Nilishawaambia fans wenzangu, hii timu ukitaka irudi taratibu kule juu basi ziletwe mashine za kazi, Kwa system ya huyu kocha Inahitaji watu wa kazi wenye akili ya mpira. Wazee back three then una mido wawili tu na winga wasiokaba sawa sawa unadhani unahitaji watu wa aina gani kuweza kukava space ground kubwa namna hii pindi tu timu pinzani wakiwa kwenye transition?, ni wachezaji punda pekee na wenye akili ndio wanaweza Hilo.
Wazee 3-4-2-1 siyo mfumo wa kinafiki hata kidogo kwasababu kama huna watu sahihi ni rahisi kuwa exposed, kwanza lazima uwe physically fit, mentality fit, angalia Sasa mido yetu mainoo yeye hii itampa tabu kwasababu si aina ya wachezaji wanaweza kuingia direct kwenye hii system, kwanza anapoteza mipira hovyo na unajua ukipoteza mpira tu nyuma wako watu jua mmeliwa, si mzuri kwenye kuihamisha timu Kwa haraka kama angekuwa na uwezo hata nusu tu ya prime eriksen ingekuwa nafuu, ukimpress kisawa sawa anakuachia mpira, si aina ya mchezaji anayependa kukimbizwa sana, huu ni mfano tu wa wachezaji wetu wengi.
Haiwezekani useme ni tatizo la kocha wakati unaona kabisa unafungwa kwasababu ya wachezaji wenye ubora mdogo, kwanini usicheze na intensity ile ile au inayokaribiana na ile ya mechi kubwa, tungekuwa tunacheza Kila siku kama tulivyocheza na Liver tungekuwa wapi Sasa hivi?
Mpira ni desire, mechi na Southampton tulifundishwa mpira wa namna backthree system inatakiwa icheze vipi, kiuchezaji wale watoto wa st. Mary walituacha mbali sana, eti fans huko wanaosema UTD imerudi, this is insane hahh. Timu wachezaji wanajigonga wenyewe, hawajiamini kabisa haha. Mid table teams kama N.forest, Bournemouth, Newcastle hizi zote zimetufundisha mpira, haya timu za mkiani kama Ipswich imewafundisha kina Bruno.