MwananchiOG
JF-Expert Member
- Apr 4, 2023
- 1,970
- 4,037
Kwa kawaida baada ya timu kupitia mafanikio makubwa mfululizo huwa kuna hali ya wachezaji kurelax na kucheza kwa mazoea wakiamini ubingwa unapatikana kirahisi, Ukiachana na suala la umri wa wachezaji ambao mara kadhaa hutumika kama kisingizio, Ila ukomavu kifikra na uzoefu wa mchezaji ni jambo linalo 'matter" sana.
Hapo ndipo ukiwa kama kiongozi unapaswa utambue kwamba hali ya timu ipoje, Wachezaji gani wamefikia peak ya carrier yao, wachezaji gani wamepoteza morali ya mchezo, wachezaji gani wameshuka kiwango nk.
Kisha baada ya kudadavua yote hayo, ili club kuendelea kuwa bora na kuperfom vizuri lazima uondoe na urekebishe baadhi ya maeneo, na inabidi uwe na jicho la kuona na kutambua kwamba ili timu iendelee kuperform lazima utoe oil chafu uweke mpya, utoe plug zilizochoka, ubadili tairi ili timu itembee, au kama tatizo ni dereva lazima uondoe dereva ulete dereva mpya, yote hayo lazima ufanye mapema kabisa kabla race haijakolea! Kadri unavyochelewa kuchukua maamuzi, ndivyo unazidi kudumbukia bondeni!