KERO Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA), hili la maegesho (parking) ni kero kubwa

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Kama hujui vitu ni kheri ukakaa kimya tu ndg yangu ili ujifunze zaidi.
 
Hapo umeishamchoma jamaa kwa kuomba rushwa kwa kuanika risiti na namba za signature yake aliekuhudumia. Huyu hana kazi na wenzake wapewe onyo kali sana.

Rushwa naichukia sana ila kila kwenye mwanya wenye akili huwa wanaziba. Lakini kwa sababu tusizozijua unaona Rushwa ipo kila kona.

Wenzetu wameachana zamani sana na mambo ya kuweka wapokea hela. Technology imekuwa kiasi sasa huku majuu hata hospital kama unajua unaumwa nini unatuma msg tu na unaambiwa kachukue dawa pharmacy uliyochagua. Sasa mambo ya parking attendant mwisho ni zaidi ya miaka 20.

Kila kitu dili tu mpaka mnakera
 
Huu uzi ulinisaidia sana maana jana nilikuwa na safari ya kwenda Mwanza na nimerudi leo. Nilifika alfajiri na mapema nikapatafuta. Papo Terminal 3 (katika mpaka na terminal 2) pameandikwa Long Parking.

Gharama zake ni Shs 15,000/= kwa masaa 24. Nimelipa 30,000/= kwa vile ilizidi masaa 24. Nimefurahia hii huduma maana tunaoishi mbali mfano kwa mwenzetu gari lilikaa masaa 72 hivyo ulitakiwa kihalali kulipa 45,000/=. Watu ni wajanja walitaka ulipe 50,000/= ili akalipe 45,000/= na yeye achomoke na ganji ya 5,000/=
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…