Wala sihuzuniki kabisa, Bora unaona makapi ni yapi na vipi unaweza kuyaondoa. Haya ni mchanganyiko wa mazao ya recruitment mbovu, maamuzi mabovu (Kwa baadhi ya wachezaji), kocha anajaribu kutoa muda Kwa wachezaji wote Ili basi Kila mmoja aoneshe alichonacho.
Nusu ya magoli tuliyofungwa ni ya set pieces, mengi ya haya magoli ni wachezaji wenyewe kushindwa kufanya marking, awareness ya mchezaji binafsi mfano goli la Leo si suala la kocha kukufundisha ni mchezaji mwenyewe tu ameshindwa kujitambua afanye Nini, ni kama mtu mzima kufundishwa kuchamba kitu ambacho anatakiwa awe anajua automatically.
Mafuta na maji yataanza kujitenga, nilishasema Kuna wachezaji utaona wanaanza kujitoa taratibu, performance zao utaona zitaanza kukukera na hapo ndipo utaona uhitaji wa wachezaji "PUNDA" wenye akili na si wapaka poda.
Nasemaje Bora tufungwe lakini at least tuone kocha anajaribu kuanza kutafuta kitu gani. Sisi si timu ya kuwa na kocha zaidi ya misimu mitano kama timu Fulani halafu tuishiwe kusifiwa tu pira mchuzi sijui Haram football, hivyo wachezaji lazima watambue hili.