Manchester United (Red Devils) | Special Thread
Mashabiki wa utd tuwaombe msamaha makocha wote walipita hapo sio makes yao labda tu kama wao ndio waliohusiku kutuletea hawa wachezaji. Mashibiki inapaswa wagome kwenda uwanjani na kushinikiza timu yote mikatava ivunjwe tusajili upya United inafabase kubwa sana duniani tupo tayari kuchangia hela ya kuvunja mikataba ya hawa ngedere.
Ndio sababu Amorim alitamani aje baada ya msimu huu kuisha, kwa sasa binafsi siwezi kumlaumu kocha. Hata uongozi wa timu pia ulifanya makosa, wangeacha Ruud aendelee mpaka mwisho wa msimu.
 
Ndio sababu Amorim alitamani aje baada ya msimu huu kuisha, kwa sasa binafsi siwezi kumlaumu kocha. Hata uongozi wa timu pia ulifanya makosa, wangeacha Ruud aendelee mpaka mwisho wa msimu.
Hizo ni excuse tu, ila mnagongwa kinyama.
 
Poleni sana. Historia huwa ina tabia ya kujirudia.
1734884678763.jpg
 
Wala sihuzuniki kabisa, Bora unaona makapi ni yapi na vipi unaweza kuyaondoa. Haya ni mchanganyiko wa mazao ya recruitment mbovu, maamuzi mabovu (Kwa baadhi ya wachezaji), kocha anajaribu kutoa muda Kwa wachezaji wote Ili basi Kila mmoja aoneshe alichonacho.

Nusu ya magoli tuliyofungwa ni ya set pieces, mengi ya haya magoli ni wachezaji wenyewe kushindwa kufanya marking, awareness ya mchezaji binafsi mfano goli la Leo si suala la kocha kukufundisha ni mchezaji mwenyewe tu ameshindwa kujitambua afanye Nini, ni kama mtu mzima kufundishwa kuchamba kitu ambacho anatakiwa awe anajua automatically.

Mafuta na maji yataanza kujitenga, nilishasema Kuna wachezaji utaona wanaanza kujitoa taratibu, performance zao utaona zitaanza kukukera na hapo ndipo utaona uhitaji wa wachezaji "PUNDA" wenye akili na si wapaka poda.

Nasemaje Bora tufungwe lakini at least tuone kocha anajaribu kuanza kutafuta kitu gani. Sisi si timu ya kuwa na kocha zaidi ya misimu mitano kama timu Fulani halafu tuishiwe kusifiwa tu pira mchuzi sijui Haram football, hivyo wachezaji lazima watambue hili.
 
Back
Top Bottom