Mwisho wa Msimu mambo yatakuwa kama hivi,
1. Liverpool atakuwa ameshafikisha mapoint kibao(Bingwa tayari)
2. Arsenal atakuwa kwenye vita kali ya kupambania nafasi yake ya Tatu hapa ndo msemo wa linda ulichonacho utaanza kazi.....Tumaini la ubingwa litapotea kabisa
3. Nottingham atakuwa kila mechi anacheza jihad ili tu kusalia nafasi ya pili
4. Chelsea,Tottenham,aston vila, man city na takataka nyingine zote hao watakuwa kwenye vita kali sana watarogana, Kupigana mabuti, fukuza fukuza ya makocha itashamiri mwisho wa msimu hii yote itasababishwa na kugombania tonge la Nne(Nafasi ya nne)
5. Man utd itakuwa kwenye vita kali na wakina ipswich na Leicester wanagombana wasishuke daraja,
Yani hapo Mbungi litapigwa Man utd atahonga hata VAR zisiletwe uwanjani... ili tu abakishwe Epl asiende mchangani. Kwa dokezo tu kipindi hiki Gabachori wenu Amorim atakuwa anapangiwa kikosi na yule kocha wenu Van ndame.