Kadri siku zinavyozidi kwenda ili niwe na amani itabidi niache kutizama mpira wa timu yangu hii Man U. Kwa kweli hii siyo Machester United ni man u. Yaani wachezaji wetu ni kama vile mpira wamejifunzia mchangani na ninawasiwasi na uwezo wa ni mdogo sana pengine hata wa kiakili, yaani mchezaji hata kupiga pass hawezi, boli control hakuna, accuracy zero sijui huwa wanasajiliwa kwa vigezo vipi.
Kweli leo United tunacheza na Bournemouth sisi tunakuwa underdog? Hawa wamiliki naona hawako serious. Mchezaji kama Malacia anarukaru tu mule ndani. Huyu kocha kwa hawa wachezaji atadhalilishwa zaidi ETH, kwanza hakuwaleta yeye.
Huwezi ukawa na wachezaji wa timu kubwa ambao hawajiamini na hata chenga moja hawawezi piga. Ingepaswa January hii kocha apewa fangio afagie nyumba, hata Pep Gadiola alipokwenda City alifagia nyumba.