Mamlaka za usimamizi wa usafiri wa abiria kutoka Moshi mjini kwenda wilaya jirani mko wapi abiria wananyanyasika

shamzugi

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2021
Posts
569
Reaction score
1,200
Habari za muda huu wakuu??

Jumamosi ya tarehe 5/7/2025 nilisafiri kuelekea mkoa wa Kilimanjaro, wilaya ya Hai mjini wa Bomang'ombe. Nilifika Moshi mjini majira ya saa Moja usiku.

Pale stendi ndogo nilikuta magari machache ya abiria yanayoelekea maeneo mbalimbali ya jirani. Gari za kuelekea Sanya juu zilikwepo ila makondakta walikua wakitabgaza nauli kiasi cha shilingi elfu mbili Kwa abiria wanaoshuka noma. Nikimfuata na kumuuliza kwanini anatangaza bei hiyo wakati nauli ya noma inajulikana ni shilingi elfu Moja?? Akanianbia jombaa, nauli muda huu ni buku mbili kama huna usiguse chuma.(Kwa lafudhi Ile ya maeneo ya kaskazini). Anadai kuwa wakati wa kurudia Kwa muda ule hatopata abiria ndo mana anachukua nauli mara mbili ya nauli elekezi.

Nilikaa nikafikiria Kwa muda kidogo nikaona hii Sasa si sawa. Na imekua ni mchezo wanaoufanya hasa nyakati za jioni, Kwa miezi ya mwisho wa mwaka sehemu ya nauli elfu Moja hutozwa Hadi shilingi elfu tatu Kwa abiria. Nikaamua kwenda pale getini gari zinapotokea, mana Kulikua na askari wa usalama barabarani. Namkuta yule konda ambayo nlikua nimeingoa Naye akanipa majibu ya hovyo. Nikajitambulisha na kuelezea kero yangu mbele ya yule kondakta, nikatoka na Mmoja Hadi kwenye gari. Nikamuobesha gari. Abiria wakaulizwa wakasema kweli wametangaziwa nauli mara mbili.

Yule afande wa kike alimmaindi sana yule konda na kuahidi atamuandikia faini siku inayofuata na kumtishia kufuta leseni yake ya usafirishaji wa abiria. Ila nilijiuliza jambo Moja, je wale polisi hawaijui hii kero, au wanapozwa kitu kidogo na hawa makondakta, yule kondakta alikua anafanya nini pale Kwa askari muda mfupi baada ya Mimi kumuuliza kwanini anatoza nauli mara mbili?? Au ndo alienda kuweka mazingira vizuri na bahati mbaya yake nikatokea na kutibua mpango wake. Je ni kanradi ka hao askari wanaokua zamu za usiku kupiga hayo madili machafu. Mamlaka za usafiri za mji huo hazitambui uwepo wa huu mchezo mchafu wa kuchelewesha abiria kufika majumbani kwao na kutozwa kiasi kikubwa cha nauli.

Kama mamlaka husika hazifahamu, naomba wafahamu hilo kupitia jukwaa hili na wachukue hatua stahiki Ili kuondoa kero hii
 
Hawa wanaiga matatu za Nairobi hawajui huku uchumi wa nchi ni mdogo
 
Hatari sana hili suala mbunge alisemee ila kweli ruti za jioni maeneo hayo hazina abiria Bora kupaki gari abiria walale kwa jirani
 
Back
Top Bottom