Maneno na kauli za Masikini wanapojifariji

Maneno na kauli za Masikini wanapojifariji

Masikini walifurahi Sana jiwe alipowashughulikia matajiri, wakiamini umasikini wao chanzo ni tajiri.
wengine walifurahi sana mzee rugemalila kusota ndani mda mrefu...siku anatolewa akafatwa na VX, mafukara wakapigwa na butwaa.
 
Tatizo mijitu mingine ni mivivu by nature, leo nimekuja site flani hivi, kulikuwa na kifusi cha kuhamisha, kama lorry mbili, nikaona vijana wamekaa chini ya mwarobaini wanapiga soga, nikwaambia kuna laki 1 hapa ingizeni hiki kifusi kwenye shimo, shimo lenyewe lipo kama mita 30 tu toka kwenye kifusi, eti hawataki, kazi ngumu, halafu ukiwaangalia hata uhakika wa msosi hawana, hivi hii inakuwaje hii? Mbona mi sielewi?! Nikapigia simu vijana wangu wa kazi, wakaingiza chote chapchap tena kwa elfu hamisini tu, nusu yake
Mkuu, malezi mabaya, ulevi na marafiki wabaya pia huchangia uharibifu na umasikini wa vizazi vyetu.
Mimi kijana wangu amemaliza kidato cha nne juzi, sasa kuna baadhi ya vitu vilitakiwa vihamishwe kutoka mkoa mmoja kwenda mkoa mwingine, hiyo kazi nilimpa yeye na akaniuliza "baba sasa nafanyaje?" Nikamjibu kaniletee beer nyinywe kwanza alafu nitakupa maarifa. Basi mama yao akaanza kugomba kwamba nampa kijana kazi ngumu, then sikumjibu. Jioni niliporudi toka kwenye mizunguko yangu nikamkabidhi kijana ticket ya kusafiri kesho yake, Kisha nikamwambia akifika aniambie ni pesa ngapi ya gharama kusafirisha vile vitu.
Basi baada ya siku mbili, narejea toka kitaa nikakuta mizigo imeshafika, sikutaka hata kuiangalia wala kushukuru.
Then maisha yakaendelea...😂😅
 
Mwanamke mmoja mlokole alishaniambia aheri niwe na mwanamme mume wangu msimangaji nikiwa kwenye benz nalia kuliko kwa mwanamme asiye na kitu eti ana maneno matamu lakini kanipakiza juu ya baskeli
 
Tatizo mijitu mingine ni mivivu by nature, leo nimekuja site flani hivi, kulikuwa na kifusi cha kuhamisha, kama lorry mbili, nikaona vijana wamekaa chini ya mwarobaini wanapiga soga, nikwaambia kuna laki 1 hapa ingizeni hiki kifusi kwenye shimo, shimo lenyewe lipo kama mita 30 tu toka kwenye kifusi, eti hawataki, kazi ngumu, halafu ukiwaangalia hata uhakika wa msosi hawana, hivi hii inakuwaje hii? Mbona mi sielewi?! Nikapigia simu vijana wangu wa kazi, wakaingiza chote chapchap tena kwa elfu hamisini tu, nusu yake
Wewe una matatizo makubwa. Unataka kulazimisha watu wafanye kazi ngumu kwa ujira unaoamua wewe kwa sababu tu wana shida?
 
Sio ujira ninao taka mimi, mimi nimetoa offer, means unaweza ukasema unataka uongezewe kiasi gani, lakini sio kusema tu hiyo kazi ngumu, sifanyi, hilo ni tatizo
Basi walikuwa na mipango mingine au kazi kama hizo hawazifanyi. Kila mtu ana haki ya kuchagua kazi . Sioni unacholalamikia hapa.
 
Majumba na pesa vyote vya kupita yakiwemo na magari ,hatukatai Ila pambana vipitie kwako na wewe sasa
 
Back
Top Bottom