Manabii wa uongo

Manabii wa uongo

Eli Cohen

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2023
Posts
4,460
Reaction score
13,715
Tabu zetu zimetunyanyasa kwa kiwango kikubwa kupelekea kuwa wahanga wa watu wanaotutumia sisi kama fursa na wale wanaomtukuza shetani wao kupitia huduma wanazotufanyia.

Kwanini wanajiita manabii? ina maana miaka ya 2000 kurudi nyuma hawakuwepo au hawakutosheka kujiita "mchungaji". Jibu rahisi ni kuwa wanajiita hivi ili wawe marketable zaidi.

Ukweli ni kuwa wachungaji wengi wa kisasa ni "WAGANGA PRO MAX".

Sipatii picha miujiza yao inaachaga alama zipi katika roho zetu.

Mamlaka ya kulitamka jina la Yesu Kristo wanayo kwa maana hata biblia imeandika wataweza kutumia jina la Yesu wakiwa wanafanya huduma zao feki. Hii imepelekea wao kuwa wa ushawishi mkubwa sana katika jamii.

Mimi si mkamilifu wala mtakatifu ila mtu yoyote anefanya yafuatayo basi ni dalili halisia ya nabii feki.

1: Kulipa kiasi flani ndio ili upate huduma yake ana kwa ana

2: Kuuza maji, chumvi, vitambaa, mafuta.

3: Hana mafundisho ya kukuza watu kiroho bali ni stori tu za miujiza na kutetea muujiza wake.

4: Anang'ang'ania watu maarufu kanisani kwake.

5: Anajiita majina kama nabii, mtume, mwana wa Mungu.

6: Anatukuzwa yeye kanisani kwake kuliko Mungu.

7: Anakupangia sadaka ya kutoa huku akipenda kusema waliotoa sadaka kubwa ndio waliopata muujiza mkuu.

8: Hawakufundishi kujisamia kimaombi kwa maana wa wanajua utayapata majibu yako so wana market nguvu zao kukuonesha kuwa bila wao hautafika popote.
 
Hawa tunaweza kuwaita matapeli tu, hawana sifa za kuitwa manabii kwa mujibu wa maandiko ya biblia. Manabii gani wanakula bata pamoja na watawala?

Manabii gani wanaishi maisha ya anasa na ufahari? Manabii wana vitambi na shavu dodo! Wamenenepeana kuliko waumini wao kwa ukwasi walionao. Hawa ni wajanja fulani wenye kazi maalumu kwa jamii na sio unabii wa Mungu
 
Wengine walikuwa waganga wa kienyeji wakaona wanakimbiwa na wateja wanaokimbilia makanisani ikabidi wawafuate huko kwa kujifanya ni wataua wa Mungu
 
Tabu zetu zimetunyanyasa kwa kiwango kikubwa kupelekea kuwa wahanga wa watu wanaotutumia sisi kama fursa na wale wanaomtukuza shetani wao kupitia huduma wanazotufanyia...
Ni kweli ila hizo nyakati zilishatabiriwa kuwa wataibuka manabii wauongo!
 
Ndio unaijuaa kweli Leo ww mkuu..mbona wajanja washashtuka dini imekuwa fursa na watu wanatajirika haswa ww mwenyewe cjui unasubiri nn uckariri mistari yakuogofya watu na kuwapamba ukachukua spika lako na maiki ukiingia mbez pale stend ukizuga zuga na mistari na kelele nyingi na mziki mkubwaa na kuhakikishia mpk jion unaondoka na fungua la sadaka la kutosha ,mdg mdg unapata jina unafungua nawe taasisi yk ya kanisa ..n ushauri tu
 
Duh hatari ndugu
Ndio unaijuaa kweli Leo ww mkuu..mbona wajanja washashtuka dini imekuwa fursa na watu wanatajirika haswa ww mwenyewe cjui unasubiri nn uckariri mistari yakuogofya watu na kuwapamba ukachukua spika lako na maiki ukiingia mbez pale stend ukizuga zuga na mistari na kelele nyingi na mziki mkubwaa na kuhakikishia mpk jion unaondoka na fungua la sadaka la kutosha ,mdg mdg unapata jina unafungua nawe taasisi yk ya kanisa ..n ushauri tuuh
 
Hakika
Hawa tunaweza kuwaita matapeli tu, hawana sifa za kuitwa manabii kwa mujibu wa maandiko ya biblia. Manabii gani wanakula bata pamoja na watawala? Manabii gani wanaishi maisha ya anasa na ufahari? Manabii wana vitambi na shavu dodo! Wamenenepeana kuliko waumini wao kwa ukwasi walionao. Hawa ni wajanja fulani wenye kazi maalumu kwa jamii na sio unabii wa Mungu
 
Tabu zetu zimetunyanyasa kwa kiwango kikubwa kupelekea kuwa wahanga wa watu wanaotutumia sisi kama fursa na wale wanaomtukuza shetani wao kupitia huduma wanazotufanyia...
7. Inasemekana kuna Mchungaji maarufu Dar akipewa sadaka 5,000/= na Muumini, Mshirika au mgeni atasema "Ahsante sana" ila akipewa sadaka 10, 000/= atanena "Mungu akubariki sana"

Ubinadamu ni kazi/Humanity is a work.
 
Kwenye kuombea muungano kule dodoma walibahatika kuwepo kwenye orodha ya viongozi wa dini, walikuwepo manabii kama watatu wanne hivi nao walipewa nafasi ya kuombea muungano, hali kadhalika kulikuwepo na waimbaji injili waliozua mijadala mikali mitandaoni kwa kuharibu ndoa zao huku wakiendelea kuhudumu kana kwamba hawajui walichokifanya kwa ndoa zao takatifu. Sikuona mganga wa kienyeji/mchawi/mgaguzi aliyepata ualiko naye kuombea muungano wakati nao wana washirika wengi!
 
7. Inasemekana kuna Mchungaji maarufu Dar akipewa sadaka 5,000/= na Muumini, Mshirika au mgeni atasema "Ahsante sana" ila akipewa sadaka 10, 000/= atanena "Mungu akubariki sana"

Ubinadamu ni kazi/Humanity is a work.

hahah

Yeah humanity is a burden
 
Hahahahhh
Kwenye kuombea muungano kule dodoma walibahatika kuwepo kwenye orodha ya viongozi wa dini, walikuwepo manabii kama watatu wanne hivi nao walipewa nafasi ya kuombea muungano, hali kadhalika kulikuwepo na waimbaji injili waliozua mijadala mikali mitandaoni kwa kuharibu ndoa zao huku wakiendelea kuhudumu kana kwamba hawajui walichokifanya kwa ndoa zao takatifu. Sikuona mganga wa kienyeji/mchawi/mgaguzi aliyepata ualiko naye kuombea muungano wakati nao wana hahhahaha
 
Tabu zetu zimetunyanyasa kwa kiwango kikubwa kupelekea kuwa wahanga wa watu wanaotutumia sisi kama fursa na wale wanaomtukuza shetani wao kupitia huduma wanazotufanyia.

Kwanini wanajiita manabii? ina maana miaka ya 2000 kurudi nyuma hawakuwepo au hawakutosheka kujiita "mchungaji". Jibu rahisi ni kuwa wanajiita hivi ili wawe marketable zaidi.

Ukweli ni kuwa wachungaji wengi wa kisasa ni "WAGANGA PRO MAX".

Sipatii picha miujiza yao inaachaga alama zipi katika roho zetu.

Mamlaka ya kulitamka jina la Yesu Kristo wanayo kwa maana hata biblia imeandika wataweza kutumia jina la Yesu wakiwa wanafanya huduma zao feki. Hii imepelekea wao kuwa wa ushawishi mkubwa sana katika jamii.

Mimi si mkamilifu wala mtakatifu ila mtu yoyote anefanya yafuatayo basi ni dalili halisia ya nabii feki.

1: Kulipa kiasi flani ndio ili upate huduma yake ana kwa ana

2: Kuuza maji, chumvi, vitambaa, mafuta.

3: Hana mafundisho ya kukuza watu kiroho bali ni stori tu za miujiza na kutetea muujiza wake.

4: Anang'ang'ania watu maarufu kanisani kwake.

5: Anajiita majina kama nabii, mtume, mwana wa Mungu.

6: Anatukuzwa yeye kanisani kwake kuliko Mungu.

7: Anakupangia sadaka ya kutoa huku akipenda kusema waliotoa sadaka kubwa ndio waliopata muujiza mkuu.

8: Hawakufundishi kujisamia kimaombi kwa maana wa wanajua utayapata majibu yako so wana market nguvu zao kukuonesha kuwa bila wao hautafika

nawafata wenyewe kwa tamaa ya mali hamtaki kufanya kazi,

Tabu zetu zimetunyanyasa kwa kiwango kikubwa kupelekea kuwa wahanga wa watu wanaotutumia sisi kama fursa na wale wanaomtukuza shetani wao kupitia huduma wanazotufanyia.

Kwanini wanajiita manabii? ina maana miaka ya 2000 kurudi nyuma hawakuwepo au hawakutosheka kujiita "mchungaji". Jibu rahisi ni kuwa wanajiita hivi ili wawe marketable zaidi.

Ukweli ni kuwa wachungaji wengi wa kisasa ni "WAGANGA PRO MAX".

Sipatii picha miujiza yao inaachaga alama zipi katika roho zetu.

Mamlaka ya kulitamka jina la Yesu Kristo wanayo kwa maana hata biblia imeandika wataweza kutumia jina la Yesu wakiwa wanafanya huduma zao feki. Hii imepelekea wao kuwa wa ushawishi mkubwa sana katika jamii.

Mimi si mkamilifu wala mtakatifu ila mtu yoyote anefanya yafuatayo basi ni dalili halisia ya nabii feki.

1: Kulipa kiasi flani ndio ili upate huduma yake ana kwa ana

2: Kuuza maji, chumvi, vitambaa, mafuta.

3: Hana mafundisho ya kukuza watu kiroho bali ni stori tu za miujiza na kutetea muujiza wake.

4: Anang'ang'ania watu maarufu kanisani kwake.

5: Anajiita majina kama nabii, mtume, mwana wa Mungu.

6: Anatukuzwa yeye kanisani kwake kuliko Mungu.

7: Anakupangia sadaka ya kutoa huku akipenda kusema waliotoa sadaka kubwa ndio waliopata muujiza mkuu.

8: Hawakufundishi kujisamia kimaombi kwa maana wa wanajua utayapata majibu yako so wana market nguvu zao kukuonesha kuwa bila wao hautafika popote.
Mtu hujaribiwa kwa tamaa zake mwenyewe, omba Mungu kisha fanya kazi kwa bidii, hakuna muujiza wa mali zaidi ya utapeli.
 
Aisee ni hatari tupu..hivi na haya makanisa ambayo wanavaa manguo meusi na nyeupe siku maalum na kunyoa viduku ni ya pande zip?
 
Back
Top Bottom