Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
Nakumbuka miaka hiyo ya nyuma naanza kazi kwenye kampuni moja ya kigeni iliyokuwa imeingia tu nchini. Walinunua gari 6 mpya, dereva mmoja baada ya kukabidhiwa gari mojawapo, alisafiri nayo kwenda Dar. Kurudi, akawa ameweka stickers 2, zina picha ya duma, halafu chini ya ya picha kumeandikwa, "Manyanga chini", HR Mkanada kuona tu zile stickers, akamwambia yule dereva kwa kufoka, ' remove those stupid stickers, they mean nothing to a sensible world"
Kwa nchi au kampuni kuna nembo zilizokubaliwa, ndiyo zinazotakiwa kuwekwa kwenye mali za nchi. Hizo huwa ni utambulisho wa haraka.
Slogans za watawala hazitakiwi kuwekwa kwenye vitu vya kudumu vya Taifa. Zinaweza kuwekwa kwenye vitu ambavyo vitaondoka utawala wake unapoondoka, kama vile mabango ya uhamasishaji.