KERO Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA), hili la maegesho (parking) ni kero kubwa

KERO Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA), hili la maegesho (parking) ni kero kubwa

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Hao TAA ifike sehemu wabinafsishwe ili waweke vitu vya kisasa, mfano Barabara za kurusha ndege walishindwa kujenga mpaka wakapewa Tanroad, sasa hivi sijui hata viwanja nivya taasisi IPi kati ya Tanroad na hao TAA, maana wameshindwa kuviendeleza wapo wanasubiri muongozo viwanja ni vya taasisi ipi?
Kama hujui vitu ni kheri ukakaa kimya tu ndg yangu ili ujifunze zaidi.
 
Hapo umeishamchoma jamaa kwa kuomba rushwa kwa kuanika risiti na namba za signature yake aliekuhudumia. Huyu hana kazi na wenzake wapewe onyo kali sana.

Rushwa naichukia sana ila kila kwenye mwanya wenye akili huwa wanaziba. Lakini kwa sababu tusizozijua unaona Rushwa ipo kila kona.

Wenzetu wameachana zamani sana na mambo ya kuweka wapokea hela. Technology imekuwa kiasi sasa huku majuu hata hospital kama unajua unaumwa nini unatuma msg tu na unaambiwa kachukue dawa pharmacy uliyochagua. Sasa mambo ya parking attendant mwisho ni zaidi ya miaka 20.

Kila kitu dili tu mpaka mnakera
 
Leo nimeshangaa pale nilipoegesha gari Terminal 2 kwa saa 72 na kudaiwa 75,000 za maegesho na kuambiwa kuwa “Long term parking” inahesabiwa ukiegesha Terminal III.

Kwanza, kaka aliyekuwa pale nikamuomba anisaidie (najua kuna uwezekano huo kwani mfumo unaona wazi gari limekaa muda mrefu hivyo linakidhi vigezo vya kuwa kwenye discount ya Long term parking). Yule kaka akataka nimpe 50,000/- aniachie au nilipe hiyo 75,000/-. Mimi si muumini wa kutoa wala kupokea rushwa, nikaona nilipe na kupata risiti hii (nimeiambatanisha chini).

View attachment 3064664

Nilisikitika mtu mzima mwenye kuonekana mwislam safi (alikuwa na sigda) kutaka rushwa huku kukiwa na maafisa wenzake 2 nyuma yake bila aibu. Ni aibu sana kama aina hii ya treatment watakuwa wanapewa wageni toka nje ya Tanzania. Watu hawa wanaaibisha Taifa kama hivi ndivyo wanavyofanya kazi.

Hivi, JNIA si ni ileile? Pia, kuna ugumu gani wa kuweka mifumo ya kidigitali ikatenda haki badala ya kuweka watu wanaoomba rushwa waziwazi?

Ushauri:
  • Mamlaka zinazohusika ziwachunguze wahusika hawa (hasa huyu kaka aliyekuwepo leo) kwa vitendo vya rushwa, watabaini mengi
  • Mfumo wa kidigitali ufungwe kuepusha usumbufu wakati wa ulipaji gharama za maegesho
  • Nina mashaka na kampuni yenye zabuni ya uendeshaji maegesho; kama ikiwezekana wale wanaoendesha maegesho Mlimani City aidha wapewe zabuni hii au waombwe ushauri ili kuifanya JNIA kuwa na maegesho yanayoendana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia
Huu uzi ulinisaidia sana maana jana nilikuwa na safari ya kwenda Mwanza na nimerudi leo. Nilifika alfajiri na mapema nikapatafuta. Papo Terminal 3 (katika mpaka na terminal 2) pameandikwa Long Parking.

Gharama zake ni Shs 15,000/= kwa masaa 24. Nimelipa 30,000/= kwa vile ilizidi masaa 24. Nimefurahia hii huduma maana tunaoishi mbali mfano kwa mwenzetu gari lilikaa masaa 72 hivyo ulitakiwa kihalali kulipa 45,000/=. Watu ni wajanja walitaka ulipe 50,000/= ili akalipe 45,000/= na yeye achomoke na ganji ya 5,000/=
 
Back
Top Bottom