Upo sahihi mkuu,chuma ikipakia Mali kuoza lazima itembee mwendo mkubwa kusudi mzigo usiharibikie njiani na ukizingatia bodi za hizo gari hazina mifumo ya kupozesha
Mwezi uliopita wa 8, nimetoka zangu Iringa kuelekea Moro si nikasema ngoja nidandie tank maana ilikua usiku saa tatu.
Eeh bwana ikajitokeza fuso nikasema sio mbaya ngoja niingie maana comfortability ya tank imezidi kwa fuso.
Ile fuso ilipakia njegere, ule mwendo sijawahi kuona tangu nazaliwa.
Nilicho jifunza hawa jamaa wa fuso wengi wanakodiwa kubeba mali mbichi kama nyanya, bamia, viazi waziwahishe sokon mapema kwa hiyo huo mwendo sasa.
Nikarud kweny kitand nikasema angalau likitikea la kutokea naweza kusalimika ila wapi usingiz uligoma kabisa.