Mamlaka husika fanyieni utafiti haya malori aina ya FUSO

Ndo maana Bus za kichina kazkazn n chache bado zipo zle lori zenye body ya bus ya kuchonga huku ina engine ya scania machalii wanapenda mlio wa scania balaa wakiuskia hadi wanaisindikiza kwa miluzi[emoji23]
Sahiv had pikpik zinaharibiwa exhaust na zinapigwa Moshi tatu ili ilie kama scania[emoji28]
 
Modification ya bodi sawa sijajua kuhusu kadi ya gari wanafanyaje kubadili uzito kwenye kadi ili iweze kupita mzani
 
Mtu mwenye IST halafu asafiri usiku utamjua tu, achananae anaongea kimitandao hana anachokijua kuhusu anachokizungumzia, wakati mwingine unamuacha afurahishe genge.
 
Acha upuuzi unataka kutuambia Wajapani waliotengeneza hii gari hawakufanya research, mje mtake kufanya nyie Mapopoma ambao hamjawahi hata kutengeneza baiskeli ya kwenu?
Japan ndio wansozijenga hizo bodi!?? Umesoma na kuelewa !?? Au ndio ila hadithi ya nyuki na yule mdudu anaebiringisha kinyesi!?? Nafikiri ulimpa shida sana mwalimu wako!!! Kama bandiko dogo hiv huelewi vipi importance of studying physics!?? Utaelewa kweli!?
 
6D15T,6D16T 3T,6D17,6M6OT,6M61...fuso ni gari kali sana...kadiri muda unavyokwenda maboresho yanafanyiaka. Ajali nyingi za mafuso chanzo ni USINGIZI. Huku field tunawaita wakukesha, usiombe ukutane nao iyovi wana wahi mabibo.
 
Ha ha ha ha wana balaaa.. nakuakbia juzi kati wakato tunateremka usiku kuna hiyo fuso apaa ndengaa. Bila shala alikua na ndizi. Siyo kutembea kule ni kupaa. Nawasifu madereva wanaoendesha usiku. Yaan naogopa balaa. Wanawezaje?
 
Ha ha ha kiufupi hata mimi napenda scania. Na napendaga hizo makitu. Mchina unanikera sana. Napendaga jinsj engene zinavyolalamikaga. Halaf wanavyipenda ligi sasa[emoji23][emoji23] nachekaga sana ligi za mchina na msweden aisee. Ila wanakuambia mwili hauna roho tembea dere iende irudi arifuuu
 
Neno utafiti limetumika vibaya. Yaan Japan wasifanye utafiti mje kufanya utafiti Wamatumbi?
Mbona yuko sawa kutumia neno 'utafuti'. Ana maana utafiti ufanyike hapa kwetu, kutambua nini chanzo cha ajali nyingi zinazohusisha malori ya Fuso hapa kwetu Tanzania. Ili ijulikane tatizo au chanzo cha ajali. Kama ni madereva wetu, au ni mifumo mibovu ya gari lenyewe au ni miundo mbinu yetu kama Taifa nk na nk.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…