Hili suala la CORONA limekuwa kizungumkuti kwa sasa kwenye jamii yetu.
Nguvu kubwa inayotumika kuwashawishi watu wapatiwe chanjo pia nguvu kubwa inayotumika dhidi ya watu wanaotoa maoni yao dhidi ya chanzo vinazidi kuzua maswali na hofu kuu kwa wananchi.
Nadhani huu ndio muda muafaka kwa wataalamu kulitolea ufafanuzi wa kitaalamu hizi chanjo na sio kuwazodoa watu wanaopingana na chanjo.
Hayo malumbano ndio yanazidi kuwaweka wananchi njia panda na kuwajaza hofu.
Kama kupata chanjo ni khiyari ya mtu basi ibakie tu hivyo hivyo na kama kunatokea mtu anatoa maneno yanayoonekana kupotosha basi jukumu la wataalamu ni kutoa ufafanuzi kwa wananchi ili washawishike na sio vitisho na maneno ya kejeli.
Kupanic baada ya kutoa maelezo kunaleta tafsiri ya kuwa hao wanaopanic huenda wana maslahi na hii chanjo kwa namna moja au nyingine.
Mungu ibariki Tanzania
Zile si hoja za Gwajima,bali ndio sayansi ilivyo....anayedhani kwamba Gwajima anaongea upuuzi basi huyo ndio mwenye matatizo kichwani.
Ukitaka kujua kama hoja alizotoa Gwajima(si hoja za Gwajima) ndio ukweli wenyewe,subiri uone kama kuna mtu yeyote atajitokeza kuweka debate naye hadharani....siasa na sayansi ni mambo mawili tofauti kabisa....
Siasa ndio iliyoruhusu sigara ipigwe chapa ya TBS wakati mtengenezaji wa sigara ameandika kwamba uvutaji wa sigara ni hatari kwa afya yako.
NB:
1.Chanjo haina hata miaka 2 tangu igunduliwe,tutajuaje madhara yake baada ya miaka10 ijayo kwa mdungwaji?...na ndio maana wataalam halisi wa sayansi wanasema chanjo hii imetumia muda mfupi sana hadi kutumika....yapo madawa ambayo yanaweza kukusababishia kifo hata baada ya miaka 15 au hata 20 baada ya kuanza kutumia, mfano ARVs...
2.Hakuna peer reviewed scientific paper inayoonesha kwamba effects za muda mfupi,kati na mrefu za chanjo hii baada ya kudungwa,HAKUNA....yaani ugunduzi mpaka utumiaji wa chanjo hii haukufuata taratibu za kisayansi na ndio maana hata hao mabwana zao FDA hawajaidhinisha.
3.Hata ukidungwa haina maana kwamba you are safe,bado unaweza kuambukizwa ama kuambukiza(ingawa wanasema unapunguza uwezekano,but you are not free) na bado unatakiwa kuvaa barakoa....sasa nini faida za maana za chanjo hii?
4.Utadungwa kwa variant moja,ikibadilika chanjo haina maana tena,unatakiwa kudungwa nyingine...hivi watu hawaoni huu upuuzi kweli?
5.Nini kimetulinda tangu mwaka 2019 na hii covid19 hadi sasa ilihali asilimia kubwa yetu tulikua hatuvai barakoa na bado hatuvai,tunachangamana hadi kwenye viwanja vya michezo...mfano fikiria pale Kariakoo mtaa wa Kongo watu walivyo wengi na hawavai barakoa....
Ndio maana hata watu wa 'uswahilini' ambao hawajaenda shule wanaelewa hoja hizi,maana ziko wazi kabisa kumshtua mtu kutoka usingizini...ila kuna watu aidha kwa kujidanganya wamesoma ama wana maslahi kwenye hili suala ndio maana wanaunga mkono.
Kupinga hoja hizi yahitaji kujitoa ufahamu kwanza.....maana hata Antonio Fauci sijamwona akipinga hoja hizi wakati yeye ndio kiongozi chanjo hizi.