Manabii wanapingwa sana ila alichokifanya nabii Clear Malisa ni kitendo cha kishujaa.

Tatizo letu hatufuatilii mambo zaidi ya tulipoishia kufundishwa, hii nayo ni safari ndefu sana katika kuelewa.
 
Sahihi
 
Mtaji viongozi wa dini yetu ya kikristo ni ujinga tulionao waamini , michango michango, matoleo sijui mavuno sijui Nini , mbona waislamu viongozi wao ni wakawaida tu hatusikii malalamiko ya michango Wala maigizo ya kuponyana na kufufuana. Ukitaka kubatiza mtoto v8z8ngiti kibao. Ukitaka kuoa vizingiti , kuachana napo tabu.
mweeeeee kwale mayito kwenoko ,kulagha nenga
 
Hao manabii waafrika wameifanya waafrika kuanza kukubalika Marekani,Ulaya na Asia kuwafundisha.Wamekubali kuwa waafrika tunajua na tunaweza

Manabii wanaokubalika sana nje ya nchi ni huyo Ulbert Angel,Nabii Lovy Elias Nabii Passion Java wanazunguka mabara yote wanaokubalika na kujaza watu wazungu,Wahindi nk wanapokelewa vizuri

Wawe wa kweli au la ninachokiona ni kuwa waafrika tumeanza kukubalika kwenye hayo mabara ni dalili nzuri yaweza kuwa Mungu anataka kufungua milango ya waafrika kuanza kupeleka Injili kwenye Mabara yote na kukubalika huko.Naona mwelekeo mzuri
 
Mkuu endelea kujifunza lakini kikubwa ruhusu kuwa na akili huru unaweza ukahisi unaona kumbe unaonwa.
 
Be blessed
 
Wajinga ndio mtaji wa manabiii wa hovyo
 
Ujinga kama maarifa ni suala la kukubali tu,
Ukikubali ujinga unakuwa mjinga halkadhalika ukikubali maarifa unakuwa mwerevu.
 
Nyie kina Mlaki mnakuwaga na matatizo tu karibia wote kwenye ukoo wenu. Yule mdogo wenu alienda kugombea ubunge nilijua ndo popoma kuliko wote ila sasa nimekuona wewe na mawazo yako nime change mtazamo kwa kweli.
 
Nyie kina Mlaki mnakuwaga na matatizo tu karibia wote kwenye ukoo wenu. Yule mdogo wenu alienda kugombea ubunge nilijua ndo popoma kuliko wote ila sasa nimekuona wewe na mawazo yako nime change mtazamo kwa kweli.
Sina mdogo katika ukoo aliyewahi kufanya hivyo, huenda unachanganya
 
Wajinga ndio mtaji wa manabiii wa hovyo
Hao wanaitwa manabii wa uongo wamekuja kuliamsha kanisa liwe na uamsho sababu wanaojazana huko wanatoka kwenye hayo Makanisa makubwa

Ni kuwa hayo makubwa hayana majibu Kwa shida za waumini wao wako nazo .Waamke wawe na majibu Kwa shida za waumini wao sio tu kukusanya sadaka
 
Malisa+Mlaki=Wapigaji

Naona baada ya mwitikio kuwa mdogo na makusanyo kuwa tofauti na mlivyotegemea muhasibu umeona usogee mitandaoni kuwaandaa zombies wenu kuhusu warsha mtakayoifanya mwisho wa mwaka huu mkijidai kufunga mwaka kwa unabii.
 
Unaweza kuniambia hapa Kanisa linanisaidia vipi leo nikilala njaa?kodi yangu ya nyumba ikiisha Kanisa litanisaidiaje?

Hakuna mtatuzi wa shida za mtu zaidi ya yeye mwenyewe kujua namna ya kupambana nazo huko Kanisani ni pa kwenda kusali kuomba Mungu anionyeshe mimi muumini namna bora ya kupambana na changamoto za dunia yangu siyo kuwekewa mikono na the so called nabii kwa gharama ya 100K ndiyo changamoto ziondoke.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…