Mamlaka zijitahidi kuzuia wananchi wasigeuke kuwa " Wananchi wenye hasira Kali"

Mamlaka zijitahidi kuzuia wananchi wasigeuke kuwa " Wananchi wenye hasira Kali"

Salaam, Shalom!!

Mahusiano ya Dola na wananchi yanatakiwa kuwa sawa na mahusiano ya kipofu na Mwizi anayekula Kwa kificho na kipofu, Si vyema kukosea na kumshika mkono akastuka.

Watu wanapotea na kutekwa hadharani viongozi kimya, unyanyasaji Kwa wasio HAKI sasa haujifichi, wananchi wanachokozwa hapo.

Sasa wananchi wamefika hatua ya kutafuta namna ya kujilinda wao wenyewe ilhali KAZI ya Serikali ni kuuhakikishia umma ulinzi.

Wananchi wanapoungana Kwa nguvu ya asili Kwa hasira na visasi huitwa " Wana chi wenye hasira Kali". Hawa hawazuiliki.

Sijawahi ona au kusikia popote Duniani wananchi wenye hasira Kali wakipelekwa court, ni kama vile wao wakishahukumu inatosha. Nadhani ndio Hasa Nia ya kuzuia mikusanyiko isiyo na kibali Cha polisi Ili kuwazuia watu Hawa wasigeuke kuwa " wananchi wenye hasira Kali".

Angalizo: Wananchi wasichokozwe, HAKI itendeke Kwa wote, wasijepandwa na hasira Kisha kugeuka kuwa " Wananchi wenye hasira Kali ".

Ubarikiwe Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿.

Serikali kama haisadii wananchi kwa chochote kunakuwa hakuna haja ya hiyo serikali. Wizi wa Uchaguzi wizi wa rasilimali, teuzi za hovyo, inflation, TRA mbovu, Kodi lukuki.
 
Serikali kama haisadii wananchi kwa chochote kunakuwa hakuna haja ya hiyo serikali. Wizi wa Uchaguzi wizi wa rasilimali, teuzi za hovyo, inflation, TRA mbovu, Kodi lukuki.
Kama wamelala waamke.

Kwa yanayoendelea hayana faida yoyote Kwa mustakabali wa usitawi wa Nchi yetu.
 
Kama wamelala waamke.

Kwa yanayoendelea hayana faida yoyote Kwa mustakabali wa usitawi wa Nchi yetu.
Wengi wananchi wa kawaida Tanzania hata Duniani ni wajinga sana. Ukoloni uliwagawanya, Dola ya sasa Duniani inawaganya , viongozi wa Tanzania wanawagawanya.

Wako radhi wapigane na jirani yao kuhusu dini, chama, kabila. Huwa hawasikilizi sera, ukweli, tafiti.

Nchi zilizoendelea wamevuka hizo level. Wanaangalia record yako.
 
Back
Top Bottom