Maneno ya Kiswahili yaliyopo mbioni kuharibiwa na vilaza

Maneno ya Kiswahili yaliyopo mbioni kuharibiwa na vilaza

Ni wewe umesema gentleman, sasa pale manyara na mbulu kuna shamba gani la ghali? Babu yangu mwenyewe kanunua zaidi ya hekari 1000 achana na mzee?
Tanzania ina mamilioni ya hekta za ardhi isiyotumika kila pembe ya nchi, huna haja ya kung'aa macho na kushangaa maghorofa mjini gentleman:putinWalk:
 
Tanzania ina mamilioni ya hekta za ardhi isiyotumika kila pembe ya nchi, huna haja ya kung'aa macho na kushangaa maghorofa mjini gentleman:putinWalk:
Nashangaa vipi vitu vya kijinga gentleman binafsi mimi sio raia wa nchi ya kijinga kama unayotoka wewe gentleman.
 
Hana muda na ana muda ni vitu viwili vyenye maana mbili tofauti, kwahiyo

"Hana muda" maana yake hajapata muda
"ana muda" maana yake anao muda

Kwahiyo huwezi kurekebisha Hana muda kuwa ana muda maana ni vitu viwili tofauti vyenye maana tofauti.
I know all that
nilichoandika ni kile ninachokisikia na kukiona wakiongea na kuandika miaka hii tofauti na zamani
Mf. Mtu anasema: "Huna shilingi laki moja uniazime?" Akimaanisha "Una shilingi laki moja uniazime?"
Au mtu anasema: "Hunataka kusafiri wakati una nauli? Akimaanisha "Unataka kusafiri wakati huna nauli?"
Huu ndiyo uharibifu wa lugha unaojadiliwa hapa.
 
I know all that
nilichoandika ni kile ninachokisikia na kukiona wakiongea na kuandika miaka hii tofauti na zamani
Mh. Mtu anasema: "Huna shilingi laki moja uniazime?" Akimaanisha "Una shilingi laki moja uniazime?" Huu ndiyo uharibifu wa lugha unaojadiliwa hapa.
Aah sawa hapo nimekusoma kweli hao wapo wengi
 
Lisaa badala ya Saa
neno hili huharibiwa sana wapuuzi wa Dar
Ona sentensi hii: Njooni baada ya saa moja . 1. Inaweza kuwa ni saa moja (i.e wakati) eg ya jioni au asubuhi. 2. Inaweza kuwa ni baada ya muda wa dakika 60 kupita. Suluhisho: ongeza li kwenye saa.
 
Ila lugha huwa ina tabia ya kubadilika kilingana na vizazi. Maneno ya lugha ya kiswahili ya miaka ya 1980 mengi yamebadilika
Ni kweli. Ila kuna maneno kubadilika na maneno kuharibiwa kwa kukosewa na yakaleta maana nyingine kabisa. eg Tafadhari husichukue ile gali ya wakiri (Tafadhali usichukuwe lile gari la wakili)
 
Ni kweli. Ila kuna maneno kubadilika na maneno kuharibiwa kwa kukosewa na yakaleta maana nyingine kabisa. eg Tafadhari husichukue ile gali ya wakiri (Tafadhali usichukuwe lile gari la wakili)
Lahaja za kimaeneo. Kiswahili cha mtu wa kanda ya ziwa nitofauti na mtu wa kusini. Vile vile ni tofauti kati ya pwani na kaskazn. Mfano kanda ya ziwa maneno kama usichukue wanasema husichukuwe [wasukuma] maneno kama lala watasema rara nk
 
Kuandika hakuna uhusiano wowote na lahaja hasa kwenye nchi moja. Ndiyo maana kuna shule za kujifunza ili tu-harmonize namna lugha inavyoandikwa. Tanzania tumekubaliana namna ya kuandika maneno ya kiswahili ili tuwe na standard ya aina moja, kuondoa migongano.
 
Ndan ya nchi moja lahaja zipo tu. Ndio maana nimekupa mfano. Kwa maana lahaja huwa zao la lugha mama. Mpare ni ngumu kutofautisha tha na sa msukuma u ataweka hu nk
 
Ndan ya nchi moja lahaja zipo tu. Ndio maana nimekupa mfano. Kwa maana lahaja huwa zao la lugha mama. Mpare ni ngumu kutofautisha tha na sa msukuma u ataweka hu nk
Wewe unazungumzia lafudhi na siyo lahaja. Hili la kushindwa kutamka maneno ni eneo la lafudhi. Lafudhi inaathiriwa na asili ya mzungumzaji na mara nyingi huathiriwa na lugha ya kwanza ya mzungumzaji eg kisukuma. Wakati Lahaja ni lugha inayozungumzwa katika eneo fulani au na kikundi fulani cha watu, yenye tofauti kidogo au kubwa katika matamshi, msamiati, na sarufi. mfano kiswahili cha Unguja na kiswahili na Kilimanjaro. Bottom line ni kuwa shuleni tunakwenda kusoma kiswahili sanifu, hivyo basi kama nchi yetu ilivyo na mtaala mmoja wa kiswahili, hakuna excuse ya kukosea maneno kwenye kuandika. Unaweza kukubali makosa kwenye matamshi lakini siyo kuandika.
 
Mtu unaitwa Musa watu wa hovyo wanakuita Msa inakera sana
 
Back
Top Bottom