[emoji1787][emoji1787][emoji1787] Huyu Harmorapa hana muda mrefu ataanza kuikumbuka timu yake ya Sporting Clube de Portugal, hii Man Utd yetu ni kama roba la misumari kila ukijitahidi kulibeba vizuri na lenyewe ndio linazidi kukutoboa.
Ndani ya muda mfupi tu Ruud van Nistelrooy alikua ameshaanza kutengeneza chemistry ya timu na kila mechi tulikua tunapata matokeo ya kuridhisha, vile uongozi wa timu haupendi kuona mashabiki tukiwa na furaha ya kudumu badala ya kumpa Nistelrooy muda mpaka dirisha dogo, tumemtimua na kulazimisha kumleta Amorim ambae aliomba apewe muda mpaka mwisho wa msimu ndio aje Utd.