Manchester United ni ile ile, bado kuna kazi ya kufanya

Manchester United ni ile ile, bado kuna kazi ya kufanya

JohnGarcia

New Member
Joined
Jun 12, 2024
Posts
1
Reaction score
0
Ikiwa ni mchezo wa pili toka ligi ya England ianze Manchester United imepoteza mchezo wake baada ya kukubali kipigo cha mabao 2 kwa 1 kutoka kwa Brighton & Holves Albion huku mabao ya Brighton yakifungwa na Danny Welbeck na Joao Pedro huku Unitedwakifunga bao la kufutia machozi kupitia kwa Amad Diállo.

Licha ya kutandaza kandanda safi la kuvutia na kutengeza nafasi za kutosha bado United imekuwa na changamoto ya umaliziaji na kutokuwa makini kwenye eneo la ulinzi limekuwa na shida kiasi hukaribisha mashambulizi mengi katika eneo lao.

Kitu nilichokibaini kwenye mchezo wa jana ni kuwa United ni ileile hakuna kitu kilichibadilika licha ya kuimarika kwenye maeneo machache bado wana kazi kubwa ya kufanya ili kupata mafanikio katika michuano mbalimbali wanayoshiriki msimu huu.

Mashabiki wa Manchester United wasitegemee makubwa msimu huu, ingawa mabadiliko ya kiuongozi yanaweza kuleta mwanga ndani ya misimu michache ijayo.
 
Back
Top Bottom