DOKEZO Mamlaka za Serikali zichunguze Mradi wa Kongani la viwanda Maranje wenye thamani ya zaidi ya Sh Bilioni 300

DOKEZO Mamlaka za Serikali zichunguze Mradi wa Kongani la viwanda Maranje wenye thamani ya zaidi ya Sh Bilioni 300

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Serikali kupitia Bodi ya Korosho Tanzania (CBT) inatekeleza mradi wa Kongani la Viwanda vya Korosho wenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 300 katika eneo la Maranje, Halmashauri ya Mji Nanyamba mkoani Mtwara, unaolenga kuongeza ubanguaji wa korosho ndani ya nchi ifikapo Mwaka 2030.

Hata hivyo, kuna madai ya ongezeko lisilo la kawaida la gharama za utekelezaji wa mradi huo, huku mmoja wa watumishi wa CBT (jina limehifadhiwa) akitajwa kuhodhi kila kitu kwa maslahi ya watu binafsi na sio taasisi wala Sekta ya Korosho nchini.

Vilevile, inadaiwa kuwa kuna viongozi wa Bodi ya Korosho Tanzania ambao wanahusishwa moja kwa moja na kampuni inayosimamia miradi hiyo ijulikanayo kama KOROSHO INVESTMENT TANZANIA LIMITED, jambo linaloibua mgongano wa kimaslahi.

Taarifa za kuaminika zinaeleza kuwa mali zote za CBT pamoja na mradi wa Kongani la Viwanda zimekabidhiwa kwa kampuni hiyo jambo linaloibua maswali, hivyo kuwa na haja ya kufanya uchunguzi ili kuondoa wasiwasi huo lakini pia kuisafisha bodi dhidi ya madai hayo.
 
Kama ni kweli inabidi hatua stahiki zichukuliwe dhidi yao.. Hivi huu upigaji usio na maslahi kwa Wananchi wala mashirika ya Umma utaisha lini😥
 
Bodi ya Korosho Tanzania imechokwa mpaka na Wizara ya kilimo kutokana na madudu yanayoendelea ndani, huku Bodi ya wakurugenzi ikiwa kimya na kumuacha Mkurugenzi mkuu afanye atakavyo.

Katika kile kinachodhihirisha Taasisi hiyo ya umma kuchokwa na mpaka na Serikali, hata Viongozi wa Wizara ya Kilimo ambayo CBT ni moja ya Taasisi zilizoko chini yake, hawakuonekana kwenye mkutano wa wadau wa Korosho uliofanyika Mkoani Morogoro Agosti 27, 2026.

Mgeni rasmi katika mkutano huo muhimu alikuwa awe Waziri wa Kilimo Mhe.Daniel Chongolo na hata ratiba ilionesha hivyo tangu awali, lakini sio yeye wala Naibu Waziri waliofika kwenye mkutano huo jambo ambalo limeendelea kuzua mijadala.

Katika hali isiyo ya kawaida, Ilibidi Mhe.Waziri awakilishwe na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro jambo ambalo halijawahi kutokea katika mikutano ya wadau wa sekta ya Korosho, ambayo imewahi kuhudhuriwa mpaka na mawaziri wakuu miaka ya nyuma.

Ni kweli kwamba wiki ya mkutano ilikuwa na hekaheka nyingi ikiwepo kujiuzulu kwa makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Emmanuel Nchimbi, vikao vya Kamati kuu ya CCM, uteuzi wa makamu wa Rais, vikao vya Bunge nk.

Na pengine huo ndio utakuwa utetezi wa CBT kama ilivyo kawaida yao, lakini kiuhalisia na kwa taarifa za ndani ni kuwa isingeshindikana japo Naibu waziri kushiriki mkutano huo hasa ikizingatiwa kuwa ulikuwa unafanyikia Morogoro ambapo sio mbali na Dodoma, lakini viongozi hao waliususia mkutano huo kutokana na sintofahamu inayoendelea kufukuta ndani ya CBT.

Tuhuma zinazoiandama Taaissi hiyo ya Umma hadi sasa ni pamoja na matumizi mabaya ya Ofisi yanayofanywa na Mkurugenzi Mkuu, uwiano usio sawa unaoashiria upendeleo wa wazi kwa baadhi ya wafanyakazi, ubadhirifu wa fedha za miradi kama Kongani la Viwanda Maranje, ujenzi wa Ukumbi wa CBT, uuzwaji wa viwanja vya CBT vilivyopo Dar es Salaam, kufungwa kihuni kwa kizuizi cha ukaguzi wa Korosho Mkuranga nk.

Vilevile Mkurugenzi Mkuu anatuhumiwa kuwatumia baadhi ya wabunge kwa kuwalipa kiasi cha fedha ili wawe wanamtetea na kumsemea vizuri kwa mawaziri wa Kilimo tangu enzi za Waziri Hasunga, Hussein Bashe na sasa Daniel Chongolo, kaisi kwamba imekuwa vigumu sana mtendaji huyo kuwajibishwa na Wizara.

Kwa upande wa Bodi ya Wakurugenzi inatuhumiwa kushindwa kumsimamia na kuwajibisha Mkurugenzi mkuu kutokana na kuwatengenezea mazingira ya kuoata fedha (posho), lakini pia kumpa fursa mbalimbali mwenyekiti wa bodi kinyume na utaratibu, kwa kifupi inaonekana kama Bodi hiyo haipo tu maana hakuna inachofanya.

Kwa sasa jambo pekee wadau wanalotamani ni Mhe.Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kuivunja Bodi ya Wakurugenzi ya CBT, kumuwajibisha Mkurugenzi Mkuu, na kuunda kamati maalum itakayofuatilia na kuwasilisha ripoti ya wazi na ukweli ili hatua zichukuliwe.

Mhe.Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan atasaidia kwa sababu yeye ndio mtu pekee ambaye Mkurugenzi hawezi kumuweka mfukoni, lakini sio kamati za wizara,CAG nk..hizo zilishashindwa kuinusuru Taasisi hiyo.
 
Attachments

  • Screenshot_20260902-211824_All PDF Reader.jpg
    Screenshot_20260902-211824_All PDF Reader.jpg
    90.9 KB · Views: 15
Nchi inatafunwa mno,huku wakulima wa korosho wakiishi katika umasikini
 
Insemekana kuwa tayari madudu ya CBT yameshaanza kufika kwenye mamlaka za kiserikali na zinaendele kukusanya taarifa/vielelezo muhimu zikiwepo hizi zinazochapishwa Jamii Forums kwa ajili ya kuanza kuzifanyia kazi kwa wakati muafaka.

Hili ni jambo jema, lakini swali ni je, mamlaka hizo zitakuwa huru kwa kiasi gani?ikumbukwe kuwa zilishawahi kuundwa kamati/Tume mbalimbali na pia kumekuwepo na ufuatiliaji wa Taasisi kama PCCB, Ofisi ya CAG nk. lakini ripoti zake hazikuwahi kuleta mabadiliko yoyote ya kiutendaji ndani ya Taasisi, kama ilivyokuwa imetarajiwa mapema.

Pengine awamu hii labda mambo yatakuwa tofauti, wacha wadau tuendelee kupaza sauti, na kuna mambo mengi ya kushangaza tutaendelea kuyaweka humu ili mamlaka zipate pa kuanzia, na pengine zijue vile wananchi wanavyozitegemea kukomesha kiburi cha Mkurugenzi Mkuu wa CBT, baadhi ya watendaji wake wakiongozwa na wawili wa juu na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya CBT.

Zinachotakiwa kujua mamlaka hizo za uchunguzi ni kwamba zitakutana na kila aina ya ushawishi wa kuzima mambo na bila uadilifu mambo yatakuwa yakeyale, Mkurugenzi atawatumia hadi baadhi ya wabunge wa mikoa inayolima Korosho ambao ndio imekuwa kinga yake kubwa kwa miaka zaidi ya mitano sasa, wakipokea fedha kwa ajili ya kumlinda mpaka kwenye vikao vya kamati za bunge (majina ya wabunge hayo yapo).

Sio siku nyingi baadhi ya wabunge na viongozi wengine walipewa fedha mkoani Dodoma ili wakakutane na wananchi kupooza hali ya uhaba wa pembejeo aina ya Salfa na hakuna walichofanya (hili tutakuja nalo wakati mwingine) tuna ushahidi wa namna ambavyo CBT imekuwa ikitumia fedha kulinda maslahi ya viongozi wake.

Kinachofurahisha ni kwamba taarifa zipo nyingi na za kuaminika sana, mfano taarifa za kufungwa kihuni kizuizi cha Mkuranga, pale kulikuwa na Mgambo,Polisi, nk. ambao hao wote wana taarifa nyeti ambazo zinaeleza namna ambavyo Mwenyekiti na Mkurugenzi Mkuu walitumia kizuizi hicho kufanya madudu yao.

Tutashangaa sana kuona kamati/tume zikishindwa wakati huu na hapo ndipo tunapotaka kuiona nguvu ya Serikali na kwa kuanzia na maelekezo aliyotoa Mhe.Rais kwa wakuu wa Mikoa hivi karibuni juu ya kwenda kumuwakilisha vema katika mikoa husika.
 
KOROSHO KUTOKA ZAO KUU LA BIASHARA LA KIKANDA HADI LA KITAIFA

1.Korosho ni zao kuu la biashara nchini Tanzania, lilingia katika karne ya 16 likitokea nchini Msumbiji na mikoa ya Mtwara, Ruvuma na Lindi ilikuwa ya kwanza kulima zao hili.

2.Wareno walileta Korosho kama njia ya kudhibiti mmomonyoko wa udongo na si zao la biashara, hata hivyo baada ya vita ya pili ya Dunia matumizi ya zao hilo yalibadilika kutoka chakula na kudhibiti mmomonyoko wa udogo na kuwa zao la kibiashara na mwaka 1970 Tanzania ilishika nafasi ya pili Duniani kwa uzalishaji wa korosho.

3.Takwimu zinaonesha kuwa katika kipindi hicho tani 7,000 za korosho kwa mara ya kwanza zilisafirishwa nchini India, na hapo mtazamo ukabadilika, mikoa ya Pwani na Tanga ikaingia katika orodha ya wakulima wa Korosho japo kwa kiasi kidogo.

4.Pamoja na Pwani na Tanga kulima korosho bado, zao hilo lilikuwa linajulikana kama zao la kikanda, yaani kanda ya kusini, lakini kwa sasa hali ni kinyume, korosho si tena zao la kikanda bali ni zao la kitaifa, haya ni mapinduzi makubwa.

5.Miaka 56 sasa idadi ya wakulima wa korosho waliosajiliwa imefikia 549,936 wenye mashamba yenye ukubwa wa ekari 4, 567, 210.30 yenye mikorosho 132,016,333 kwa mujibu wa sensa ya wakulima wa zao hilo ya mwaka 2025 na Bodi ya Korosho Tanzania (CBT)

6.Idadi ya mikoa inayolima korosho nayo imeongezeka kutoka Mitano ya asili yaani Mtwara, Lindi, Ruvuma, Pwani na Tanga hadi kufikia mikoa 21 iliyotawanyika Tanzania nzima, na hii ni baada ya utafiti kuonesha kuwa korosho zinaweza kufanya vizuri katika mikoa hiyo.

7.Mikoa mingine inayolima korosho kwa sasa ni pamoja na Morogoro, Dodoma, Mbeya, Singida, Tabora, Kigoma, Katavi, Songwe, Njombe, Sumbawanga, Shinyanga(Ushetu), Mbeya, Kagera (Biharamulo), Iringa, Geita, na Kilimanjaro hivyo kufikisha idadi ya mikoa 21.

8.Uzalishaji wa korosho umeongezeka na kufikia tani 618,497 msimu 2025/26 zilizowaingizia wakulima kiasi cha Tsh. 1.302 trilioni na fedha za kigeni zaidi ya Dola za Kimarekani milioni 512 kupitia mauzo ya nje.

9.Haya yote yamewezekana baada ya Bodi ya Korosho kuanzisha mpango maalum ya kusambaza miche bora bure kwa wakulima wa zao hilo kuanzia mwaka 2022. Taarifa zinasema kuanzia mwaka 2022 hadi sasa CBT imesambaza miche bora ya korosho 8,604,024.

10.Ongezeko hilo la miche mipya kunatengeneza matarajio makubwa ya uzalishaji wa korosho nchini kuongezeka kutoka tani 618,497 hadi kufikia makadirio ya tani 750,000 msimu 2027/28 na tani 1,000,000 msimu 2029/30.

Jitihada hizi za Bodi ya Korosho Tanzania hazipaswi kutanzamwa kimyakimya bila kupongezwa na kuungwa mkono na wakulima na wadau wote wa zao hili nchini ili malengo ya kufikia uzalishaji wa Tani 1,000,000 ifikapo 2030 yawze kufanikiwa.
MUNGU IBARIKI TANZANIA
 
Kuhusu wafanyakazi wa CBT kuhamishwa kiholela hilo lipo wazi na ushahidi upo hadi Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara ina taarifa hizo, na hapa ni vema Wizara ya Utumishi ikaliangalia hili ambapo itabaini namna ambavyo Mkurigenzi Mkuu wa CBT ameshiriki sio tu kuwahamisha watumishi kwa maslahi yake binafsi, bali pia alivyompambani mmoja wa maafisa ambao hana sifa kupewa Cheki namba hivi karibuni.

Wakati Mkurugenzi Mkuu anaingia Bodi miaka ya 2019 kuchukua nafasi ya Profesa Magigi alikuta tayari Mkurugenzi wa Kilimo alishahamishiwa Morogoro kihuni, lakini cha kushanga bwana Francis Alfred naye akashindwa kumrejesha hivyo Kurugenzi hiyo muhimu kubaki bila mtu.

Badala yake alianza kumpa mmoja wa Chawa wake (Juma Yusufu) majukumu makubwa ya Kurugenzi na baadae kuhakikisha kuwa anapata ajira rasmi huku akijua kuwa uwepo wake ndani ya CBT ulikuwa na utata kwani mwaka 2016 aliyekuwa Waziri Mkuu alielekeza mtumishi huyo kurejeshwa Wizarani kutokana na kuvuruga minada ya Korosho misimu 2016/2017.

Kinachotokea CBT ni kuwa Mkurugenzi Mkuu akikukubali utakula sana mema ya nchi, unachotakiwa wewe ni kuwa chawa wake tu basi, utasafiri na kupewa vipaombele mpaka utachoka.

Na usipokuwa chawa wake utawekwa benchi mpaka utaiona kazi ngumu, na ukiwa humnyenyekei utahamishwa ofiasi mara moja na wapo watumishi waliohamishiwa Mbeya,Dar es Salaam, Tanga, Dodoma, Singida nk.

Yule aliyehamishiwa Katavi na baadae akarejeshwa kesi yake ni tofauti kidogo, hii tutaielezea wakati mwingine maana Mkurugenzi Mkuu wa CBT amishirikiana na Mbunge mmoja anayeongoza kupewa hongo za CBT kumhamisha Mtumishi kwa maslahi ya Mbunge Jimboni na kulinda madudu ya usafirishaji Korosho Karanga kinyemela (hili faili ni kubwa, litakuja kivyake wakati mwingine)

Failk jingine la kujitegemea litakalokuja ni matumizi mabaya ya Ofisi kwa Mkurugenzi mkuu kufikia hatua ya kuwadhalilisha kingono baadhi ya watumishi au interns wa kike walioahidiwa kupata mikataba na hawakupata kutokana na kushindwa kukidhi vigezo binafsi ya Mkurugenzi mkuu alivyotaka vitimizwe kabla ya kusaini mikataba.

Hili la udhalilishaji ni kubwa nalo litakuja kwa kujitegemea, kwa sababu lina ushahidi uliotimia kutoka kwa watumishi watatu, na interns mmoja aliyelazimika kuondoka baada ya kushindwa kutimiza matakwa ya kingono kwa bwana Mkubwa.

Kwa kifupi kuna mambo mengi yanakuja, hizi taarifa siku zinavyoenda ndivyo zinavyozidi kumiminika mpaka Wizara kupitia Waziri mwenye dhamana atakavyochukua hatua, na wakishindwa basi Mhe.Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan atawaonesha namna ya kufanya kazi kuanzia Waziri,Katibu Mkuu (Kilimo), Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Bodi ya Wakurugenzi wa CBT na Mkurugenzi Mkuu wa CBT kwa kushindwa kuwajibika na kuiacha Taasisi ya Umma ikibaghazwa huku wakiwa wanaona, ni jambo la muda tu.
 
Back
Top Bottom