Maneno ya Kiswahili yaliyopo mbioni kuharibiwa na vilaza

Bora hao kuliko wale wa xaxa, cc, apana, auheni, haueni, kikao kimegairishwa, ridhiki, mamb, taadhari, nk

Hizo ulizoandika mara nyingi hazikwepeki na mtu hafanyi kusudi. Hebu niwaachie homework ili tuone wengine wapo humu humu

Ipi ni sahihi kati ya

TASFIDA au TAFSIDA
LADHA au RADHA
LAMBA au RAMBA
CHANUO au CHANIO
MUHSINI au MUKSINI
CHAKARIKA au CHAKALIKA
DHARURA au DHARULA au DHALURA
SAHIHI au SAINI (nomino)
AMEPOZA CHAI au AMEPOOZA CHAI
KUNYWA DAWA au KULA DAWA
ISIVYO BAHATI au BAHATI MBAYA
MTOTO ANAKUA au MTOTO ANAKUWA
KIKAO KIMEAHIRISHWA au KIKAO KIMEHAIRISHWA au KIKAO KIMEGHAIRISHWA
 
Sahihi lakini kuna standard language,ile ambayo inatumika CNN au BBC
 
Dialect ni tofauti na pronunciation.
 
Ila lugha huwa ina tabia ya kubadilika kilingana na vizazi. Maneno ya lugha ya kiswahili ya miaka ya 1980 mengi yamebadilika
Basi itabidi tuawazoo tu vilaza wa insta wanasema "tyuu" badala ya "tu" , "piah" badala ya "pia"
 
Mimi nachukia kuna watu wanasema ela badala ya hela, aya badala ya haya. akitaka kusema hana hela anasema ana ela. maniiiina
Aisee hunizidi mimi katika kuwachukia watu wa namna hiyo. Halafu watu maarufu ndio wanaotuharibia jamii unakuta jitu kubwa kabisa lakini linavyoongea au kuandika sasa, ni kinyaa tupu!
 
Gentleman,
umeona hapo katikati kwenye silabi k iliyofuatiwa na m lugha ya kiswahili ilivyohatibiwa kwa makusudi?
Vijana wa lumumba ,sio kwamba hamna akili nikwamba hamna pesa na mnatamani muwe nazo nawawaonea huruma sana 😭
 
Siku hizi wavivu wa lugha hawaandiki au kutamka tena
Sebule- wanasema seble
Muziki- wansema mziki
Muda- wansema mda!
na huyu mtaalamu wa lugha wanasema yeye anasema wansema....😎
 
Basi itabidi tuawazoo tu vilaza wa insta wanasema "tyuu" badala ya "tu" , "piah" badala ya "pia"
Dogo zangu moja siku hiyo limetuma sms ndefu ndefu ivi kuifungua nakuta mbwembwe kibao maeksi eksi mengi, ma sii sii ya kutosha na ujinga mwingine mwingine mfano wa huo

Nikaelewa vizuri kabisa ujumbe ule alikuwa ana mambo ya msingi tu kuhusu chuoni kwao lakini nikauchuna. Amekaa siku hiyo anapiga simu bro sasa unajua vilikwenda vikarudi nikamwambia mimi sms yako sikuweza kuisoma kwanza nikajua labda umekosea namba. Mbona alinyooka tangu siku hiyo

Hawa wavurugaji wa lugha ukitaka wasiendelee kwanza mshushue papo hapo wakati anaongea au anaandika, mbona mwenyewe anaacha
 
yaani uone njaa halafu usindwe kuisikia kweli..!?πŸ€”πŸ€”πŸ€”
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…