esperence anavyocheza. Ndio maana nimemtaja hapo juu sehemu nilipowataja hao wawili. Na nikaweka sababu why simba hatakutana nae.

Mamelodi hatishi kwa simba kama hao wengine.

Nenda katazame mechi zote mbili za mwaka huu 2023 zilizochezwa caf kati
Mamelodi vs Al hilal ya sudan.

Ya kwanza south africa

Na ya pili sudan

Jiulize Al Hilal na simba wana tofauti gani kiuwezo.

Kama Al hilal anaefanana kiwango na Simba anamsumbua Mamelodi why Simba ashindwe

Unajua hata huo msimu wa 2016 Mamelodi alitolewa kwenye mtoano. Akarudishwa tena mashindanoni acheze nusu fainali kwa maamuzi ya nje ya uwanja. Mamelodi Hakupita robo kwa kushinda mechi uwanjani.

Hata huo ubingwa wake aliupata kibahati maana alishatolewa.

Mamelodi anamuwezea Al Ahly hilo nakubali.. ila kwenye hatua za makundi. Sio kwenye mitoano.

Kwenye mitoano mamelodi hajawai mtoa Al Ahly zaidi ya mara moja.

Mara nyingi wakikutana mitoano Al Ahly ndie anaepita kwenda next stage
 
Okay so unadhani Mamelodi hawjalitambua hilo kila mwaka watakua wanarudia makosa yale yale?
 
Anakuja mtu, anakuambia Mamelodi ni wa kawaida. Ukimuuliza sababu, anakuambia habari za misimu iliyopita. Sijui mnatumia viungo gani kufikiri!

Mamelodi anaeongelewa hapa ni wa msimu huu. Mamelodi ambae yuko kwenye ubora wa hali ya juu. Kabisa mnategemea akina Onyango wawavushe kwa Mamelodi aliemtandika Al Ahly tano? Hamko serious!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…