Mamlaka zidhibiti video zinazoonyeshwa ndani ya mabasi

Mamlaka zidhibiti video zinazoonyeshwa ndani ya mabasi

Kuna siku nilikua kwenye bus. Wameweka movie inaonesha utupu wa watu halafu bus limejaa wanafunzi. Nlimwambia konda bila kupepesa mdomo wakaitoa. Muda mwingine kabla ya mamlaka tuanze sisi abiria.
Safi sana...nyie ndio super woman👍
 
Hii huwezi kuelewa mpaka siku moja upande basi moja na bi mkubwa wako halafu wa~play hizo video.
 
Basi wasiwe wanawasha hizo Tv. Maana walikuwa wanaweka za Mkojani kwakuwa hqzina mmomonyoko wa maadili mkawa mnaponda, wakiweka za dini mnalalamika ubaguzi, mkiwekewa video za Harmo na wasafi bado mnalalamika.
 
Ukiwa unasafiri kwa mabasi ya kwenda mikoa mbalombali kuja video za muziki, filamu au vichekesho huoneshwa humo kuburudisha wasafiri. Lakini kwa baadhi ya video maudhui yanawwza kutazamwa na rika miaka zaidi ya 18.

Katika mazingira ya basi ambapo kuna watoto na wanandugu wanasafiri ni muhimu kudhibiti kabisa maudhui yanayorushwa.

Je, kuna mamlaka zinafuatilia na / ama kudhibiti hili?
Umegusa hisia zangu, nami nimeumia muda mrefu, juzi nilikuwa safarini nilikereka sana nikasema Lazima niende LATRA nikaongee nao kwamba wanahusika au hawahusiki maana ndio wanaotoa leseni na kusimamia usalama wa abiria.
 
Kila kitu sahv ushnzushz tu
Upuz ujing ujing unapewa kipaumbele
Kizaz cha sahv kishakata kamba

Ova
 
Kuna siku nilikua kwenye bus. Wameweka movie inaonesha utupu wa watu halafu bus limejaa wanafunzi. Nlimwambia konda bila kupepesa mdomo wakaitoa. Muda mwingine kabla ya mamlaka tuanze sisi abiria.

Hilo Basi la wapi?
Mabasi ya kaskazini yalishapita hizo zama za kale za mawe
Kule mabasi hupiga mziki wa taratibu na kwa sauti ya chini kabisa na mengine yakiwa safarini wanazima kabisa hizo ma tv. Kiujumla watu wa ukanda huo hawapendi makelele kwenye vyombo vya usafiri.....

Kuna siku nilipanda basi la kwenda mikoa ya watu hadi kichwa kiliniuma, sio kwa makelele hayo na kiyoyozi kimewasha utafikiri upo kwenye firiji!
 
Ww ni mjinga na huna hoja
Chombo cha kusimamia maadiri ni basata.

Sasa km basata wamepitosha bas tamthilia au movie iyo ina maadili yakutosha

Shida ya watu wengi wahapendi uharisia wa maisha kushikana kubusiana iyo ni uharisia na sio suala la maadili ilo
 
Nunua usafiri wako binafsi, hiki unachohitaji kifanyike ni ndoto za alinacha.
 
Kila kitu mamlaka we kama abiria chukua hatua , punguzeni malalamiko
 
Duh..so ni afadhali waonyeshe mizagamuano waachane na dini au sio
Hapana, wanaweza kuonyesha wanyama ama maudhui ya vijiji vya Tanzania si kutuonyesha dini za wazungu na waarab, zinatusaidia nini sisi Watanzania?
 
Kuna siku nilikua kwenye bus. Wameweka movie inaonesha utupu wa watu halafu bus limejaa wanafunzi. Nlimwambia konda bila kupepesa mdomo wakaitoa. Muda mwingine kabla ya mamlaka tuanze sisi abiria.
Saaafi kabisa.
 
Mimi nina bahati mbaya na ,nilipanda BM,ABC,ASANTERABI zote nilikutana na jamaa anitwa Mkojani anafanya ujinga ujinga wake mule hata hajanikera...so sina comment leo
 
Hapana, wanaweza kuonyesha wanyama ama maudhui ya vijiji vya Tanzania si kutuonyesha dini za wazungu na waarab, zinatusaidia nini sisi Watanzania?
Wewe kutokukuamini Mungu kusifanye na wengine wasimuamini. Solution ni wewe kununua mabasi yako utuonyeshe wanyama
 
Lakini siku hizi mabus mengi mapya yana ving'amuzi vya tv ni kuchagua tv gani tu unataka kuangalia
 
Back
Top Bottom